Jicho la tatu sakata la Mpina vs Bashe na hasira ya Spika Tulia

Unasalimiwa na Shura ya akina Ponda 😀
 
Nikajua umeandika kitu Cha maana kumbe Bado ni blaa blaa as Mpina?
 
Sakata hili lina uhusiano na ile panga pangua inayoendelea pale jumba jeupe
 
Kuanzia leo, nimeamua kukupuuza na nakuona ni kama mtu usiyeumizwa na chochote juu ya madhila yanayowapata Watanzani wenzako na ama wewe ni mtu wa mlengo fulani na kwa sababu hiyo, hata kama kunapotokea makosa kwa watu wale walio kwenye mlengo wako, kwako ni manukato kwa sababu ulishajiwekeza hivyo

Mtu yeyote mwenye akili timamu na asiyefungwa na umlengo wa unganiko fulani, sharti amuunge mkono Mpina bila kujali itikadi
 
CCM Asili vs Ccm maslahi 😳
 
Bashe kawajengea misikiti mingapi? Make nyie kuiba ni ruksa Ili mradi umegusa misikiti
 
Luhaga Mpina ameeleza umma, maamuzi ya mawaziri, Hussein Bashe (Kilimo) na Mwigulu Nchemba (Fedha) yamepoteza mapato ya Serikali zaidi ya Sh580 bilioni.

Kwa mantiki ndogo, upotevu wa fedha za Serikali ni zaidi ya ufisadi wa RICHMOND ambao ulimfanya Waziri Mkuu, Edward Lowassa kuwajibika kwa kujiuzulu.

Badala ya bunge kuunda kamati teule kuchunguza taarifa kwa kuwa upo ushahidi wa nyaraka, bunge la CCM limemuita Luhaga Mpina kamati ya maadili.

Luhaga Mpina amepelekwa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, kilichoitwa kuingilia madaraka ya Spika kwa kuwasilisha ushahidi wa tuhuma kwa umma.

Bunge la CCM limechoka. Tuhuma hizo zimebebwa na ushahidi. Bunge lilitakiwa kuunda kamati teule ya bunge, siyo kumpeleka kamati ya maadili ya bunge

Upotevu wa mapato ya serikali Sh580 bilioni ni zaidi ya ufisadi mkubwa wowote uliowahi kutikisa serikali na bunge ukiondoa upotevu wa TZS trilioni 1 enzi za JPM.

Tegeta ESCROW (Sh306bn), EPA (TZS 133bn), Mwananchi Gold (Sh272bn), Meremeta (Sh155bn), Mfuko wa kuwezesha uagizaji - CIS (Sh200 bilioni).

Ufisadi wote, mmoja mmoja haujafika katika ufisadi (Sh580bn) ambao unatajwa na Luhaga Mpina kuwa ulisababishwa na Hussein Bashe na Mwigulu Nchemba.

Baraza la usalama la Taifa (2014) lilikutana na kupitia taarifa ya uchunguzi PCCB kuhusu ufisadi wa ESCROW (Sh306bn) kwanini ufisadi wa Sh580bn upuuzwe?

PCCB walifanya uchunguzi ufisadi wa ESCROW na kukabidhi taarifa kwa Rais Jakaya Kikwete, kwanini uchunguzi wa Sh580 bilioni usifanyike? Analindwa nani?

Uchunguzi wa PCCB ulionesha taarifa ya Mkombozi Bank (20/01/14-14/08/14) na malipo kutoka akaunti ya VIP engineering kwenda kwa watu mbalimbali.

Tunashangaa, badala ya bunge kuunda kamati teule kuchunguza taarifa na kuujuza umma, bunge limeamua kumtisha Mpina kwa kutoa ushahidi kwa umma.

Hizo ni juhudi za kumnyamazisha Luhaga Mpina na kuwatetea watu hao anaowatuhumu kwa ufisadi na upotevu wa fedha za serikali zaidi ya Sh580 bilioni.

Martin Maranja Masese, MMM.
 
Kuchukua madaraka huko ccm ni wingi au ni kuwa kwenye nguvu ya madaraka?
 
Hujuwi kile wakiandika
 
Wewe umeelewa nini mkuu 'Rabbon', mimi nimetoka kimasomaso.
Sioni haja ya kuandika lugha pinda alivyo fanya huyu uliyemwelewa kwa hayo aliyoweka hapo. Sikuona lolote la maana sana aliloeleza.
Ujumbe wake una seal/ code.

Na amefanya kusudi Ili waliolengwa waelewe na wengine wasome na wasielewe.
 
Amenisikitisha sana huyu dada anamaanisha kua mtu akiona maovu Anyamaze kwamba akisema ukweli atanyimwa nafasi ya kurudi bungeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…