JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Alitoa vitu vkali lakini hakudumu sana, R.I.P Mpongo Love.
FB_IMG_1695551836184.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
JE UNAJUA Kituo cha Polisi cha Selander Bridge zamani ilikuwa ni hoteli moja maarufu sana?

Jengo hili zamani ilikuwa ni hoteli maarufu iliyokuwa inaitwa “Sun and Sands Hotel”
iliyokuwa inamilikiwa na familia ya Habib Punja waliokuwa mabepari wakubwa wa kihindi miaka ya 1920- 50. Hotel ilijengwa mwaka 1949. Habib Punja alikuwa mfanyabiashara mkubwa aliyekuwa na biashara ya viwanda vya kutengeneza sabuni (1933), baadae akawa kwenye milling (1941) na baadae akawa kwenye biashara ya vifaa vya ujenzi (building materials) na urban property. Jengo lingine maarufu lililokuwa linamilikiwa na hii familia ni Jengo la Habib Punja Star Building lililokuwa mtaa wa Aggrey na Indira Gandhi kabla ya kuvunjwa mwaka 2008.

Hii hoteli ilikuja kutaifishwa na kuchukuliwa na serikali baada ya makomando wa kikaburu kulipua daraja la Selander, Nyumba ya Balozi wa Uingereza pale Toure Drive na Oil Depot Kurasini mwaka 1972. Makomando hawa (South African Special Forces Brigade-RECCE) waliitumia fukwe mbele ya hili jengo kujitayarisha na mission yao. Baada ya huu mkasa ndo serikali ikaamua kuongeza ulinzi na ikajenga Kituo cha Polisi cha Selander Bridge na hili jengo likataifishwa.
FB_IMG_1695644528344.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili ni gari la Waziri mkuu marehemu Sokoine baada ya kupata ajali mwaka 1984. Sikuwepo wakatu huo, nilikuwa bado sijazaliwa ni tukio natamani kujua undani wake, ilikuwaje msafara wa waziri mkuu ukapata ajali wakati tunajua jinsi misafara ya viongozi wakuu wa kitaifa kama Rais, makamu na Waziri mkuu inavyolindwa kwa nguvu zote za dola. Mliokuwepo mlioshuhudia hili tukio la kihistoria,

a) Chanzo cha ajali kilikuwa ni nini? Ajali ilitokea wakati gani na eneo gani?

b) Waziri mkuu Sokoine alipoteza maisha palepale katika eneo la tukio au alifariki akiwa hospitali?

c) Kuna wengine waliopoteza maisha katika ajali hiyo zaidi ya Waziri mkuu?

d) Ni nani aliyezembea hadi Waziri mkuu akapata ajali na kupoteza maisha? Alichukuliwa hatua gani?

e) Je gari la Waziri mkuu lilikidhi vigezo na viwango vya kiusalama kama kuwa na airbags, bodi imara la chuma kigumu nk?

f) Kuna uchunguzi wowote uliofanyika kubaini kama kulikuwa na njama au hila? Majibu ya uchunguzi yalikuwaje?View attachment 2765970

Sent using Jamii Forums mobile app
Mshana Jr, mwaka 1984 hujazaliwa wewe? Kwa hiyo umezaliwa 2000 na ngapi?
 
Mbaraka Mwishehe....jabari la muziki.....

•Afrika hoyeee
•Akula mwembe Songo
•Amina Mpenzi
•Baba mdogo
•Betty
•Bibi wa watu
•Biverina
•Chakula bora
•Choyo uache
•Daktari ni mimi
•Dokta kleruu
•Dawa ya mapenzi
•Esta wangu
•Ewe mwana
•Fujo Acha
•Jirani nisaidie
•Jogoo la shamba
•Kanuni za afya
•Kasema hakutaki
•Kazi ndio msingi
•Kibena
•Kifo cha karume
•Kifo cha pesa
•Kigeugeu
•Kilichochokuzuzua
•Kwela Africa
•Makao makuu dodoma
•Mapenzi shuleni
•Mapenzi yananitesa
•Mashemeji Wangapi
•Mashetani
•Masika Mtindo mpya
•Masikitiko yetu
•Matilda huna siri
•Matusi ya nini
•Miaka kumi
•Morogoro
•Mshenga
•Mtaa wa saba
•Mwongozo wa Tanu
•Nalilia raha
•Ni siku nyingi
•Nikupendeje
•Niliota ndoto
•Nimechoka kusemwa
•Nipeleke nikashuhudie
•Nisalimie wanazaire
•Nitaiandika Talaka
•Nitamtuma Mshenga
•Pesa
•Picnic Ya volcano
•Pole dada
•Poleni Rufiji
•Posa
•Regina
•Roho ndio muamuzi
•Safari sio kifo
•Sarakasi ya yasinta
•Shida
•Siku Mingi
•Sululu ya Moro
•Tamaa ya kuku
•Tambiko la wahenga
•Tina turudiane
•Tunawapongeza wanasoka
•Uaminifu Nimeutambua
•Ugeni shida
•Ugeni tabu
•Ukombozi wa Africa
•Unanitafutia nini
•Urafiki mwisho wa mwezi
•Utamaduni
•Viongozi wetu
•Waandishi wa magazeti
•Watalii
•Zawadi kwa Rais.

FB_IMG_1696569029289.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom