JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Hii picha sijui ni wapi, inaonekana sio mjini. Picha ya mwisho ilikuwa airport, anatoka kwenye Benz anaingia kwenye jengo VIP lounge, Ila sio hii, na hata kwenye picha alionekana amedhoofika.
 
Office yao ilikua inajisughulisha na nini au kuuza ma-cheni kama jina linavyojieleza ?
Alikuwa na bar maarufu sana mkabala na bondeni hotel.. Bar yake asilimia 50 ya wateja wake walikuwa ni maahoga na machangu.. Jina la macheni lilitokana na kupenda kuvaa cheni nyingi shingoni halafu kubwakubwa
 
#TBT Kutoka Maktaba ya Mhenga hii ilikuwa Mwaka 1955 Mwanasiasa Mkongwe Lawi Nangwanda Sijaona aliibiwa Baiskeli yake Dar Es Salaam na ikapatikana Bagamoyo Baiskeli hiyo alikabidhiwa Rafiki yake John Umi tarehe 1 November 1955 na Tanganyika Police, Kariakoo Division kwa kuwa Lawi Nangwanda Sijaona alirudi Newala na alikuwa anafanya Kazi za TANU huko Lawi na John walisoma wote Shule ya Sekondari ya Chidya Masasi na Minaki kipindi hiki Jeshi la Polisi Tanganyika lilikuwa na uwezo wa kufuatilia na kukamata Baiskeli tofauti na sasa Watu wengi wanaibiwa Magari na hayapatikani kwa kweli tumetoka mbali kwa hisani ya Adam Sijali Nangwanda Sijaona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…