JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

FB_IMG_1698644210271.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo miaka 10 toka mwamba huyu wa utangazaji Julius Omang’ere Nyaisangah afariki. Nyaisangah alikuwa mmoja wa watangazaji hodari sana mwenye sauti na matamshi laini na matamu sikioni kwa msikilizaji.

Endelea kupumzika kwa amani brother ukiwa na timu rtd- Nadhir Mayoka, Hendrix Michael Libuda, Idd Mchatta,Ahmed Jongo, Siwatu Luwanda, Salama Mfamao, Hassan Mkumba, Juma Ngondaye, Nelly Kidela, David Wakati, Omar Jongo, Sarah Dumba, Batty Kombwa,Halima Mchuka, Suleiman Hegga na wengineo.

Pia wasalimie team IPP MEDIA wote huko Mwenyekiti Reginald Mengi, Rodney, John Ngahyoma, Misanya Bingi, Moses Justine-Papaa Mo, Isaac Muyenjwa Gamba, Robert Mbando, Baba T, Rehema Mwakangale, Oscar Mirindo, DJ Rankim Ramadhan, Dj Rico na wengineo. Nyote tunaendelea kuwakumbuka kwa mchango wenu mkubwa kwenye tasnia hii.
FB_IMG_1698644519400.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu anaitwa THEKLA MGAYA jina la usanii anaitwa AISHA WA MAMBO HAYO
Ndiye wanzilishi wa kundi la mambo hayo akiwa na sumbi na bocha baadaye akaja waridi
Baadaye wakatoka sumbi na bocha wakaja bishanga na richi
FB_IMG_1698644717313.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
"KOROKORO",
Wale Nduguzangu Wahenga wa Kinondoni, Magomeni na ilala wanaukumbuka mchezo huu. Kulikuwa kunawekwa meza kubwa ambayo ina vyumba vidogo vidogo vyenye michoro au namba zinazofanana na hizo zilizopo kwenye kete hizo pichani.

Kucheza kwake ilikuwa kila mchezaji, anachukua pesa yake na kuweka mezani kwenye chumba ambacho kina namba au picha inayofanana na hizo za kwenye kete kujaribu bahati yake. Kete hizo pichani huchukuliwa na kuwekwa kwenye kopo na Mchezeshaji halafu hutingishwa zikiwa ndani ya kopo na kumiminwa mezani.

Namba zitakazoonekana juu ya kete kama hivyo hapo pichani ndiyo namba za ushindi. Na wewe kama uliweka pesa yako kwenye chumba chenye mchoro au namba inayo fanana na hizo zilizopo juu ya kete kama hapo pichani, basi utakuwa umevuna ulichopanda, utapata nyongeza ya kiasi fulani cha pesa, kama hakuna basi pesa yako itakuwa imeliwa.

Ukipata bahati basi kama uliweka Shilingi moja unapata shilingi tano au mpaka shilingi kumi, hiyo ni kutokana na meza uliyokwenda kucheza. Waliopata pesa walipata na wengine tuliondoka vichwa chini, inafikia kipindi unaliwa pesa zote sasa unamuomba mchezeshaji wa korokoro akutafutie nauli japo na wachezeshaji wa korokoro nao sikunyingine walikuwa wanaliwa pesa mpaka mtaji unakwisha. Dah hatari kwelikweli.
FB_IMG_1698645385451.jpg
FB_IMG_1698645379986.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ndio JUKEBOX ni mashine ilikuwa katika baa ambayo hucheza muziki uliorekodiwa kwenye santuri wakati sarafu imewekwa ndani yake. Vijana wazamani wanaelewa...
FB_IMG_1698645657446.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom