Jifunze Jinsi ya kufanya Manunuzi kwa Ebay mtandaoni

Jifunze Jinsi ya kufanya Manunuzi kwa Ebay mtandaoni

Ee bwana naomba ujuzi nataka kununua graphics card ya kompyuta kutoka Amazon vp kuhusu shipping company yenye bei nafuu zaidi ya Dhl na Fedex?
Hili suala pia unaweza wasiliana na seller maana yeye ndo anachagua shipping company/courier. So unaweza ukarequest kama ataweza tumia US PS au middlemen kama ComGateway. Ila pia kama ungekuwa unatumia Amazon Prime ungefaidi zaidi. Nilisomaga benefits zake lakini tukashindwana ada na the fact kwamba eBay ndo kumekuwa kama nyumbani, Amazon pakakosa mashiko kabisa rohoni.
 
Je ilishatokea hivyo hapo kabla? Au ndo mara ya kwanza unafanya payment kwa hao GoDaddy?/mara ya kwanza kwa payment kusumbua?
Jeh, hao GoDaddy wanaruhusu "straight payments" toka kwenye credit card (ingawa hapa ningekushauri sana uwe unatumia PayPal account)? Au ni njia gani wanazotumia kwa malipo? Kama wana option ya kulipia na PayPal (ambayo ndio "standard" form of payment kwenye masoko mengi ya online), emb jaribu kuitumia uone kama itasumbua.

Unaweza ukawa ume'activate card yako ifanye MOTO/mihamala ya mtandaoni, lakini bank yako haijatambuliwa, ishu ambayo inatatulika kirahisi sana kama uta'link credit card yako na account ya PayPal.

Pia kumbuka PayPal ina'guarantee sana usalama wa transactions zako online.

Yangu ni hayo tu ndugu angu.

Thanks for ur concern mkuu,, tatzo SOLVED... kumbe wanataka address ziwe zinafanana, nimegundua baada ya kupitia comment ya mdau mmoja hapo juu,,
I'm happy now nshailink kadi yangu na paypal now ni mwendo wa kupurchase tuu teh teh teh😀😀
 
Wakuu naomba kuuliza je hapa mzigo umeshafika Dar au upo njiani kuja?
Screenshot_20170411-211733.png
 
Mzigo mpaka kufika umetumia siku ngapi labda?
Nimeagiza March 31 umenifikia jana April 12 nï siku 12 tu.
Huo ni toka Hong Kong umetumwa kwa:- Standard international Shipping (Hong Kong post)
Kuna mwingine niliagiza Rochester USA tokea March 20 umenifikia April 11 yaani siku 21 (USPS) first class international
 
Kwa uzoefu wangu, mizigo kutoka Hong Kong na Netherland ndo mizigo inayotumia muda mfupi kabisa mpaka kuutia mikononi. Kati ya siku 6-12, sehemu nyingine kama China,turkey,Singapore ni kati ya siku 12-21 hii ni kwa kutumia standard shipping
 
Vipi kuhusu Economy International Shipping? Inaweza ikachukua muda gani kufika?
 
Vipi changamoto katika upokeaji mkuu? hawajakulima kodi ndefu? ulipigiwa simu au ulijipeleka mwenyewe? procedures in general zikoje?
Nilijipeleka mwenyewe ila kufika pale walidai mzigo bado haujafika niende kuchukua J4 baada ya sikukuu.
Niliwauliza mbona tracking inaonyesha umefika tokea jana yake wakajibu kwamba bado upo GPO utafika mchana.
Sikuwa na jinsi nikaondoka ila baada ya nusu saa hivi wakani pigia simu nikachukue mzigo.
Yaonyesha ulikuwapo ila sijaelewa sababu za kuchelewesha kuutoa.
Kuhusu ushuru hawakunidai
 
Back
Top Bottom