Jifungie zako ndani, tazama filamu hizi

Mkuu Steve nakubaligi sana recommendations zako uwe unafanya kutupia kila baada ya miezi kadhaa kama zamani
 
Kwahyo mkuu unamaanisha nini kwa sie tupendao horror? [emoji1][emoji1][emoji1] Tutaishia kuwa walozi?
Mkuu.. mim nitaftie movie flan za terrorism
Americans n the middle east flan hiv or americans vs russia . Ujasus.. nukipata kama 3 hiv. Na barid lililoko hapa nilipo now -1... Itanifaa sanaaa
 
Kikosi maalum cha polisi kinafanya Operasheni ya kushtukiza katika kitongoji kidogo cha kilatini kwa lengo la kukamata watumiaji na wauzaji wa mihadarati.

Katika oparesheni hiyo yumo mdada anayeitwa Camila, mstari wa mbele kabisa na bunduki yake akitimiza majukumu yake kwa ujasiri mkubwa.

Hapa na pale katika uwanja wa mapambano, Camila anajikuta akianguka kama mzigo toka darini mpaka chini, ajabu anapotua anakaribishwa na mwanamke albino aliyevaa joho jeupe akiwa pamoja na wenzake wasoonekana nyuso, watu hao wapo katikati ya matambiko ya damu, mwanamke huyo albino anamwambia Camila kuwa amekuja wakati muafaka na punde baada ya kusema hayo wanajichoma moto!

Baadae Camila anaokolewa akiwa ameungua vibaya mwili mzima, anakaa kwenye 'coma' kwa muda wa masiku kadhaa, rafiki yake aitwaye Fatima na 'partner' wake aitwaye Angel wanakuwa naye karibu katika safari ya kuuguza lakini Camila anapokuja kupata ahueni anaonekana akiwa si Camila yule wa awali.

Camila wa sasa hana hisia, ni wa ajabu, si mchangamfu wala wa kujichanganya, lakini zaidi ni kwamba mwanamke yule albino yupo kando yake kama kivuli. Mwanamke huyo anawachezea shere watu hawa watatu; Camila, Fatima na Angel.

Sasa namna gani ya kumkabili mtu huyo ingali nafsi yake ilifungamanishwa na mhanga Camila katika tambiko lile? Na itakuaje ukizingatia Camila wa sasa si tena binadamu wa kawaida?
 
[emoji419]
 
Mbona zinatisha ivyo..πŸ™„πŸ™„..hapana
 
Back from the dead 😁😁 lazima nizifatilie hizo
 
Mbona zinatisha ivyo..[emoji849][emoji849]..hapana
Basi hii hapa...


Dr. Nate ameingia kwenye ugane muda si mrefu baada ya kumpoteza mke wake kwa ugonjwa wa saratani, kama haitoshi mke anamwachia mabinti wawili wa kuwalelea peke yake, watoto ambao hakuwahi kuwa nao karibu kama baba, achilia mbali hakuwa hata karibu kumuuguza mke wake kama mume!

Basi kwasababu ya kutengeneza ukaribu na familia yake ili angalau wajiponyeshe na maumivu ya kumpoteza mama, Dr. Nate anaamua kuwapeleka wanae wawili 'vacation' huko Afrika ya kusini, mbugani, ili wakaone mahali ambapo mama yao alipata kukulia.

Safari hiyo ya kujiponyesha vidonda vya kumpoteza mama inageuka kuwa mapambano ya uhai pale simba aliyenusurika kuuawa na majangili anapoanza kuifuatilia familia hii ili apate kuitokomeza kwaajili ya kulipa kisasi!

Sasa Dr. Nate anapata mtihani wa kudhihirisha mapenzi yake halisi kwa wanae na familia yake kwa kupambana na simba huyu kuhakikisha usalama wa watoto wake.

Mapambano hayo si marahisi, kwani mmoja wao inabidi aende ili mwingine abaki kuwa hai.
 
Mkuu unaonaje kama ungekuwa unatuwekea na links za ku-download kabisa maana sio wote humu wana utaalam wa kuzitafuta!!
 
Hbari zenu wakuu??
mwenye links za movie ya wakanda na woman king naomba please!!!
 
Kwahyo mkuu unamaanisha nini kwa sie tupendao horror? [emoji1][emoji1][emoji1] Tutaishia kuwa walozi?
Unaweza kuwa mlozi ukakomaa na kile kinachofanyika au ikakuongezea waswas katika mambo flanflan...!! Now movie zenye mazingira ya kutisha na uchawchawi nmeacha kuchek ase now najiona nmeanza kuwa normal
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…