JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Picha ya mwisho kupiga Mwalimu Nyerere katika Maisha yake
Wakati Leo CCM inasherekea miaka 45 ya kuzaliwa Kwa Chama hicho,
Leo nimeamua kukuletea picha ya mwisho ya Mwalimu Nyerere,
Picha unayoiona hapo Chini ndio picha ya mwisho kupigwa na Mwalimu enzi za uhai wake,
Picha hii ilipigwa tarehe 17 September 1999 saa tatu na dakika ishirini za Tanzania,
muda mfupi kabla ya baba wa taifa kupanda ndege kuelekea London -Uingereza kwa matibabu,
hii ndiyo picha yake ya mwisho kupiga akiwa hai hapa duniani,
" Ninajua nitakufa sitapona nawaomba watanzania waipende nchi yao waipende Kama wanavyowapenda mama zao maana hawana nchi nyengine".
Huu ulikua wosia wa mwisho wa BABA WA TAIFA kwa Taifa lake.
Pumzika kwa amani Mwalimu Nyerere Baba wa Taifa la Tanzania.

View attachment 2108857
Hii picha sijui ni wapi, inaonekana sio mjini. Picha ya mwisho ilikuwa airport, anatoka kwenye Benz anaingia kwenye jengo VIP lounge, Ila sio hii, na hata kwenye picha alionekana amedhoofika.
 
Hii picha sijui ni wapi, inaonekana sio mjini. Picha ya mwisho ilikuwa airport, anatoka kwenye Benz anaingia kwenye jengo VIP lounge, Ila sio hii, na hata kwenye picha alionekana amedhoofika.
Hii ndio ya mwisho.
Screenshot_20230222-202441.jpg
 
#TBT Kutoka Maktaba ya Mhenga hii ilikuwa Mwaka 1955 Mwanasiasa Mkongwe Lawi Nangwanda Sijaona aliibiwa Baiskeli yake Dar Es Salaam na ikapatikana Bagamoyo Baiskeli hiyo alikabidhiwa Rafiki yake John Umi tarehe 1 November 1955 na Tanganyika Police, Kariakoo Division kwa kuwa Lawi Nangwanda Sijaona alirudi Newala na alikuwa anafanya Kazi za TANU huko Lawi na John walisoma wote Shule ya Sekondari ya Chidya Masasi na Minaki kipindi hiki Jeshi la Polisi Tanganyika lilikuwa na uwezo wa kufuatilia na kukamata Baiskeli tofauti na sasa Watu wengi wanaibiwa Magari na hayapatikani kwa kweli tumetoka mbali kwa hisani ya Adam Sijali Nangwanda Sijaona.
FB_IMG_1678409803047.jpg
 
Back
Top Bottom