JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

FB_IMG_1690526496200.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
TUNAMKUMBUKA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE. JE TUNAMFAHAMU MAMA YAKE MZAZI?

UNAMJUA BIBI CHRISTINA MGAYA WA NYANG'OMBE?

Ameandika Francis Daudi

Hayati Bibi Christina Mgaya wa Nyang'ombe alikuwa mke wa tano(Kati ya wake 22) wa chifu Nyerere Burito. Hayati Bi. Mgaya ndiye mama mzazi wa baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Chifu Burito alikuwa kiongozi wa kabila la Zanaki wa Butiama wakati wa Ukoloni. Alitawala kuanzia 1912 mpaka mwaka Machi 30, 1942 alipofariki.

Inasemekana Bibi Mgaya wa Nyang'ombe alizaliwa mwaka 1897. Alijaaliwa kupata watoto sita ambao ni Nyerere (Julius)Kambarage, Nyangete Nyerere, Nyakahu Nyerere, Nyakigi Nyerere, Kizurira (Joseph)Nyerere na kitindamimba aliyeitwa Kiboko (Josephat) Nyerere. Hivyo utaona mama huyu alikuwa na kazi kubwa ya malezi kwa watoto, akiwemo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alikuja kuwa baba wa Taifa letu.

Kwa sifa zake, Inaelezwa Bibi Christina Mgaya alikuwa mtu mwenye busara kubwa na aliyependa kuongea kwa mafumbo yenye kubeba mafunzo Fulani. Hata Mwalimu Nyerere alipokuwa raisi bado bibi huyu aliendelea kushiriki shughuli za shamba na hata sherehe za utamaduni na watu wengine hapo Butiama kabla ya umauti kumkuta mwaka 1997.

Kulingana na Mzee Peter DM Bwimbo Katika kitabu chake kinachoitwa: ‘MLINZI MKUU WA MWALIMU NYERERE’ anaeleza kwamba Mwalimu Nyerere alimuheshimu sana mama yake, Bibi Mgaya Nyang’ombe. Mara zote akiwepo Butiama, aliamka mapema kabla ya kufanya chochote alienda kumsalimu. Hata kulipotokea jambo ndani ya familia, aliheshimu kauli ya mama yake bila kujali madaraka yake kama raisi wa nchi.

Inaaminika alifariki akiwa na miaka 105( mwaka 1997) amezikwa karibu kabisa na kaburi la Chifu Nyerere Burito. Ingawa maandiko mengine yanaeleza kuwa alizaliwa mwaka 1897 hivyo basi kwa mwaka 1997 angekuwa na miaka 100.

Kiufupi, Bibi Christina Mgaya wa Nyang'ombe ni sehemu muhimu sana katika uandishi wa historia ya Tanzania. Yeye ni kati ya WANAWAKE waliosahaulika kabisa katika kurasa za historia yetu lakini ujenzi wa TAIFA hili uliitaji mtu aliyepitia malezi muhimu hasa utotoni. Ambaye alifunzwa tangu utotoni kupenda watu, kutetea watu na kuamini katika Misingi ya HAKI na USAWA.

Bila shaka elimu hii hakuipata kwa kumsoma KARX MARX au PLATO, ilianzia kwa mama ambaye hakupata kabisa elimu rasmi. Ila mwenye ucheshi, mkarimu na upendo wa hali ya juu. Huyu ndiye mama yake Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
FB_IMG_1690609019614.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Mohammed Shebe"
(Mwenye kofia nyeusi), Wahenga huyu ndie mpiga picha wa kwanza wa "Baba wa Taifa"

Mohammed Shebe amepiga picha nyingi za wakati wa TANU, hata siku ya kwanza Mwalimu anatoka hadharani kuhutubia Mnazi Mmoja, Mohammed Shebe alipiga picha. Picha ya Pili, mwenye begi.
FB_IMG_1691141404756.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
ENDELEA KUPUNZIKA KWA AMANI
BAVON MARIE MARIE

