Jifungie zako ndani, tazama filamu hizi

Jifungie zako ndani, tazama filamu hizi

Movie gan hizo?? Zaman nlikuwa napenda movie za aina hii ila kwa sasa nmeachana nazo..! Sasa napenda movie za ucheshi na stori za maisha...!
Kuna movie moja inaitwa THE BANKER itafute hii kama ww ni kijana mpambanaji bas itakutia moyo sana
Ya Denzel Washington?
 
Kikosi maalum cha polisi kinafanya Operasheni ya kushtukiza katika kitongoji kidogo cha kilatini kwa lengo la kukamata watumiaji na wauzaji wa mihadarati.

Katika oparesheni hiyo yumo mdada anayeitwa Camila, mstari wa mbele kabisa na bunduki yake akitimiza majukumu yake kwa ujasiri mkubwa.

Hapa na pale katika uwanja wa mapambano, Camila anajikuta akianguka kama mzigo toka darini mpaka chini, ajabu anapotua anakaribishwa na mwanamke albino aliyevaa joho jeupe akiwa pamoja na wenzake wasoonekana nyuso, watu hao wapo katikati ya matambiko ya damu, mwanamke huyo albino anamwambia Camila kuwa amekuja wakati muafaka na punde baada ya kusema hayo wanajichoma moto!

Baadae Camila anaokolewa akiwa ameungua vibaya mwili mzima, anakaa kwenye 'coma' kwa muda wa masiku kadhaa, rafiki yake aitwaye Fatima na 'partner' wake aitwaye Angel wanakuwa naye karibu katika safari ya kuuguza lakini Camila anapokuja kupata ahueni anaonekana akiwa si Camila yule wa awali.

Camila wa sasa hana hisia, ni wa ajabu, si mchangamfu wala wa kujichanganya, lakini zaidi ni kwamba mwanamke yule albino yupo kando yake kama kivuli. Mwanamke huyo anawachezea shere watu hawa watatu; Camila, Fatima na Angel.

Sasa namna gani ya kumkabili mtu huyo ingali nafsi yake ilifungamanishwa na mhanga Camila katika tambiko lile? Na itakuaje ukizingatia Camila wa sasa si tena binadamu wa kawaida?View attachment 2440006
Mkuu uko vizuri[emoji122][emoji122]
 
Basi hii hapa...
View attachment 2440168

Dr. Nate ameingia kwenye ugane muda si mrefu baada ya kumpoteza mke wake kwa ugonjwa wa saratani, kama haitoshi mke anamwachia mabinti wawili wa kuwalelea peke yake, watoto ambao hakuwahi kuwa nao karibu kama baba, achilia mbali hakuwa hata karibu kumuuguza mke wake kama mume!

Basi kwasababu ya kutengeneza ukaribu na familia yake ili angalau wajiponyeshe na maumivu ya kumpoteza mama, Dr. Nate anaamua kuwapeleka wanae wawili 'vacation' huko Afrika ya kusini, mbugani, ili wakaone mahali ambapo mama yao alipata kukulia.

Safari hiyo ya kujiponyesha vidonda vya kumpoteza mama inageuka kuwa mapambano ya uhai pale simba aliyenusurika kuuawa na majangili anapoanza kuifuatilia familia hii ili apate kuitokomeza kwaajili ya kulipa kisasi!

Sasa Dr. Nate anapata mtihani wa kudhihirisha mapenzi yake halisi kwa wanae na familia yake kwa kupambana na simba huyu kuhakikisha usalama wa watoto wake.

Mapambano hayo si marahisi, kwani mmoja wao inabidi aende ili mwingine abaki kuwa hai.
Daah hii kali
 
Mkuu unaonaje kama ungekuwa unatuwekea na links za ku-download kabisa maana sio wote humu wana utaalam wa kuzitafuta!!
Jaman njoon ofisini kwangu BoBmovies Sinza madukani ...buku lako tu[emoji16][emoji16]
 
Wakati mama yake akiwa kitandani hoi bin taaban, hajiwezi na anahitaji msaada haraka iwezekanavyo, mtoto Rose (mwenye miaka kumi) aliishia kumtazama tu mpaka kifo chake!

Hakujigusa na wala hakutaka kujisumbua kwani alikuwa hampendi mama yake kwa namna alivyokuwa anamtenda.

Alimchukia toka ndani na chuki hiyo ilimfanya asijali hata pale mama yake alipokiri kuwa amefanya makosa, badala yake akaufunga mlango na kumwacha mama akitwaliwa na umauti.

Miaka mingi mbele, Rose anakuwa daktari wa magonjwa ya akili. Anaipenda kazi yake mno na anaifanya kwa moyo wake wote. Anapokea na kuwasaidia watu kiasi kwamba anakuwa tegemezi hospitalini hapo. Mambo ni shwari kabisa. Ana mpenzi anayempenda na pia ana kazi anayofurahia kuifanya.

