Leo nimefanikiwa kupata shipment yangu ya kwanza kati ya mbili nilizonunua online ... kwa manufaa ya wote, zoezi zima lilienda kama ifuatavyo..
Baada ya kukamilisha ku -link na paypal online Atm card yangu, tarehe 24 nikanunua earphone kwa dola 34, (free shipping ) hapa contcacts zangu wakachukua zile nilizotumia kujusajili paypal , jina langu , email adress yangu, namba yangu ya simu ie. +255...... , mkoa na mtaa , sina sanduku la posta kwa hiyo sikujaza box namba. free shipping zinatumwa through registerd mail ( 5 to 45 days) kwa hiyo baada ya kununua nikapata email kutoka kwa seller ikiwa na tracking number ,baada tu ya kununua nikapata sms kwenye simu yangu kuwa nimetoa ths 56700 , ina maana rate ya dola kwa transaction hiyo ilikuwa kama $1-tsh 1660. jana nilitumiwa sms na watu wa posta kuwa kuna rejista yangu, leo nimekwenda posta mpya na kuchukua mzigo,upo kama nilivyoagiza, bila tatizo lolote na sijalipia chochote.
tarehe hiyo hiyo nikanunua simu kupitia hapa kupitia etotalk , thamani yake iliuwa ni dola 228, hapa seller alinipa option tatu, DHl china dola 55, (2-7days delively) DHL dubai dola 42 (7-10days ) ya tatu iliuwa ni registerd airmail, dola 25 (5-45 days ). nikaopt Dhl dubai kwa hiyo gharama yote ilkawa dola 270, hapa baada ya kufanya manunuzi kupitia paypal nikapata sms ya kutoa ths 457699 kwa rate ile ile ya 1$- ths 1600, kama seller wa mwanzo alivyofanya naye akanipatia tracking number , challenge ni kuwa etotalk wapo hongkong kwa hiyo mzigo ulikuwa unapitia kwa courier agent wa huko (zj express) kwanza ,kabla ya kufika Dhl dubai. track number niliyopewa ilikuwa ya zj express ,siku tatu za kwanza nilikuwa na track kupitia huko ,mzigo ulipofika dubai nikapewa track number ya dhl, trackin inaonesha simu tayari imeshafika Dar, DHL wanafanya clearance ambayo wanasema itabidi nilipe kodi, uzuri ninayo tin number, nafikiria kama nisingekuwa nayo delays zingekuwaje, ukizingatia gharama za juu wanazochaji kusafirisha mizigo,nilitegemea shipment zao zingekuwa super fast. ila usumbufu unaojitokeza huko dhl unakula muda na kukatishaa tamaa sana , nitaendelea kuwajuza siku nitakapokamilisha zoezi hilo huko dhl.
Nimejifunza registered air mail haina usumbufu, japo challenge iko kwenye usalama wa mizigo,kwa wasio nabox namba kama mimi inabidi ukachukue mizigo posta mpya, that is, kama rejister haina box number haitoki makao makuu.