Jifunze Jinsi ya kufanya Manunuzi kwa Ebay mtandaoni

Unaposema MTU ajiande kulipia kodi mzigo wake ukifika sija kupata fresh

Ni kwa baadhi ya items au?

Maana nimeagiza simu na nimeipata trh 28/09/2020 yaani free kabisa bila tozo yoyote

Embu tolea ufafanuzi
Ulipoagiza hiyo simu hukulipa chochote?? Nje ya gharama ya simu na shipping costs??
 
Naomba ufafanuzi juu ya hili nashindwa kuagiza mzigo e bay kutokana na huu ujumbe unasema shiping address niiupdate.
 
hivi ukitaka simu za iphone na samsung pamoja na laptop za Hp ni application gan nzur kununua yaaan wa coast ya kawaida kati ya aliexpress,ebay,amazon, kama kuna nyingine unayojua na nzur niambie
 
Jaman kwa sie tulioko nje ya Dar, Hivi mzigo ukionekana umefika dar na kukaa zaidi ya wiki mbili bila kuupata huku mkoani, ni wapi pa kuulizia taarifa zake tofauti na hizi office za posta wilayani ambapo ukienda kuuliza jibu ni moju tu kwamba "mzigo hujafika"
 
Hivi mzigo ukionekana umefika dar na kukaa zaidi ya wiki mbili bila kuupata huku mkoani, ni wapi pa kuulizia taarifa zake tofauti na hizi office za posta wilayani
"tofauti na hizi office za posta wilayani"
Hakuna.
Hivi mzigo ukionekana umefika dar na kukaa zaidi ya wiki mbili bila kuupata huku mkoani, ni wapi pa kuulizia taarifa zake
Mahala ulipofungulia sanduku lako la posta ndio unapaswa kufika kwa msaada zaidi.

Wape tracking number ya mzigo wako, wape maelezo au print out kuonyesha mzigo ulipofikia.
- Watawajibika kupiga simu dar es salaam HQ ili kushughurikia mzigo wako.
- Hakikisha unasubiria hapo hapo posta hadi upate jibu la kueleweka kuhusu mzigo wako.
 
Mimi toka mei 5 mpaka sasa sijapata mzigo nikipiga simu namba za posta hawapokei kabisa..nikumuuliza muuzaji anasema wasiliana na wakala wako.. hapo nifanyaje wazee?
Duh I see,leo mimi nimepokea vifurushi ambavyo niliagiza mwezi wa tatu,nilishakata tamaa kabisa. Hii paseli zilishafika wakati ule wa corona maana kila niki-track naona vyote vipo Dsm[emoji23][emoji23][emoji23] bado vichache nasubiria tena
 
Mwl rct nahitaji. Kioo cha ipad ai 2 model 1567 naomba unipe bbei kila kitu adi bongo sitak uniagizie
 
Alibaba nimeona dollar23
Uko sahihi, alibaba waweza kuta wamekuandikia hata $15 ila tambua kuwa
- Bei unayoiona sio bei halisi utakayolipia.
- Bei unayo iona haina shipping cost
- Bei halisi itatokana na express shipment utakayotajiwa

Mfano
- Item utakuta imeandikwa US $15, ila kusafirisha ukaambiwa $120, Tafakari kwa kuangalia mfano hai hapa: Alibaba online mnazingua
- Pitia michango ya wadau

Je nini cha kufanya
#1. Angalia bei halisi ya item husika amazon.com, ebay.com na aliexpress.com
#2. Chagua muuzaji ambaye bei yake itakuwa ni nafuu ukilinganisha na wauzaji wengine
#3. Kisha nipe link yake.
 
petition ilifikia wapi mkuu? it has been a while
 
Naomba ufafanuzi juu ya hili nashindwa kuagiza mzigo e bay kutokana na huu ujumbe unasema shiping address niiupdate.View attachment 1590212
Unatakiwa ufungue shipping address ya Marekani kutoka websites zinasofanya hiyo kazi then hizo websites ndo unawapa shipping address ya bongo hao sellers wautume kwny hiyo shipping address ya Marekani then hayo makampuni yakutumie Bongo
 
Ukitaka kupata bidhaa ambazo huwa zinakuwa na shipping cost moja kwa moja tumia Amazon kwa sababu ndyo digital online marketing site ambayo inaaminika duniani kwa sasa na pia huwa wanajumuisha na import fee
 
Je alibaba wanaweza kuship kwa Po box yangu kama aliexpress? Na km ndio vp kuhusu tracking information?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…