Jicho la Ujasusi la Tanzania linatakiwa kuwa macho sasa kuliko wakati mwingine wowote ule

Jicho la Ujasusi la Tanzania linatakiwa kuwa macho sasa kuliko wakati mwingine wowote ule

CWR2016

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2017
Posts
2,773
Reaction score
6,349
Habari wana JF
Watanzania, nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania..

Nitajadili mambo makubwa mawili
1. Vita 'kamili' ya III ya dunia.

2. Namna Tz inavyofanyiwa ujasusi

Hoja No. 1

Kwa wasiojua ni kwamba vita kamili ya 3 ya Dunia imekwisha kuanza. Pole kwa wale wanaosema kuna tishio la WW3, sio tishio, ni vita kamili ilishaanza.

Naomba wanaoita hili, kuwa ni tishio, wawe ni layman tu, wasiwe kati ya Majasusi wetu. Maana kama akili ya jasusi na kufunzwa kote, hajajua vita ishaanza, huyo atakuwa hajafuzu bado na ni hasara kwa kwa Taifa.

Katika mazingira kama hayo, Niwaulize Majasusi wetu. Ni nani alitoa pendekezo la Mama kwenda kufanya ziara Marekani wakati huu?

Hakuna kosa kubwa sana Ujasusi wa Tanzania mmefanya kama hili. Iko hivi, vita yoyote ya dunia huigawa dunia ktk mapande mawili. Sasa niwaulize, mmetupeleka Watanzania upande wa Mmarekani?

Mnaelewa ni kwa nini baada ya Vita ya pili ya dunia (WW2), Tanzania na mataifa baadhi tuliamua kuwa non-aligned (NANs)/, tusioegemea upande wowote.

Huu ni wakati wa kukaa chini na ku draft, serikali yetu inajiendeshaje. Viongozi wetu wapi wanatembelea, na kwa nini, na wanaenda na hoja zipi.

Mfano sio wakati wa kuacha, eti Rais ajiamulie tu aende popote. Mfano kwenda kwake Marekani kumetusaidia nini katika kipindi hiki. Hakuna. Kakaa marekani karibu siku 10. Tumepata nini kama Taifa?!. Hakuna. Wapo watakaosema eti ''Loyo Tua'', au mikataba aliosaini. Mkataba ambao Rostam angeweza saini hata bila Rais kuwepo, ndio mnaouzungumzia kweli?.

Maswali ya kujiuliza...
a. Mama ametoka tu Marekani, Makamu wa Rais wa US aliyekutana na Mama anajitangaza kapatwa na Covid-19, is it a coincidence?

b. Concentration ya Marekani ipo ktk kukusanya nguvu/ushawishi na bajeti kupigana na Urusi, hamkujua kuwa Mama hawezi kusaini chochote na Amerika saivi!?

c. Kwa nyie kwenda Amerika, Je itakapofika wakati tunatakiwa kutoa vijana wakapiganie upande huo, tutawapeleka? Hamjui Wazee wetu walipigana WW1, na WW2 bila fidia yoyote? na ndio maana tukaamua kutofungamana na upande wowote.

d. Kwa nini hamkuwaza ku cancel hayo ma 'Loyo tua' ili yaje yazinduliwe baadae huko? Au mnataka tuamini hii 'Loyo tua' sio yetu, na ndio maana tunafuata tu ratiba ya Director wa muvi?!

Ushauri kidogo
1. Taifa kupitia viongozi wake wanatakiwa wawe na ziara za kimkakati tu ktk wkt huu.
Mfano kutembelea mataifa ambayo tunaagiza kwao mafuta/nishati. Kuhakikisha tuna uhakika kwamba tutaendelea kuuziwa mafuta kwa muda kama tulivyoafikiana.

2. Kutembelea mataifa ambayo yana mbadala wa bidhaa tulizokuwa tunapata Urusi/Ukraini.

3. Ziara zingine ziwe ni ktk mataifa ambayo hayafungamani na upande wowote au yapo moderate ktk mijadala hii.

4. Lazima Cabinet ikae na kuja na mpango mbadala wa uzalishaji wa dharura wa ndani ya nchi ili kufidia gap la bidhaa zitakazoadimika. Mfano mbolea, mazao ya kilimo (mafuta ya kula, ngano, shayiri, mchele, maharage, mahindi, n.k)
Hii iende pamoja na serikali kuwasaidia moja kwa moja wakulima vifaa vya kuhifadhia ziada ya mazao yao.

Ni ujuha kukaa kama vile dunia ni ile ile. Ni upumbavu kukaa na kusema tuombe Mungu vita iishe, akili aliyotupatia Mungu tunaifanyia nini?

