Jifungie zako ndani, tazama filamu hizi

Blood Red Sky ni bonge moja la Movie.

Ila wasisahau kuongeza na hii👇
 

Attachments

  • IMG-20221210-WA0008.jpg
    111.7 KB · Views: 42
Mkuu ebu elezea hiyo ya will smith, na hiyo ya good night mommy
GOODNIGHT MOMMY (2022)


Baada ya ndoa kuvunjika, baba na mama waliobarikiwa watoto wawili mapacha, Elias na Lukas, wanatengana kila mtu akienda kuishi upande wake, baba anasalia mjini na watoto huku mama akienda kuishi kijijini (countryside) peke yake.

Baada ya muda fulani, watoto wanamtembelea mama yao ambaye ametoka kufanyiwa upasuaji wa uso muda si mrefu hivyo uso wa mama huyo umefunikwa na bandeji isipokuwa macho na mdomo wake tu ... ni ngumu kumtambua kama wewe ni mgeni kwake .... huko watoto wanapowasili mama anawapatia sheria za makazi yake, moja, hawatakiwi kwenda kwenye jengo la kuhifadhi mazao na wanyama, pili, hawatakiwi kuacha madirisha wazi, tatu hawaruhusiwi kuingia kwenye ofisi yake wala chumbani kwake, nne na mwisho hawaruhusiwi kupiga kelele!

Swala hili linawashangaza watoto, Elias na Lukas, kwani kwa wanavyomjua mama yao si mtu wa kutunga na kuwawekea sheria, lakini wakawaza pengine ni kwasababu ya upasuaji alofanyiwa ndo' maana amegeuka kuwa mbogo lakini mmmh ... shaka inaongezeka zaidi pale mama yao anapokataa kuwaimbia wimbo wa kuwalaza usiku, hii si kawaida kabisa kwani tangu utotoni amekuwa akiwaimbia usiku kabla ya kulala, leo imekuaje?

Taratibu watoto hawa wakaanza kujenga shaka kuwa huenda mwanamke aliyefunikwa na bandeji si mama yao wanayemjua, ni mtu mwingine kabisa! Kadiri siku zilivyokuwa zinaenda wakawa wanazidi kupata hisia na sababu kuwa huyu si mama yao kutokana na matendo yake ya ajabu.

Kwanini hataki waingie chumbani kwake? Kwanini hataki waende kwenye jengo la kuhifadhia mazao? Bila shaka kuna kitu atakuwa anaficha! ... Elias akaenda kuchungulia kwenye jengo hilo na kubaini kuna midoli na magazeti ya zamani, ila zaidi kuna damu ukutani!

Huyu mwanamke ni nani?

Watoto wanafanya jitihada ya kuwasiliana na baba yao lakini mama anagundua hilo, anaamua kuharibu simu na kuwafanya watoto wawe hawana msaada wowote ule ... Ni wao na yeye tu!

Sasa nini kitajiri? Huyu mama ni nani? Na mama yao halisi yu wapi?

Mwisho wake utakuacha mdomo wazi.



 
[emoji120]

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Jitahidi kabla hujafa uwe umeitazama Knives Out.

Anyways, Glass Onion kwa wapenzi wa 'Mysteries' na 'Thrillers' utaenjoy sana.
 
Aisee
 
Movie za miaka ya siku hizi zimekua za kiboya Sana,naenjoy kuangalia movie za action/comedy za 80,s,90's,2000-2010 hapo.Za miaka hii Ni no go zone kwangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…