NImenunua kwa gharama ya TSH 644300.. Hii ni pamoja na gharama ya usafirishaji. Simu niliyonunua ni Samsung S4 mini.
Maduka mengi ya Tanzania niliulizia bei yake ilikua 850,000 na kuendelea. Baada ya kusoma post ya
C6 kwamba amefanikiwa kununua kitu ebay na kukipata, na mimi nikapata ujasiri wa kununua.
Note: Nilitengeneza akaunti ebay, kisha nikachagua simu ninayoitaka, baada ya kuona wana ship Tanzania kwa kutumia FedEx ndio nikaamua kununua. Baada ya kununua nikapewa no kwa ajili ya kua na track mzigo wangu. Siku ya jumatatu asubuhi nikapigiwa simu na mtu wa FedEx kua mzigo wangu umefika. Nikaenda FedEX nikachukua simu yangu ikiwakwenye box lake.
Kwenye picha chini hapa unaweza ukaona namna nilivyokua nautrack mzigo wangu
View attachment 113510
View attachment 113511
Ikiwa unahitaji maelezo zaidi usisite kuniuliza. Ila ninaweza kuchelewa kukujibu kutokana na shughuli ninayoifanya