View attachment 1743149
Huyu tumbili anayeitwa Jackie, aliyepewa cheo cha Koplo baada ya Kuhudumu Kama Mwanajeshi Katika Jeshi la SA Lililoingia Vitani Miaka ya 1910.Alishonewa Sare za Kijeshi,Akiwa Vitani Jackie Alipigwa Risasi na Kuumia, Alirudi Vitani na Kufariki Mwaka 1921.Koplo Jackie alikuwa tumbili katika jeshi la Afrika Kusini wakati wa Vita ya kwanza ya dunia 1910s. Alifanywa mascot wao wakati mmiliki wake Albert Marr alipoandikishwa kwenda vitani, na asingemuacha Jackie nyumbani, ilikuwa lazima afuatane naye.Jackie alipata majeraha wakati wa vita kama vile kupigwa risasi begani na kupigwa risasi nyingine katika mguu wa kulia. Jackie alifundishwa kupiga saluti kila alipomuona afisa mkuu wa kikosi.Baada ya vita Jackie alipewa heshima kwa ushirika wake, na akapewa medali ya huduma ya wananchi wa Pretoria, baadaye akafa kwa kuungua na moto nyumbani, ilikuwa ni miaka kadhaa baada ya kutoka vitani.
View attachment 1743151View attachment 1743153