SuperImpressor
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 1,505
- 648
Ila kwa kweli hawa jamaa wa posta wakati mwingine wana kauvivu fulani lakini kuna wakati pia wanazidiwa na kazi kwa sababu kwa sasa hivi watu wanaoagiza mizigo kutoka nje wamekuwa wengi na hivyo kuwawia ugumu fulani wa kushughulikia swala hilo. Kwa mfano mtu anapoitwa kuchukua mzigo wake ni hatua zipi hufanyika mpaka kukabidhiwa mzigo wake. Hapa ni baadhi tu, 1. Kufungua mizigo na kuweka vifurushi vya mhusika pamoja, 2. Kuandika namba za simu na kumwita mhusika, 3. Kuscan barcode za vifurushi, 4. Kujaza jina na taarifa za kitambulisho chako kwenye kitabu, tarehe na muda wa delivery nk.Wakati mwingine posta makao makuu wanachanganya mizigo. Mzigo ambao unatakiwa uende kibiti posta unaenda singida.
Mfano halisi : niliagiza mzigo tangu mwezi wa 10 mwaka Jana na ulifika posta kuu mwezi wa kumi na mbili{shipping way haikuwa express). Mzigo ulipaswa kufika Chalinze.
Nilisubiri Sana mzigo haukufika na nikitrack naambiwa anuani imekosewa ingawa mzigo upo nchini.
Sasa mwezi wa pili mwaka huu posta kawe walinipigia Kama Kuna mzigo upo kwao na ulitumwa kimakosa. Nikawaambia ok fine,tumeni huo mzigo uje Chalinze.
Mpaka muda huu mzigo bado hawajatuma na Kila nikiwatafuta wananiambia watatuma.
Kwa hiyo posta kuu wakati mwingine wanamisplace mizigo.
Sent using LEAGOO M12
Na wakati mwingine network inasumbua,
Hizo ni sababu ambazo wakati mwingine zinasababisha mimi sasa nianze tu kuwa navumilia ucheleweshaji huo.
Ila hilo la kukupiga danadana mmmmhh walifanyie kazi ni muda mrefu sana.
Sent using Jamii Forums mobile app