JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

D7358CB7-6E5D-43BA-AA64-7AC171787705.jpeg

JPM akiwa Rais akipanda T1
 
Sijui nani anakumbuka ile meli iliyokuja kutusaidia Patrol miaka ya 2000 mpaka tukakamata wavuvi haramu (Samaki wa Magufuli) wakati JPM akiwa wizara ya Uvuvi na Mifugo

Basi hii ni Meli kubwa ya kufanya doria baharini (Offshore Patrol Ship) inayomilikiwa na Serikali ya South Africa na ilikuja kwa ushirikiano wa SADC

Hii meli ilianza kuundwa mwaka 2003 na ilipewa jina kwa heshima ya huyu mama inaitwa Sara BaartmanView attachment 1532996View attachment 1532997
Mmh mkuu au mi ndo sijakuelewa? imeundwa mwaka 2003, ila kufanya doria ocean sea ikaja mwaka 2000 ngachoka hoi
 
Dah! kweli ya kale ni dhahabu, katika kupitia pitia huu uzi kuna mkoti wa suti nimeuona nimejikuta nacheka kwa sauti.
 
Mmh mkuu au mi ndo sijakuelewa? imeundwa mwaka 2003, ila kufanya doria ocean sea ikaja mwaka 2000 ngachoka hoi
Tofautisha miaka ya 2000 na mwaka 2000(Labda sijui kiswahili chake 2000s)

Mtu akisema miaka ya 2000 manaake hajataja tarehe husika ila ni kuanzia 2000-2010, akisema miaka ya 2010 ni kuanzia 2010-2020 haswa pale anapokua hana uhakika na tarehe. Mengine unajiongeza


Nilikua sina tarehe ya uhakika ni lini sikua na muda wa kufanya research kabisa ila ilikuja Bongo March 2009

Natumaini umeelewa sasa
 
View attachment 1532945
Sara Baartman aka Hottentot Venus(1979- December 29 1815)
STORI YA KUSIKITISHA

Alikamatwa kama mtumwa huko Afrika ya kusini na alishikiliwa kwa muda kadhaa kabla ya wale wamiliki wa watumwa kugundua kwamba ana maumbile ya ajabu sana ambayo hawajawahi kuyaona. Akiwa na wowowo kubwa na matiti makubwa sana.Wakaanza kumtumikisha kingono na inakadiriwa alibakwa na kunyanyaswa kijinsia mara 400 wakaona hio haitoshi wakampeleka Paris France ambako walianza kumfanyia maonyesho kama zoo wakimzungusha mijinmbalimbali na wanaume wakija kumshangaa maumbile yake na mwenye hela anamnunua kwenda kulala nae.Alitumika kwa njia hiyo mpaka akachoka sana na akaanza kudhoofika na baadae alifariki. Uchunguzi baada ya kifo(autopsy) unaonesha kwamba alikua na inflammatory ailment, smallpox, syphilis, mild yeast infection na maambukizi mengine mengi ya bacteria.Haikuishia hapo baada ya kifo chake Dec 1815 waliukata kata mwili wake(Disection) wakatoa Ubongo wake, skeleton yake na sehemu za siri pamoja na nyonyo wakzaiweka Makumbusho(Paris Museum) kutangaza mwanamke aliyekua na maumbile ya ajabu mpaka mwaka 1974 nchi mbalimbali zilipoanza kupiga kelele juu ya udhalilishaji huo na hatimaye mwaka 2002 mwili wake ulirudishwa kwa Afrika ya Kusini na kuzikwa kwa heshima
View attachment 1532965View attachment 1532966View attachment 1532967View attachment 1532968View attachment 1532969
cc Rostema utakuja kuongezea nyama na mie nimeandika fasta fasta #bluemonday si unajua
Wazungu washenzi sana

Jr[emoji769]
 
Back
Top Bottom