Ukweli kabisa sijaelewa, maana fb nina marafika 4900 na kwenye page kuna watu walio active kama 157 hivi nina miaka kama 5 natangaza kitu ninachokifanya au fani ninayoifanya tena kwa kutupia ujuzi mpya lakini sijawahi pigiwa hata simu ya kazi .sijui shida ipo wapi hapo
Ngoja nikupe darasa kidogo upande wa social media marketing na online business kiujumla....
Ipo hivi kuna marafiki wa kawaida wanaokufahamu kuwa wewe ni mtu fulani au mlisoma shule fulani... Yaani yeye anakuwa rafiki siyo kwasababu anapenda au kuvutiwa na huduma au Biashara unayofanya ila ukaribu fulani wa kijamii na wa kawaida tu.
Kwa upande wa Facebook page. Kuna followers wanao like page yako nao siyo kwasababu Wanapenda au kuvutiwa na huduma yako...
JUKUMU LAKO KUU NI LIPI?.
jukumu lako kuu ni kutengeneza mazingira ya kuamisha mitazamo ya hao marafiki na page followers wakuone wewe ni mtoa huduma au Mfanyabiashara ili waanze kuishi na wewe kama mtoa huduma na mteja na siyo RAFIKI wa kawaida tu.
Kumbuka katika hao marafiki na page followers siyo wote wana uwezo au uhitaji na hicho unachokifanya hivyo sasa ni jukumu lako wewe kuanza kutafuta wateja miongoni mwa hao marafiki na sehemu nyingine.
Unawapataje hao wateja au watu wanaopenda hicho unachokifanya ?
Hapo sasa ndipo ujuzi wa Digital Marketing upande wa social media unapoingilia kati...
Settings za page yako na muonekano wake uko vipi?
Profile yako inaongea nini kuhusu unachofanya? Yaani, Je naweza pitia profile yako nikaelewa unatoa huduma hii pasipo kuwa na haja ya kuuliza?
Mtego unaotumia kunasa wateja au watu watakao penda huduma yako na kuwa tayari kulipia ni upi?
Mfano wa mtego ni video, picha, makala au content ya aina yoyote yenye UJUMBE ambao watu unao walenga watafurahia na kuamua kukufuatilia zaidi page yako na mwisho wa siku kuwa wateja.
Miaka mitano mingi sana ungekuwa na uelewa mzuri kuhusu social media marketing ungefika mbali sana.
Niulize chochote kuhusu Digital marketing na kama kitakuwa ndani ya uwezo nitatoa ufafanuzi hapahapa.
Mengine zaidi karibu DM