Nitaendelea sehemu ya 2

Namna Tanzania inavyofanyiwa ujasusi (Rw, Ug, Ke...
 
Kukaaa nchi ya ugenini sku 10 , unazurura mtaani ni jambo la hovyo Sana , Raisi yupo outdated na haya mambo, waliomzunguka ni wazuri wa diplomasia lakini ni wabovu na washamba wa national security ...!! malengo Yao ni soft appearance but in deep nchi inaoza ....!! Madhara ya BRN ndo haya
 
hahahahaha kwa Tanzania kutofungamana na upande wowote baada ya WW2 tulinufaika na nini au tunanufaika na nini?..

Athari fani walipata waliofungamana na upande fulani ambazo kwa sasa zinatutofautisha nao..

Japs in WW2 walikuwa allies wa Hittler mwanzoni wa Vita kule russia, lakini leo hii ndio rafiki chanda na pete na USA...German ya Hittler ilikuwa adui wa Ulaya na USA lakini leo ni chanda na pete....

Mama kaenda USA kwa ajili ya maslahi ya Tanzania sio vinginevyo, akitakiwa kwenda Russia kwa maslahi ya Tanzania atakwenda pia..

Nitajie idadi ya ziara za Mwalimu Nyerere Russia na China vz USA..
Nitakie ziara ya rais mwingine wa Tanzania kwenda Rusia na China Vz USA..
 
Hii ni story kama story zingine. Kwanza hakuna vita ya 3 ya dunia. Unaweza nipa proof au article inayothibitisha vita ya 3 ya dunia imeanza 2022.

Tanzania tutabaki kua taifa lisilo fungamana na upande wowote. Nakukumbusha balozi ya urusi Tanzania jana imetoa salamu za muungano kwa niaba ya rais wa urusi
 
ni kweli mkuu ww3 tayari ishaanza maana kwa matamshi aliyotoa waziri wa mambo ya nje wa Marekani kuwa urusi inatakiwa kudhoofishwa sioni namna ya kutokutokea vita kubwa huko Ulaya na kama naziona baadhi ya nchi kutokukalika tena
 
Kwenye mahojiano yake akiwa Marekani, rais Samia hakuonyesha kuunga mkono upande wowote kwenye vita ya Ukraine na Russia.

Pia badili “fonts” au uzikuze kidogo.
 
Kukaaa nchi ya ugenini sku 10 , unazurura mtaani ni jambo la hovyo Sana , Raisi yupo outdated na haya mambo, waliomzunguka ni wazuri wa diplomasia lakini ni wabovu na washamba wa national security ...!! malengo Yao ni soft appearance but in deep nchi inaoza ....!! Madhara ya BRN ndo haya
Ziara haikuwa na 'substance' kabisa. Huwezi kui rate kama ilikuwa ziara ya kiongozi wa nchi.
 
Kwenye mahojiano yake akiwa Marekani, rais Samia hakuonyesha kuunga mkono upande wowote kwenye vita ya Ukraine na Russia.

Pia badili “fonts” au uzikuze kidogo.
Urusi hajawahi kututumia salamu za Muungano huko nyuma.

Utaelewa kwa nini wakati huu ametutumia salamu hizo. Kuna mengi ya kutafakari.
 
Na cha ajabu, kumbe ile ya barua ya Urusi kumpongeza Rais kwa sababu ya sherehe za Muungano ni ya kweli. Nimeona kwenye page ya Russia in Tanzania(Ubalozi wa Russia).
 
Na cha ajabu, kumbe ile ya barua ya Urusi kumpongeza Rais kwa sababu ya sherehe za Muungano ni ya kweli. Nimeona kwenye page ya Russia in Tanzania(Ubalozi wa Russia).
Tusimlaumu Sana MAMA KWENYE HILI!!YEYE hakuandaliwa kuwa Raisi tangu mwanzo!!!???KWA hiyo code za uraisi hazijui na hakujiandaa kuwa RAISI ndio maana KILA ushauri anaopewa YEYE anajichimbia kaburi!we ona wakati akiwa USA kinana anafanya ziara za ki CHAMA unadhan ni co incidence tena nasikia na msoga yupo huko huko USA!Kuna jambo linapikwa tuupe muda UAMUE!!!!
 
Habari wana JF
Watanzania, nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania..

Nitajadili mambo makubwa mawili
1. Vita 'kamili' ya III ya dunia.

