Mac Alpho
JF-Expert Member
- Aug 5, 2019
- 13,953
- 27,825
Ni wazo zuri ila litafanikiwa kama tu hayo makubaliano yatafanywa kisheira (mikataba), hii itaondoa uwezekano wa hao mafundi kuleta unoko na hiyana pale ambapo watahisi unanufaika sana kuliko was (unawanyonya)Najua wengi wana akaunti katika mitandao ya kijamii; sasa ni wakati wa kutumia hiyo mitandao kuingiza pesa.
Anza hivi:-
No. 1
i. Fundi wa kupaua
- Tengeneza 'database' ya mambo yote yanayohusu ujenzi
- Ingia makubaliano na hawa mafundi:-
ii. Fundi wa plasta
iii. Fundi wa urembo-decoration
iv. Fundi wa kuskimu
v. Fundi wa ma-grill
vi. Fundi wa aluminium
vii. Wazibuaji wa vyoo
viii. Mafundi bomba
ix. Fundi umeme
x.Fundi wa kujenga
No. 2
- Ingia makubaliano na maduka ya vifaa vya ujenzi
- Ingia makubaliano na kampuni za mabati
- Ingia makubaliano na wanaokodisha vifaa vya ujenzi
No.3
- Ingia kwenye akaunti yako na tengeneza jina, mfano:- Equation x Bingwa wa ujenzi
- Alika marafiki wa kila namna kadri uwezavyo, na hakikisha kwenye akaunti yako una marafiki hata zaidi ya 10,000
- Akaunti yako iunge na magrupu mbalimbali
- Usiruhusu wale ulioingia nao makubaliano kufanya chochote kwenye akaunti yako
- Tangaza zile kazi zinazofanywa na watu ulioingia nao makubaliano ila tumia njia kuonekana wewe ndio unafanya, na mawasiliano yote yawe ni kwako.
- Na wale ulioingia nao makubaliano wanatakiwa waonekane wewe ndio umewaajiri, yaani wewe ndio boss wao.
- Anza kupokea 'order' na kula mafao
- Anza kumiliki kampuni kubwa kubwa
NB. Unaweza kutumia hii njia hata kwenye idara zingine si lazima, ujenzi.
Kawaida ya mbogo atakukubalia wakati wa kuanza project, utahangaika kutengeneza platform kwa zaidi ya hata miaka kadhaa ila wakati ambapo utaanza kuviona mafao lazima wakuletee nongwa za kuona kama unanufaika bure kupitia kwako.Kuepusha hilo,ni lazima uhakikishe unawafungisha mikataba yenye kuwabana haswa.
Sambamba na hilo wazo kama mtaji ukikua,si vibaya kufungwa hata kiwanda cha kufyatua mayofali ya block, na kufungua hardware za vifaa cya ujenzi ili hela isipotee kwenye circle kwenda kwingine.