PostGE2025 Jicho la tatu: Watanzania tuingie katika maridhiano kama Serikali ya Samia inavyotaka

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

mangichogo

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2023
Posts
1,229
Reaction score
2,414
Ushauri tu wangu binafsi, nimefikiria kwanini Jumuia ya Madola imetuma Mwakilishi/Kiongozi atakayesimamia au kuongoza maridhiano, naona hapo kama pana kamtego furani hivi

Wananchi tukikataa maridhiano, vyama vya upinzani vikikataa maridhiano, hamuoni kama tunampa Samia credit na serikali yake?

Jumuia ya Madola sio taasisi ndogo na inaweza ikaenda kwenye taasisi kubwa nyingine duniani na kuwaambia kuwa tatizo la Tanzania sio serikali bali ni vyama vya kisiasa, watasema serikali ilikubali kukaa chini na kuzungumza ili kuyamaliza lakini watanzania ndio hawataki na sisi wananchi tukakosa sapoti ya hizo taasisi

Mimi sioni haja ya kuogopa mazungumzo. Si wamemwita muwakilishi kutoka jumuhia ya madola? Tuingie kwenye mazungumzo ili huyo mwakilishi ashindwe yeye. Mimi ninaamini wananchi na vyama vya upinzani tuna hoja bora na za nguvu sana za kuishinda CCM na huyo mwakilishi wao.

Tukwepe huo mtego, tuingie kwenye majadiliano ili washindwe wenyewe na hizo jumuhia zitafahamu wapi kwenye matatizo
 
Anaandika Askofu Bagonza PhD

MARIDHIANO YASIYOHITAJI KUKAA MEZANI

Kwa hali ilivyo, wito wa maridhiano haupokelewi kirahisi. Hatuna watu wengi wenye uadilifu wa kuaminika pande zote. Tuna mfumo unaoamini kila mtu ana bei na kwamba serikali HAIJAWAHI kushindwa. Mazingira haya ni magumu kupata maridhiano. Nashauri tujikite katika maridhiano yasiyohitaji kukaa mezani. Yakifanyika, ndipo kukaa mezani “labda” kunawezekana. Ni haya;

1. Sitisha utekaji na ukamataji kwa kauli na vitendo. Utekaji na ukamataji unachochea mpasuko.

2. Achia bila masharti waliotekwa, walio mahabusu na wanaoshtakiwa kisiasa.

3. Ruhusu watu wapate miili ya ndugu zao na “kama” kuna iliyofukiwa waonyeshwe ili wachukue udogo au kuweka shada la maua. Itawafanya wamalize matanga.

4. Lifanye taifa liwe la wote - wanaopinga na wanaounga mkono. Si afya wanaopinga kuwa wakimbizi. Inaongeza chuki na kuanika mambo yetu.

5. Acha siasa uchwara (spinning) za kukanusha kanusha na kuficha ficha. Inaongeza hasira. Wajaluo wanasema “binti hawezi kuficha matiti; yakiota yameota”. Tuna msiba mkubwa. Ruhusuni taifa liomboleze. Ni njia ya kuridhiana.

6. Acha fikra za kipumbavu kuhusu dini. Walioua wamo wa dini zote. Hawakutumwa na dini zao kuua. Waliouawa wamo wa dini zote. Hawakufa kwa sababu ya dini zao.
Mali za waumini wa dini zote akiwamo Mtani wangu Wasira ziliharibiwa. “Aliyeruhusu kuua” kama yupo, hakuagiza kuua watu wa dini fulani tu. Ukitumia dini katika hali tuliyo nayo, unaiponza serikali kwa kudhani unaisaidia. Pia unaifanya dini yako ionekane ni bangi inayoondoa uhalisia.

7. Serikali ibadili mkao wake na “kujionyesha” iko upande wa wanaoomboleza. Itoe tamko linalokiri kuwa katika kulinda mali na uhai, kuna kitu kilienda vibaya. Baada ya tamko, watu waone vitendo vya kuwajibishana au kujiwajibisha. Hiyo itaponya na kuunganisha taifa. Tusisubiri kulazimishwa kuwajibika au kuwajibishana.

8. Serikali iwe na mtu anayetoa matamko na msimamo wa serikali. Kwa sasa umma ndiyo wenye haki ya maoni. Walio serikalini na chama tawala wasiwe na maoni nje ya vikao vyao. Eti, “Wananchi waridhiane na wananchi”!? Kweli?😳😳

9. Penye msiba, kuna waombolezaji huwa wanaondoka na vijiko na sahani.
Sitisheni matumizi ya fedha katika kuzima moto huu. Wanaoishi kwa kutegemea posho za kushughulikia “wachochezi” ni wezi wa vijiko na sahani msibani. Asiyetaka kujitolea akae pembeni.

10. Tukubali kuna mgogoro wa madaraka ndani na nje ya CCM. Kuutatua kwa mtutu ni kuuongeza. Kabla ya kukaa mezani, iruhusuni CCM kiwe chama kifanye siasa. Kiwe huru kukemea na kukaani dhuluma katika nchi. Hivi sasa dhambi za serikali ni za CCM na dhambi za CCM ni za serikali. Amkeni kumekucha.

11. Wanaohubiri amani tu hawajipanga kama wanaoharibu amani. Gen Z na serikali wamejipanga vilivyo kuharibu amani. Nawashauri wanaohubiri amani tu, wajipange vizuri. Haki ya kuishi haihojiwi na mamlaka yoyote.