Mambo yanakuja kubadilika pale usiku mmoja Dr. Rose anapokutana na mgonjwa wa ajabu, msichana wa chuo kikuu ambaye ametoka kushuhudia profesa wake akijiua mbele yake!

Msichana huyo anamweleza Dr. Rose kuwa tokea hapo amekuwa akifuatwa na roho ya ajabu ikimwambia kuwa naye atakufa! Roho hiyo ipo katika mfumo wa mtu anayetabasamu ikiwa inahama toka mtu na mtu, tukio na tukio.

Msichana huyo amejaribu kuwaambia watu wengine lakini hakuna anayemwamini. Kila mtu anamdhania amewehuka kiasi cha kukosa msaada, bahati mbaya hata huyu Dr. Rose naye anaamini mtu huyu ni mgonjwa.

Ghafla msichana huyo anadondoka chini akihangaika kama mtu aliyeshikwa na degedege kali! Dr. Rose anawahi kupiga simu ya msaada lakini anapokata simu hiyo nakumtazama mgonjwa wake anamkuta akiwa amesimama salama salmin kama si yeye alotoka kuhangaika kiasi kile!

Kama haitoshi mgonjwa huyo anatabasamu kiajabu, mkononi ameshikilia kwanguvu kipande cha chungu cha maua. Kufumba na kufumbua, msichana huyo akiwa anatabasamu, anajikata shingo na kuanguka chini akiwa mfu!

Dr. Rose anatoa macho kustaajabu. Anaogopa mno. Lakini asilolijua ni kwamba, huu ni mwanzo tu ... Mwanzo wa maisha yake kuwa kama ya digidigi porini huku watu wake wa karibu wakimwona amewehuka!

Dr. Rose anaanza kuona sura za ajabu zikimtabasamia huku akiupata ujumbe wa kifo chake vilevile kama alivyokuwa akielezwa na mgojwa wake wa mwisho!

Dokta anakuja kubaini kuwa kifo cha mgonjwa yule mbele yake kilikuwa ni kupokea kijiti cha laana, lakini chanzo ni nini? Na kwanini yeye?
View attachment 2444355

Na je, atamudu kujinasua kabla hajakumbwa na umauti?
Duuuh kazi ninayo...yaan haya ndo mambo yangu Wit[emoji848][emoji848][emoji15]
 
Ya Denzel Washington?
Ni ya Anthony Mackie na Samuel Jackson.
79d8c8eac2adeb42c1685cb9d42272b4.jpg
 
Inahusu nini mkuu?
NOPE (2022)

Mzee Otis anafariki kifo chenye kujawa na utata, kwa mujibu wa maelezo ya polisi mzee huyo alitobolewa na shilingi iliyodondoka toka juu angani, wakiamini shilingi hiyo ilitoka kwenye ndege ikamfikia mzee huyo jichoni na kumpasua ubongo.

Bada ya kifo hicho, watoto wawili wa marehemu Otis wanakaimu ranchi ya mzee wao kwa lengo la kuiendeleza hapo wakishughulika na kuwatazama na kuwafunza farasi ambao walikuwa wanawauzia Hollywood kwaajili ya maigizo.

Lakini biashara hii, mikononi mwa hawa watoto, haionekani kuwa na faida, pengine kwasababu warithi hawa hawakuwa na ujuzi kama ule alokuwa nao baba yao. Kwasababu hiyo basi, mtoto wa kike anaegemea zaidi kupata mwanya huko Hollywood huku kaka yake akitazamia namna ya kujikuza kiuchumi.

Muda si mrefu, watoto hawa wawili wanakuja kubaini kuna kitu cha kushangaza angani! ... Ni kama wingu kubwa hivi lakini lenye umbo la ajabu mithili ya ndege wanazotumia viumbe kutoka sayari zingine (UFOs), wingu hilo la ajabu linawaogopesha farasi wao wa kwenye ranchi na hata binadamu pia.

Kijana wa kiume, Otis junior, anaona kitu hiko kinaweza kuwa fursa kwao. Endapo wakifanikiwa kukirekodi kwenye kamera na kikathibitishwa kuwa ni kweli basi wanaweza kupata fedha nyingi sana kwasababu kuna tovuti na vyombo vingi vya habari vingeinunua habari hiyo.

Lakini kabla hawajaanza kupata hata senti mkononi, wanabaini wingu lile si kitu cha mzaha kabisa, ni zaidi ya kile walichokuwa wanakifikiria na kukitegemea. Ni kitu chenye njaa na roho za watu!

Mambo yanabadilika juu chini, chini juu, kwani sasa badala ya kuwaza kutengeneza pesa, wanahaha kutetea uhai wao ambao upo mashakani chini ya kitu ambacho huenda kilitoa uhai wa baba yao!

ab6ce8af508b237140a845088b0cf857.jpg
 
View attachment 2445990
Duuh
 
Back
Top Bottom