JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Enzi zetu akija mkubwa wa nchi ya kigeni, shule zinafungwa na tunasimamishwa mitaani kumpokea.
FB_IMG_1703568153789.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
JE UNAJUA: Kanisa la kwanza la Kikristo nchini Tanganyika/ Tanzania lilianzishwa na kujengwa kule Magila Msalabani, Muheza mkoani Tanga mwaka 1843? Hili kanisa lilianzishwa na Johann Kraft na lilikuwa kanisa la ki-Anglikana. Pia shule ya kwanza Tanganyika ilianzishwa hapa pia mwaka 1886. Hii sehemu ya Magila Msalabani ipo hadi leo.
FB_IMG_1703591165084.jpg
FB_IMG_1703591162487.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikuwa mwaka 1986. Hayo ni maeneo ya Posta ya zamani jijini Dar es salaam na mbele hapo linaonekana Kanisa la Lutherani la Azania Front. Hapo barabarani naona daladala ISUZU ELF ikizunguka kuja huku stendi baharini kwenye Mikungu kupakia abiria. Pichani pia naona gari ndogo nyeupe ikiwa imepaki hapo na vijana wa zamani nao hapo wakiwa wamekaa kwenye ukuta. Karibu sana.View attachment 2852393

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo Isuzu ilikuwa ikipiga ruti za Buguruni na Posta, na ilikuwa ikilala Ilala, long time Leo umenikumbusha, shukurani sana
 
Mnaikumbuka album hii COMME UN ya mwanamuziki Jean Baron akishirikiana na kundi la Loketo? Ilitoka mwaka 1991 ikiwa na nyimbo 6; Mami Lolo,Nabeleli,Koudia ndambou,Pantalon Moriba,Comme Un..na Lutter Lutter. Hakika hii album iliziteka hisia za wapenda muziki wengi ilihusisha wanamuziki maarufu kama vile Aurlus Mabélé, Lucien Bokilo, Djunny Claude, Dally Kimoko, Awilo Longomba nk
FB_IMG_1703825918913.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikuwa ni miaka ya 1960. Hongera kwa uangalizi mzuri sana wa hii mashine. Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akipeana mkono na Dereva wa Treni hii ya makaa ya mawe ama Gari moshi kama zilivyofahamika kutokana na kutumia makaa ya mawe kufanya kazi. Nyingi zilipewa majina ya Kizawa kama hiyo TANGANYIKA, Nyingine ziliandikwa, SUKUMA, CHAGA, ZIGUA yaani makabila ya hapa nchini. Karibu sana.
FB_IMG_1703930649792.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom