JF Scheduled Maintenance - October 2020

JF Scheduled Maintenance - October 2020

Wakuu,

Kuna maboresho yanafanyika chini kwa chini, search functionality inaweza isifanye kazi vema kwa siku moja au mbili (tangu jana).

Tunatarajia hadi kesho muda kama huu mambo yatakuwa yamerejea sawa.

Baada ya marekebisho kadhaa, kutakuja features ndani ya JF na urahisi na usalama zaidi wa matumizi ya platform yetu.

Tunafanya haya ili kuendana na teknolojia ya habari na usalama wa mitandao.

Mtarajie mabadiliko gani? Yatajionyesha, si kwenye mwonekano bali kwenye User Experience. Wenye uoni hafifu wamefikiriwa na sasa watazidi kuitumia JF bila vikwazo.

Tunashukuru kwa uvumilivu na ushirikiano mnaotupa.
Always JF is ahead on customer care.

Thank you Team kwa kutujali sisi watu wadogo wa nchi hii
 
Nimeona mkwamo kwenye search engine kumbe kuna maboresho[emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Bado nakumbuka ile JF "seizure" ya 2015 .......mwaka huu sijui itakuwaje tena!?
 
Nimejaribu kuweka uzi wangu mpya umegoma kabisa kuonekana hili nalo vipi?
 
Mkuu wangu,

Hawa hasa ndio tunawalenga. Kwenye matengenezo yetu tunajaribu kuboresha zaidi namna ya kuweka attachments ili wadau wanapofanya hivyo iwe rahisi kwa wenzetu.

KWA WENGINE:
JF ni tovuti ambayo kwa Tanzania imekuwa ya mfano kwa kuwapa fursa wenye changamoto ya kuona (wengine huwaita vipofu) ili nao washiriki kwenye mijadala anuai.

Mnaombwa mnapoweka attachments mziweke kama “full attachments” na mkiweza tafadhali wekeeni na caption ili wenzetu wenye changamoto ya kuona au wenye uoni hafifu washiriki nasi.

Technologically tumejitahidi kufanya inclusion lakini wadau huenda hamkujua hili hivyo kuwapa wakati mgumu wenzetu kusoma attachments.

Picha zikiwa attached JF wenzetu bado wanaweza kujua lakini caption zinawarahisishia sana.

Sina hakika kama mdau niliyemnukuu ana changamoto hii lakini ni “wake up call” kwetu sote kuwajali na kuwarahisishia kushiriki nasi.

Asante
Nikushukuru mkuu kwa maelezo yako mujarabu kabisa.

Binafsi mimi ni mtu asiyeona. Unayosema ni sahihi kabisa. Nimekuwa nikitumia mtandao huu kwa zaidi ya miaka sita kwa ID tofauti.

Nawapongeza sana maana kwa Tanzania ndio site na App ambayo iko accessible kwetu watu tusioona. Ni tatizo kubwa sana hapa Bongo masuala ya kiteknolojia tunasahaulika sana. Ila ninyi mnakuwa makini na hata kama tukiwasilisha tatizo yetu humu hushughulikiwa haraka.
 
Aisee!! Big up sana jf founders!

Unforgetable
 
Mkuu wangu,

Hawa hasa ndio tunawalenga. Kwenye matengenezo yetu tunajaribu kuboresha zaidi namna ya kuweka attachments ili wadau wanapofanya hivyo iwe rahisi kwa wenzetu.

KWA WENGINE:
JF ni tovuti ambayo kwa Tanzania imekuwa ya mfano kwa kuwapa fursa wenye changamoto ya kuona (wengine huwaita vipofu) ili nao washiriki kwenye mijadala anuai.

Mnaombwa mnapoweka attachments mziweke kama “full attachments” na mkiweza tafadhali wekeeni na caption ili wenzetu wenye changamoto ya kuona au wenye uoni hafifu washiriki nasi.

Technologically tumejitahidi kufanya inclusion lakini wadau huenda hamkujua hili hivyo kuwapa wakati mgumu wenzetu kusoma attachments.

Picha zikiwa attached JF wenzetu bado wanaweza kujua lakini caption zinawarahisishia sana.

Sina hakika kama mdau niliyemnukuu ana changamoto hii lakini ni “wake up call” kwetu sote kuwajali na kuwarahisishia kushiriki nasi.

Asante
Inabido mseti kwamba, kama picha inapamdishwa humu basi automatically iwe full
 
Nimeona marekebisha ila upande wa kutoa video you tube kuweka humu naona imefutwa au kuondolewa au ni vile hatujajua kuendana na mabadiliko?
 
Back
Top Bottom