Jiajiri kwenye hii biashara hata kama huna mtaji

Ni kweli kabisa, hata wakiwa kwenye payroll yako, hizi kazi zinawapa fursa kufanya kazi za ziada na kujiongezea kipato mbali na mshahara. Mnaweza kumaliza mwezi hakuna choo kilichoziba.
 
Napiga kazi ya skiming na upakaji rangi pia ninaujuzi wa ufungaji umeme na ufungaji mifumo ya maji kwenye nyumba, lakini sioni matokeo yoyote labda sijaweza kujitambua ninakwama wapi
Boresha ukurasa wako, na usialike marafiki ' watoto-kula kulala'. Alika watu wanaojitegemea wenye maamuzi,Pia onyesha picha za kazi zako zenye ubora
 
Kwa issue ya mitandao kwa bongo bado sana mwingine atakuuliza unanifahamu huwa naishia hapo
 
Nimekuelewa lakinibulimwengu tuliopo ningumu sana kuweka ushawishi kwa wateja ili hali anajuwa mtaani kwake yupo fundi furani kuliko akutafte wewe asiye kufahamu
Kwa ushuhuda mkuu, mimi huwa natumia mafundi wanaojitangaza mtandaoni,naona kazi zao, pia wananitumia zingine, tunaingia makubaliano, wanaanza safari, na kufanya kazi; nawe pia usikate tamaa, ongeza kasi ya kujitangaza
 
Kwa ushuhuda mkuu, mimi huwa natumia mafundi wanaojitangaza mtandaoni,naona kazi zao, pia wananitumia zingine, tunaingia makubaliano, wanaanza safari, na kufanya kazi; nawe pia usikate tamaa, ongeza kasi ya kujitangaza
Asante
 
Napiga kazi ya skiming na upakaji rangi pia ninaujuzi wa ufungaji umeme na ufungaji mifumo ya maji kwenye nyumba, lakini sioni matokeo yoyote labda sijaweza kujitambua ninakwama wapi
Wewe unatumia akaunti yako ya zamani ya kirafiki. Marafiki zako wa Facebook wako Namtumbo, Nanyumbu na Gwanseri alafu wewe uko labda Gongo la Mboto. Marafiki zako wengine ni watoto wa sekondari na pisi kali za 20s, hapo wateja unawapata vipi. Ukiwa na account Instagram au Facebook unafungua business one na unaweka ads za kuendana na sehemu unayotaka na umri wa unaowataka. Bila hivyo hutaona matokeo
 
Ushauri mzuri
 
Ngoja nikupe darasa kidogo upande wa social media marketing na online business kiujumla....

Ipo hivi kuna marafiki wa kawaida wanaokufahamu kuwa wewe ni mtu fulani au mlisoma shule fulani... Yaani yeye anakuwa rafiki siyo kwasababu anapenda au kuvutiwa na huduma au Biashara unayofanya ila ukaribu fulani wa kijamii na wa kawaida tu.

Kwa upande wa Facebook page. Kuna followers wanao like page yako nao siyo kwasababu Wanapenda au kuvutiwa na huduma yako...

JUKUMU LAKO KUU NI LIPI?.

jukumu lako kuu ni kutengeneza mazingira ya kuamisha mitazamo ya hao marafiki na page followers wakuone wewe ni mtoa huduma au Mfanyabiashara ili waanze kuishi na wewe kama mtoa huduma na mteja na siyo RAFIKI wa kawaida tu.

Kumbuka katika hao marafiki na page followers siyo wote wana uwezo au uhitaji na hicho unachokifanya hivyo sasa ni jukumu lako wewe kuanza kutafuta wateja miongoni mwa hao marafiki na sehemu nyingine.

Unawapataje hao wateja au watu wanaopenda hicho unachokifanya ?

Hapo sasa ndipo ujuzi wa Digital Marketing upande wa social media unapoingilia kati...

Settings za page yako na muonekano wake uko vipi?

Profile yako inaongea nini kuhusu unachofanya? Yaani, Je naweza pitia profile yako nikaelewa unatoa huduma hii pasipo kuwa na haja ya kuuliza?

Mtego unaotumia kunasa wateja au watu watakao penda huduma yako na kuwa tayari kulipia ni upi?

Mfano wa mtego ni video, picha, makala au content ya aina yoyote yenye UJUMBE ambao watu unao walenga watafurahia na kuamua kukufuatilia zaidi page yako na mwisho wa siku kuwa wateja.

Miaka mitano mingi sana ungekuwa na uelewa mzuri kuhusu social media marketing ungefika mbali sana.

Niulize chochote kuhusu Digital marketing na kama kitakuwa ndani ya uwezo nitatoa ufafanuzi hapahapa.

Mengine zaidi karibu DM
 
Dalwin nightmare.😄😄
 
Aisee sikujuwa haya before, sasa hapo kidogo umenipa mwanga. Ubarikiwe nitakucheki kwa maswala mengine ya ushauri
 
Ulishawahi kjiuliza, kwa nini vijana wadogo chini ya miaka 20 wanamiliki 'mansion' huko nchi za wenzetu?
Ulishawahi kujiuliza ni kwa nini wanyama na mashoga wana thamani kubwa huko nchi za wenzetu?
 
Nimekuelewa lakinibulimwengu tuliopo ningumu sana kuweka ushawishi kwa wateja ili hali anajuwa mtaani kwake yupo fundi furani kuliko akutafte wewe asiye kufahamu
Inaonekana haupo active, ushauri wangu jitahidi kupost kazi zako mara kwa mara na kwa lugha ya ushawishi bila kusahau namba zako za simu.
 
Ushauri mzuri sana ...ila wabongo wasivyojielewa ukimwambia akupe hela ili umsaidie process zote za digital marketing ili apate wateja wa kutosha, si ajabu akaanza kukuita tapeli
 
Ushauri mzuri sana ...ila wabongo wasivyojielewa ukimwambia akupe hela ili umsaidie process zote za digital marketing ili apate wateja wa kutosha, si ajabu akaanza kukuita tapeli
Kwetu haya mambo wanaoelewa na kuamini bado wachache.

Wengi wanajua tu mtandaoni kuna fursa ila hawajui hiyo fursa ipo vipi na inakuaje mpaka kupata matokeo kwa bundle la kawaida kabisa.

Ukikutana na mwenye uelewa huwa hawana shida kabisa kujifunza na kujitoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…