Bavon Marie Marie, mdogo wake Franco Luambo,
Alizaliwa 27/05/ 1944 na kufariki 05/08/1970

Alizaliwa katika jiji la Kinshasa na kupewa jina la Siango Bavon Marie Marie. Alipokuwa mdogo alikua mtukutu nawenye akili sana, hali hii ilimfanya akajulikana sana kwenye eneo alilokulia wilaya ya Bosobolo.
Kadri alivyokuwa akaanza kuishi maisha ya makeke zaidi kwa kuwa mlevi mzuri wa pombe na msafi aliyejiichubua kisawasawa kama ilivyokuwa desturi ya vijana wa Kinshasa wakati ule. Kama alivyokuwa kaka yake Franco Makiadi naye alikuwa mpiga gitaa mzuri sana. Alipigia bendi kama Cubana Jazz akiwa na mwanamuziki Bumba Massa, akapigia Orchestre Jamel kabla ya kuingia Negro Succes, bendi ambayo ilianzishwa 1960 za Vicky Longomba (Baba wa Awilo Longomba). Vicky aliwahi kuwa mmoja wa wanamuziki wa Tp Ok Jazz, yeye pamoja na wenzie Leon’ Bholen’ Bombolo, na mwimbaji mwenzie Hubert ‘Djeskin’Dihunga, mpiga sax Andre Menga, rhythm Jean Dinos, mpiga bezi Alphonse ‘Le Brun’ Epayo, mpiga drum Sammy Kiadaka na mwimbaji mwingine Gaspard ‘Gaspy; Luwowo wakaanzisha hiyo bendi kali kabisa Negro Succes . Bavon akawa mpiga gitaa wa bendi hii baada ya mwaka 1965, yeye na mwenzie Bholen wakawa viongozi na masupastar wa wakati huo kwa vijana wa Kinshasa. Pamoja na kuwa kaka yake Franco ndie aliyekuwa akijulikana kama Mwalimu Mkuu wa Rhumba la Kongo yeye pia alikuwa kipenzi vijana kutokana na upigaji wa solo lake lililokuwa na uchangamfu zaidi.

Mnamo Agosti 5, 1970, Bavon Marie Marie alifariki katika ajali mbaya ya gari. Usiku wa maafa ulianza na mzozo kati ya Bavon na kaka yake Franco ambapo Bavon alimshutumu kaka yake kwa kulala na mpenzi wake, Lucy. Na iliishia kwa Bavon Marie Marie kufa kwa ajali ya gari na Lucy akiwa hana miguu. Alikuwa na umri wa miaka 27 pekee yake alipofariki lakini athari na mchango wake katika muziki wa Kongo hautasahaulika kamwe.

Marehemu Siongo Bavon Marie Marie alimpenda sana Lucy lakini inasemekana kwamba mwanamke huyu pia alichumbiana na mwanasoka anayeitwa Jean Kembo ambaye alikuwa mshambuliaji wa Vita ya Vita na timu ya Taifa ya Zaire The Leopards. Jean Kembo alikuwa mpinzani wa Bavon Marie Marie juu ya Lucie huyu mrembo. Hii ndio sababu iliyomfanya marehemu Bavon kutoa nyimbo kadhaa katika utunzi wake kwa mrembo huyo zinaonyesha jinsi alivyokuwa akimpenda sana. Inasemekana kwamba kaka mkubwa wa Bavon Marie Marie Franco Luambo Makiadi pia alichumbiana na Lucie, mbali na kwamba pia alichumbiana na mwandishi wa habari maarufu huko Kinshasa.
Marehemu Siongo Bavon Marie Marie alikuwa ameacha nyimbo ambazo wengi wanadhani alikuwa na utangulizi wa kifo chake. Nyimbo zake kama "Maseke ya meme", "Libanga na libumu" au "Mamona mbua" zilizoimbwa kwa Kikongo. Siongo, anatoa hisia kuwa alijua anakaribia mwisho wake, kwani uchungu uliobebwa na tungo zake ulikuwa wa kweli.
FB_IMG_1691559765741.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom