Jibu la Halima Mdee kuhusiana na msimamo wa Lissu juu ya Wabunge 19 (COVID 19)

Jibu la Halima Mdee kuhusiana na msimamo wa Lissu juu ya Wabunge 19 (COVID 19)

Cannabis

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
11,557
Reaction score
33,535
Kiongozi wa baadhi ya wabunge 19 kutoka chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Halima Mdee ametuma emoj ya kucheka baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu kusema wanatakiwa kueleza nani alisaini mchakato wa wao kuingia bungeni huku akisema yupo tayari kuwapokea wabunge hao .

Kauli ya Tundu Lissu ilisema:

"Katibu mkuu John Mnyika hawajahi kusign fomu na sheria inasema lazima zisigniwe na katibu mkuu za kwao zilisainiwa na nani na aliyekuwa gerezani ilikuwaje akatoka gerezani akaenda kuwapa kuwa mbunge ,kama wanakuja waje wafungue siri za mioyo yao wanataka suluhu na chama waje na mioyo mieupe na tuichunguze ni mieupe kweli wasije tuu kwa sababu ya uchaguzi umekaribia " Lissu

Lakini kwa upande wake Halima Mdee Kupitia mtandao wa X alichukua kipande hicho cha sauti ya Mwenyekiti wao na kutuma alama ya kucheka

Pia soma >Tundu Lissu: Nipo tayari kuwapokea wabunge 19 wa Viti Maalum walioingia bungeni bila baraka za chama


1000021230.jpg
 
Hawa si walishafukuzwa warudi kufanya nini? Wakirudishwa wataleta bad precedence na wengine wataiga huko mbeleni utashangaa mtu anachukua fomu ya kugombea urais na hajaidhinishwa na mkutano mkuu!!

Tuna mabinti wengi wapya kina Siglada, Kasunzu, mayemba, mbugi, maasay, khunchela n.k so hao ndio twende nao oktoba watakua loyal kwa chama. Hao wengine wataleta dharau
 
Tundu Lissu ajenge chama kama alivyahaidi.

Aache Uharakati na kufukuzana na chupi. Musamaha ikufike Bulaya.

Nitamkote memba mwenzi yetu hapa
"Lissu should start to show his "STATEMANSHIP" end kwot

My take
Wanawake wa CHADEMA wameshalalamika kuwa kuna mfumo dume chamani, Lissu anakimbizana na kujibishana nao, watakosa bloc maalum Uchaguzi ya 2025. Ok
 
Halima Mdee ameonyesha emoji mbili za kucheka 😃😃 kupitia mtandao wa X katika taarifa inayomuonyesha Lissu akiongelea kuhusu msimamo wake dhidi ya wabunge hao 19
View attachment 3213007
Mimi hapa ndio simuelewi Lissu. Hivi kweli anaamini kuwa kama kungekuwa na fomu zozote Ndugai angezificha? Hiyo si ndio ilikuwa nafasi ya kumuumbua aliye zisaini na kukivuruga kabisa CDM? Kauli kama hizi za kichonganishi ndio zinanifanya nikose imani nae. Kwangu mimi wakina Halima na Esther ni bora mara kumi ya Msigwa na Slaa ambao ni rafiki zake. Hawa wanawake katika muda wote huu hawajawahi kukitukana chama chao wala viongozi wao. Lakini hao anao wakumbatia walifanya juhudi za wazi kukichimba chama chake.

Ningekuwa yeye ningetangaza ruhusa kwa yeyote ambae kwa sababu yeyote alikuwa nje ya chama kurudi kwenye familia. Mbona waliweza kumkubali mpambanaji Aidan? Kwa hawa wanashindwa nini?

Amandla...
 
Tundu Lissu ajenge chama kama alivyahaidi.

Aache Uharakati na kufukuzana na chupi. Musamaha ikufike Bulaya.

Nitamkote memba mwenzi yetu hapa
"Lissu should start to show his "STATEMANSHIP" end kwot

My take
Wanawake wa CHADEMA wameshalalamika kuwa kuna mfumo dume chamani, Lissu anakimbizana na kujibishana nao, watakosa bloc maalum Uchaguzi ya 2025. Ok
Bawacha wameonyesha wazi kuwa wako kwa Mbowe. Hiyo inamsumbua.

Amandla...
 
Hao ni mali ya kule kwenye binadamu wasio na ubongo yaani waigizaji, wapiga ngoma, wanamuziki,waganga, ma-chief, wazee jamii ya sokwe, madanga ya mjini, madalali wa magari, waandishi wa online media, wazee wa miaka ya 60, police form four failures nadhani mlijionea wiki iliyo pita pale Dodoma.
 
Hawa si walishafukuzwa warudi kufanya nini? Wakirudishwa wataleta bad precedence na wengine wataiga huko mbeleni utashangaa mtu anachukua fomu ya kugombea urais na hajaidhinishwa na mkutano mkuu!!

Tuna mabinti wengi wapya kina Siglada, Kasunzu, mayemba, mbugi, maasay, khunchela n.k so hao ndio twende nao oktoba watakua loyal kwa Lissu. Hao wengine wataleta dharau
Mnataka watu wawe loyal kwa Lissu au kwa chama? Si ndio mwanzo wa uchawa?

Amandla...
 
Back
Top Bottom