2. Namna Tz inavyofanyiwa ujasusi

Hoja No. 1

Kwa wasiojua ni kwamba vita kamili ya 3 ya Dunia imekwisha kuanza. Pole kwa wale wanaosema kuna tishio la WW3, sio tishio, ni vita kamili ilishaanza.
Naomba wanaoita hili, kuwa ni tishio, wawe ni layman tu, wasiwe kati ya Majasusi wetu. Maana kama akili ya jasusi na kufunzwa kote, hajajua vita ishaanza, huyo atakuwa hajafuzu bado na ni hasara kwa kwa Taifa.

Katika mazingira kama hayo, Niwaulize Majasusi wetu. Ni nani alitoa pendekezo la Mama kwenda kufanya ziara Marekani wakati huu?!!
Hakuna kosa kubwa sana Ujasusi wa Tanzania mmefanya kama hili.
Iko hivi, vita yoyote ya dunia huigawa dunia ktk mapande mawili. Sasa niwaulize, mmetupeleka Watanzania upande wa Mmarekani!!?
Mnaelewa ni kwa nini baada ya Vita ya pili ya dunia (WW2), Tanzania na mataifa baadhi tuliamua kuwa non-aligned (NANs)/, tusioegemea upande wowote.!!

Huu ni wakati wa kukaa chini na ku draft, serikali yetu inajiendeshaje. Viongozi wetu wapi wanatembelea, na kwa nini, na wanaenda na hoja zipi.
Mfano sio wakati wa kuacha, eti Rais ajiamulie tu aende popote.
Mfano kwenda kwake Marekani kumetusaidia nini katika kipindi hiki. Hakuna. Kakaa marekani karibu siku 10. Tumepata nini kama Taifa?!. Hakuna. Wapo watakaosema eti ''Loyo Tua'', au mikataba aliosaini. Mkataba ambao Rostam angeweza saini hata bila Rais kuwepo, ndio mnaouzungumzia kweli?.

Maswali ya kujiuliza..........
a. Mama ametoka tu Marekani, Makamu wa Rais wa US aliyekutana na Mama anajitangaza kapatwa na Covid-19, is it a coincidence?
b. Concentration ya Marekani ipo ktk kukusanya nguvu/ushawishi na bajeti kupigana na Urusi, hamkujua kuwa Mama hawezi kusaini chochote na Amerika saivi!?
c. Kwa nyie kwenda Amerika, Je itakapofika wakati tunatakiwa kutoa vijana wakapiganie upande huo, tutawapeleka? Hamjui Wazee wetu walipigana WW1, na WW2 bila fidia yoyote? na ndio maana tukaamua kutofungamana na upande wowote.
d. Kwa nini hamkuwaza ku cancel hayo ma 'Loyo tua' ili yaje yazinduliwe baadae huko? Au mnataka tuamini hii 'Loyo tua' sio yetu, na ndio maana tunafuata tu ratiba ya Director wa muvi?!

Ushauri kidogo............
1. Taifa kupitia viongozi wake wanatakiwa wawe na ziara za kimkakati tu ktk wkt huu.
Mfano kutembelea mataifa ambayo tunaagiza kwao mafuta/nishati. Kuhakikisha tuna uhakika kwamba tutaendelea kuuziwa mafuta kwa muda kama tulivyoafikiana.
2. Kutembelea mataifa ambayo yana mbadala wa bidhaa tulizokuwa tunapata Urusi/Ukraini.
3. Ziara zingine ziwe ni ktk mataifa ambayo hayafungamani na upande wowote au yapo moderate ktk mijadala hii.
4. Lazima Cabinet ikae na kuja na mpango mbadala wa uzalishaji wa dharura wa ndani ya nchi ili kufidia gap la bidhaa zitakazoadimika. Mfano mbolea, mazao ya kilimo (mafuta ya kula, ngano, shayiri, mchele, maharage, mahindi, n.k)
Hii iende pamoja na serikali kuwasaidia moja kwa moja wakulima vifaa vya kuhifadhia ziada ya mazao yao.

Ni ujuha kukaa kama vile dunia ni ile ile. Ni upumbavu kukaa na kusema tuombe Mungu vita iishe, akili aliyotupatia Mungu tunaifanyia nini?!

Nitaendelea sehemu ya 2............ Namna Tz inavyofanyiwa ujasusi (Rw, Ug, Ke....................
Duh yani kama wakat wa ku....Halafu anatowa paap ndipo ulipoishia.
 
Marekani ni makao makuu ya mashirika yote ya kimataifa, haiwezekani kiongozi wa dunia hii asifike huko, hata ghadafi alikwenda huko, pamoja na mugabe
 
Back
Top Bottom