JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Watangazaji wa Radio Tanzania walikuja Cairo Egypt kujifunza mambo ya Television miaka ya 80 mmoja kati ya hao ni Abdallah Mlawa,
Yupo na Segumba mtoto wa mzee wa Simba Habibu Segumba au Underline,alikuwa na Taxi yake 404 Simba lialia alikuwa anasahau mpaka wapi ka Park gari,mwingine ni msafiri mwenzetu wakuitwa Lupa....Down Town Cairo.
May be an image of 3 people and people standing
 
JELLA MTAGWA: Mchezaji aliyewahi kuwika akiichezea Timu ya Yanga pia Timu ya Taifa kwa mafanikio makubwa mno. Kwa kuheshimu mchango wake kwa Taifa, Shirika la Posta na Simu Tanzania wakati ule likaweka picha yake ktk moja ya STEMPU za Shirika hilo kwa ajili ya barua.
No photo description available.
 
Kutoka Maktaba ya Mhenga hii ilikuwa Mwaka 1955 Mwanasiasa Mkongwe Lawi Nangwanda Sijaona aliibiwa Baiskeli yake Dar Es Salaam na ikapatikana Bagamoyo Baiskeli hiyo alikabidhiwa Rafiki yake John Umi tarehe 1 November 1955 na Tanganyika Police, Kariakoo Division kwa kuwa Lawi Nangwanda Sijaona alirudi Newala na alikuwa anafanya Kazi za TANU huko Lawi na John walisoma wote Shule ya Sekondari ya Chidya Masasi na Minaki kipindi hiki Jeshi la Polisi Tanganyika lilikuwa na uwezo wa kufuatilia na kukamata Baiskeli tofauti na sasa Watu wengi wanaibiwa Magari na hayapatikani kwa kweli tumetoka mbali kwa hisani ya Adam Sijali Nangwanda Sijaona.
May be an image of text
 
Back
Top Bottom