Ushauri tu wangu binafsi, nimefikiria kwanini Jumuia ya Madola imetuma Mwakilishi/Kiongozi atakayesimamia au kuongoza maridhiano, naona hapo kama pana kamtego furani hivi
Wananchi tukikataa maridhiano, vyama vya upinzani vikikataa maridhiano, hamuoni kama tunampa Samia credit na serikali yake?
Jumuia ya Madola sio taasisi ndogo na inaweza ikaenda kwenye taasisi kubwa nyingine duniani na kuwaambia kuwa tatizo la Tanzania sio serikali bali ni vyama vya kisiasa, watasema serikali ilikubali kukaa chini na kuzungumza ili kuyamaliza lakini watanzania ndio hawataki na sisi wananchi tukakosa sapoti ya hizo taasisi
Mimi sioni haja ya kuogopa mazungumzo. Si wamemwita muwakilishi kutoka jumuhia ya madola? Tuingie kwenye mazungumzo ili huyo mwakilishi ashindwe yeye. Mimi ninaamini wananchi na vyama vya upinzani tuna hoja bora na za nguvu sana za kuishinda CCM na huyo mwakilishi wao.
Tukwepe huo mtego, tuingie kwenye majadiliano ili washindwe wenyewe na hizo jumuhia zitafahamu wapi kwenye matatizo