JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JE UNAJUA: Kanisa la kwanza la Kikristo nchini Tanganyika/ Tanzania lilianzishwa na kujengwa kule Magila Msalabani, Muheza mkoani Tanga mwaka 1843? Hili kanisa lilianzishwa na Johann Kraft na lilikuwa kanisa la ki-Anglikana. Pia shule ya kwanza Tanganyika ilianzishwa hapa pia mwaka 1886. Hii sehemu ya Magila Msalabani ipo hadi leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo Isuzu ilikuwa ikipiga ruti za Buguruni na Posta, na ilikuwa ikilala Ilala, long time Leo umenikumbusha, shukurani sana
 
Mnaikumbuka album hii COMME UN ya mwanamuziki Jean Baron akishirikiana na kundi la Loketo? Ilitoka mwaka 1991 ikiwa na nyimbo 6; Mami Lolo,Nabeleli,Koudia ndambou,Pantalon Moriba,Comme Un..na Lutter Lutter. Hakika hii album iliziteka hisia za wapenda muziki wengi ilihusisha wanamuziki maarufu kama vile Aurlus Mabélé, Lucien Bokilo, Djunny Claude, Dally Kimoko, Awilo Longomba nk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikuwa ni miaka ya 1960. Hongera kwa uangalizi mzuri sana wa hii mashine. Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akipeana mkono na Dereva wa Treni hii ya makaa ya mawe ama Gari moshi kama zilivyofahamika kutokana na kutumia makaa ya mawe kufanya kazi. Nyingi zilipewa majina ya Kizawa kama hiyo TANGANYIKA, Nyingine ziliandikwa, SUKUMA, CHAGA, ZIGUA yaani makabila ya hapa nchini. Karibu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…