Uko sahihi, alibaba waweza kuta wamekuandikia hata $15 ila tambua kuwa
- Bei unayoiona sio bei halisi utakayolipia.
- Bei unayo iona haina shipping cost
- Bei halisi itatokana na express shipment utakayotajiwa
Mfano
- Item utakuta imeandikwa US $15, ila kusafirisha ukaambiwa $120, Tafakari kwa kuangalia mfano hai hapa: Alibaba online mnazingua
- Pitia michango ya wadau
Je nini cha kufanya
#1. Angalia
bei halisi ya item husika amazon.com, ebay.com na aliexpress.com
#2. Chagua muuzaji ambaye bei yake itakuwa ni nafuu ukilinganisha na wauzaji wengine
#3. Kisha nipe link yake.