Siasa isiyo na dini ndani yake ni ubabe.
Dini isiyo na siasa ndani yake ni bangi.
 
Maridhiano yako vizuriii
1000207505.jpg
 
Ushauri tu wangu binafsi, nimefikiria kwanini Jumuia ya Madola imetuma Mwakilishi/Kiongozi atakayesimamia au kuongoza maridhiano, naona hapo kama pana kamtego furani hivi

Wananchi tukikataa maridhiano, vyama vya upinzani vikikataa maridhiano, hamuoni kama tunampa Samia credit na serikali yake?

Jumuia ya Madola sio taasisi ndogo na inaweza ikaenda kwenye taasisi kubwa nyingine duniani na kuwaambia kuwa tatizo la Tanzania sio serikali bali ni vyama vya kisiasa, watasema serikali ilikubali kukaa chini na kuzungumza ili kuyamaliza lakini watanzania ndio hawataki na sisi wananchi tukakosa sapoti ya hizo taasisi

Mimi sioni haja ya kuogopa mazungumzo. Si wamemwita muwakilishi kutoka jumuhia ya madola? Tuingie kwenye mazungumzo ili huyo mwakilishi ashindwe yeye. Mimi ninaamini wananchi na vyama vya upinzani tuna hoja bora na za nguvu sana za kuishinda CCM na huyo mwakilishi wao.

Tukwepe huo mtego, tuingie kwenye majadiliano ili washindwe wenyewe na hizo jumuhia zitafahamu wapi kwenye matatizo
Maridhiano yaliyokaa kimtego yataharibu zaidi

Kitendo Cha kuingia kwenye maridhiano ya mtego ccm ITAKUWA imejisafisha mazima

Watanyoshea wenzao mikono kwamba hawataki maridhiano

Pia maridhiano hayopo kwenye level ya vyama vya siasa Tena

Maridhiano yako Kwa wanachi wenyewe

Hivyo vyama haviaminiki Tena na wanachi walishashindwana muda mrefu
 
Acha ujinga wewe
 
Serikali hii ya 97% za tume
 
Watu wenye akili hawaangalii kuwa huyu amekataa kuridhiana, wanaangalia kwanini amekataa kuridhiana.

Kama hao Commonwealth hawana common sense ya kuliona hili tuwaunganishe kwenye trashbin 🚮

Sisi ndio tuliopoteza watu wetu sio wao, Sisi ndio watu wetu wametekwa hata kabla ya 29/10.
 
Maridhiano yaliyokaa kimtego yataharibu zaidi

Kitendo Cha kuingia kwenye maridhiano ya mtego ccm ITAKUWA imejisafisha mazima

Watanyoshea wenzao mikono kwamba hawataki maridhiano

Pia maridhiano hayopo kwenye level ya vyama vya siasa Tena

Maridhiano yako Kwa wanachi wenyewe

Hivyo vyama haviaminiki Tena na wanachi walishashindwana muda mrefu
Una hofu ya kushindwa kwenye maridhiano? Mbona tuna hoja nyingi sana za kuishinda ccm. TUINGIE KWENYE MAZUNGUMZO ILI TUISHINDE CCM KWENYE MARIDHIANO na tutume ujumbe kwenye hiyo jumuhia
 
Mnaanzaje kulidhiana akati mzani unasoma bado 10 - 0.

1. Ambao hawajachaguliwa bado wako Officine.
2. Walio ua na kubaka watu mchana kweupe wapo URAIANI.
3.Walio bambikiwa kesi iki Uchaguzi feki upite wako Gerezani.
4.Walio uliwa Bado hawajapatikana na kuzikwa.

Mnaridhiana NN sasa?
 
Am
Ushauri tu wangu binafsi, nimefikiria kwanini Jumuia ya Madola imetuma Mwakilishi/Kiongozi atakayesimamia au kuongoza maridhiano, naona hapo kama pana kamtego furani hivi

Wananchi tukikataa maridhiano, vyama vya upinzani vikikataa maridhiano, hamuoni kama tunampa Samia credit na serikali yake?

Jumuia ya Madola sio taasisi ndogo na inaweza ikaenda kwenye taasisi kubwa nyingine duniani na kuwaambia kuwa tatizo la Tanzania sio serikali bali ni vyama vya kisiasa, watasema serikali ilikubali kukaa chini na kuzungumza ili kuyamaliza lakini watanzania ndio hawataki na sisi wananchi tukakosa sapoti ya hizo taasisi

Mimi sioni haja ya kuogopa mazungumzo. Si wamemwita muwakilishi kutoka jumuhia ya madola? Tuingie kwenye mazungumzo ili huyo mwakilishi ashindwe yeye. Mimi ninaamini wananchi na vyama vya upinzani tuna hoja bora na za nguvu sana za kuishinda CCM na huyo mwakilishi wao.

Tukwepe huo mtego, tuingie kwenye majadiliano ili washindwe wenyewe na hizo jumuhia zitafahamu wapi kwenye matatizo
kwamba hao Jumuiya ya madola hawataangalia kwanini wapinzani wamegoma hayo maridhiano? Au wao wanaangalia upande mmoja tu? Katafute wa kuwahadaa. Hao Jumuiya ya madola hawana msaada wowote wa maana, kwani watu wamekuwa wakitekwa, chaguzi zikiharibiwa, na serekali hadi sasa inaendelea kuteka na kuua wapinzani kimya kimya. Mbona hatuwaoni hao jumuiya ya madola? Acha kututega kwa mbinu ya kichovu.
 
Back
Top Bottom