Jifunze Jinsi ya kufanya Manunuzi kwa Ebay mtandaoni

Jifunze Jinsi ya kufanya Manunuzi kwa Ebay mtandaoni

M-PESA master card naweza kufanyia manunuz mtandaoni,kama ebay!aliexpress,alibaba,kikuu
 
Simu yangu ya htc ilipasuka kioo, nikatafuta weee, mwisho kuna mtu humu jukwaani akanitajia fundi yupo posta anaitwa sele. nikaenda kufika kaniambua kioo kipo ila bei laki, haipungui wala nini, nikaona pagumu.

Mwezi uliopita nikaamua nijaribu ebay nikakuta vioo kibao nikachagua model yangu, nikalipia kwa paypal, kama elfu 36 tu na free shipping.

Baada ya wiki 3 nimekipata kioo.

Kwa wale wanaohofia kuibiwa au kutapeliwa, mie nimepata bidhaa niliyonunua, nanyi msisite kununua.

JIBU: UncleUber replied; mzigo wako utaupokelea posta au mahala popote ambapo utakuwa umeomba mzigo wako upelekwe; mfano unaweza(kama umelipia gharama za kuuleta kwa njia husika) kuja DHL au USPS n.k utaukuta kwenye ofisi husika, mara nyingi uwa wanakupigia simu kifurushi chako kikifika (hata posta wanapiga simu)

Safi sana.
 
Kuna yoyote amepokea bidhaa kutoka aliepress kwa mwezi wa sita au huu wa saba mwaka huu kwa njia ya posta Tanzania?

Nataka kujua maana posta walisitisha kupokea bidhaa
 
Kuna yoyote amepokea bidhaa kutoka aliepress kwa mwezi wa sita au huu wa saba mwaka huu kwa njia ya posta Tanzania?

Nataka kujua maana posta walisitisha kupokea bidhaa
Asante mkuu, mimi nimepata mwezi huu wa saba na vifurushi vingine vipo njiani,na viwili vimefika nchini ila sijavipata mkononi nimeona ujumbe kuwa vimefika.
 
Uliagiza mwez wa ngap? Mimi niliagiza mwezi wa tatu, track number hazina update yoyote toka March 15. Sijui hata natatiliaje au nimdai nani

Mwezi wa tatu mwaka huu. Yaani vinakuja kama maji ya kungojea. Kuna cha mwezi wa nne nimepata leo. Vingine bado vipo njiani toka mwezi wa tatu. Vingine vinaonesha vilishakuja hapa nchini lakini sijui vimekwamishwa wapi.
 
Mimi toka mei 5 mpaka sasa sijapata mzigo nikipiga simu namba za posta hawapokei kabisa..nikumuuliza muuzaji anasema wasiliana na wakala wako.. hapo nifanyaje wazee?
 
Mimi toka mei 5 mpaka sasa sijapata mzigo nikipiga simu namba za posta hawapokei kabisa..nikumuuliza muuzaji anasema wasiliana na wakala wako.. hapo nifanyaje wazee?
Pole sana mkuu, mimi tangu february kuna mizigo sijaipata. Ila naamini itafika tu. Ukiona mambo magumu omba wakurefund
 
Habari za asubuhi!ningeomba msaada kujua ofisi za Y&M express zipo sehemu gani kwa hapa Dar es salaama, maana niliagiza bidhaa kupitia kikuu but mzigo haujanifikia mpaka leo
 
Habarini wanna jamvi....
Shida tangu Ni kutaka kujua unapokuta bidhaa mtandaoni imeandikwa mfano: piece/lot 7 maana take Ni ipi?

Je..!!?
Wanamaanisha piece 1 vinakua vitu 12 au hivyo vitu 7 ndio pcs/lot?...

Nifafanulieni kupitia hii bidhaa hapa chini
Screenshot_20200730-162125.jpg
Screenshot_20200730-162035.jpg
 
1. nenda ebay.com kisha register chagua customer au kama wewe ni muuzaji chagua akaunti ya merchant.

2. kujiunga inabidi kadi yako ya benki (visa/mastercard) iwe imesajiliwa kwanza kununua mtandaoni, kisha nenda paypal.com weka details zako na za kadi yako kisha watakutumia verification code (yangu nilichukua crdb) hapo kadi yako itakuwa verified tayari na paypal.

3. nenda sehemu yoyote. wanayokubali paypal nunua chochote, ingiza. detail za paypal, watakata gharama za icho kitu basi umemaliza

very easy
mkuu naomba contact zako unielekeze Zaidi ,nahitaj sana hizo huduma but cjui pa kuanzia
 
Nimesoma huu uzi nmeona maoni tofauti tofauti lkn pia kuna cjui niseme ni kampuni au agent wanaitwa EASYBUY kule mtandaoni nmeona kitu cha usd 7 nikawauliza hadi kinifikie kitagharimu bei gan? Nilipigiwa hesabu hadi ikafika elfu 80 na bado wakaniambia inaweza kuongezeka maana kikifika inabidi kipimwe kilo, wkt kitu chenywe ni suppliments/shampoo. Kwa wenye uzoefu hii ikoje?
 
Back
Top Bottom