1. Hiyo picha ni msafara kwenda Monduli, Arusha kumzika aliyekuwa Waziri Mkuu wa tatu wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine, 1984. Edward Moringe Sokoine alifariki April 12, 1984 kwa ajali ya gari. Hapo ni Uhuru Road, Arusha siyo Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
2.
April 12, 1984 Edward Moringe Sokoine akitokea Dodoma kwa gari yake, Mercedes-Benz na msafara mkubwa uliosheheni magari ya usalama, aligongwa na gari (Land Cruiser) mali ya DUMISAN DUBE raia wa South Africa na kupelekea kifo chake.
3. Dumisani Dube alikuwa akitokea Mazimbu, alibeba chakula kwa ajili ya wakimbizi wenzake wa kisiasa kutoka South Africa waliokuwa wameweka kambi yao eneo la Dakawa. Waliendesha harakati zao za kupigania uhuru kutoka eneo la Mazimbu na Dakawa.
4. Ajali ilitokea saa 7 mchana. Msafara wa Sokoine ulikuwa ukitoka bungeni, Dodoma. Baada ya gari la Sokoine kupata ajali, magari mengine yaliyokuwa nyuma yaligonga gari hilo likiwa chini. Hali iliyochangia Sokoine kuumia zaidi na maumivu pamoja na dereva wake.
5. Dumisani Dube aliyumbisha gari na kumzubaisha dereva wa gari la Sokoine na hivyo kuacha njia na kupinduka. Maafisa usalama walimbeba Sokoine na dereva wake hadi Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu. Wote walikuwa hawajitambui.
6. Dumisani Dube alikuwa mwanachama wa African National Congress (ANC) na mpigania uhuru wa South Africa. Gari lake liligonga gari la Edward Moringe Sokoine eneo la Luhindo, Dakawa, Morogoro. ANC walifikiri uhusiano wao na Tanzania utatereka baadae.
7. Kumbuka; Wafuasi wa African National Congress (ANC) walikuwa wameweka kambi Mazimbu na Dakawa, Morogoro. Dumisani Dube alikuwa raia RSA. Rais wa ANC, Oliver Tambo na SG, Alfred Nzo walikwenda Arusha kuwakilisha ANC katika msiba wa Sokoine.
8. Dumisani Dube, ambaye alikimbilia Tanzania kutoka Afrika Kusini miaka ya ubaguzi na kujiunga na ANC, kundi linalopigana na ubaguzi wa rangi Afrika Kusini, alikiri shtaka la kuua bila kukusudia na kuomba msamaha kwa mahakama kwa kusababisha ajali hiyo.
9. Dumisani Dube hakuwa na leseni ya udereva (driving license) na alikiri kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha ajali. Kesi hiyo ilifanyika Morogoro. Dumisani Dube alihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 13 gerezani kwa kusababisha ajali na kifo.
10. Dumisani Dube alikuwa akiendesha Toyota Landcruiser 1F. Gari hizo zilipachikwa jina la Dumisani Dube baada ya kifo cha Edward Moringe Sokoine. Alishikiliwa kwa muda, baadae alichiwa kwa msamaha na kurejeshwa nchini kwao, South Africa.
PS; Aina ya kifo chake, kwanini kuna hisia za kupangwa na siyo ajali, kwanini inahusisha succession struggles kuelekea 1985? Huo ni mjadala mwingine mpya wa muda mwingine. Huko tunaweza kuwajadili Rashid Kawawa, Aboud JUMBE na Cleopa Msuya na wengine.
MMM, Brigedia Mtikila.