Jifunze Jinsi ya kufanya Manunuzi kwa Ebay mtandaoni

Jifunze Jinsi ya kufanya Manunuzi kwa Ebay mtandaoni

Kwahyo tyr unakuwa na akaunt kwao. Na una uwezo wa kutoa na kuweka hela kama kawaida?
Ndiyo lakini kutoa ni kwa banki zote ambazo zina support Viza na Mastercard.

Kuweka ndiyo lazima uweke kwenye matawi yao tu.
 
Baada ya kuwasiliana naye na kusahihisha shipping address, amenitumia swali lifiatalo " IS THIS THE CORRECT ZIP CODE? +255

Sasa hapo nimjibuje?
Achana na Zip Code maana kwa Bongo ni kama hatuna, unachotakiwa ni kujaza correct address kama ni na mwisho malizia Tanzania, yeye atajua Tz iko wapi, mkoa gani mf Tanga, Tanga wapi Tanga Mjini Mtaa gani Mtaa wa Saba, Box 1145 mzigo utakufikia bila shida
 
Achana na Zip Code maana kwa Bongo ni kama hatuna, unachotakiwa ni kujaza correct address kama ni na mwisho malizia Tanzania, yeye atajua Tz iko wapi, mkoa gani mf Tanga, Tanga wapi Tanga Mjini Mtaa gani Mtaa wa Saba, Box 1145 mzigo utakufikia bila shida

Sure! Tayari
 
simu yangu ya htc ilipasuka kioo, nikatafuta weee, mwisho kuna mtu humu jukwaani akanitajia fundi yupo posta anaitwa sele. nikaenda kufika kaniambua kioo kipo ila bei laki, haipungui wala nini, nikaona pagumu.

mwezi uliopita nikaamua nijaribu ebay nikakuta vioo kibao nikachagua model yangu, nikalipia kwa paypal, kama elfu 36 tu na free shipping.

baada ya wiki 3 nimekipata kioo.

kwa wale wanaohofia kuibiwa au kutapeliwa, mie nimepata bidhaa niliyonunua, nanyi msisite kununua.[/QU
mkuu mie nataka simu je nifanye nini ila nipo TABORA.
 
NImenunua kwa gharama ya TSH 644300.. Hii ni pamoja na gharama ya usafirishaji. Simu niliyonunua ni Samsung S4 mini.
Maduka mengi ya Tanzania niliulizia bei yake ilikua 850,000 na kuendelea. Baada ya kusoma post ya C6 kwamba amefanikiwa kununua kitu ebay na kukipata, na mimi nikapata ujasiri wa kununua.

Note: Nilitengeneza akaunti ebay, kisha nikachagua simu ninayoitaka, baada ya kuona wana ship Tanzania kwa kutumia FedEx ndio nikaamua kununua. Baada ya kununua nikapewa no kwa ajili ya kua na track mzigo wangu. Siku ya jumatatu asubuhi nikapigiwa simu na mtu wa FedEx kua mzigo wangu umefika. Nikaenda FedEX nikachukua simu yangu ikiwakwenye box lake.

Kwenye picha chini hapa unaweza ukaona namna nilivyokua nautrack mzigo wangu
View attachment 113510
View attachment 113511

Ikiwa unahitaji maelezo zaidi usisite kuniuliza. Ila ninaweza kuchelewa kukujibu kutokana na shughuli ninayoifanya

Manunuzi ya Online hadi raha unatrack ka mzigo kako bila shida
Kwa wale ambao wametumiwa mizigo kwa DHL hii inakaa Vipi?Huu mzigo si kwenye Customs umepitishwa?
Na je kama nimeweka P.o box kwenye shipping ntaletewa nilipo au kwenye box langu?au watanipigia simu?

7dot51wjl95ccevhly50.png
 
Kitu muhimu sana ni kuangalia kama wanafanya shipment Tanzania kwa sellers wengi huwa hawaleti Bongo mpaka uwasialiane na seller kwa email.Pili kwa simu hakikisha kuwa network technology iwe GSM siyo CMDA kwani carriers karibu wote Bongo wanatumia GSM
 
Jamani tunaomba feedback kwa wale walionunua vitu hivi karibuni kwa njia ya Posta,vipi gharama?
 
haina haja ya kuogopa ebay.. ukilipa hela haiendi kw muuzaji, inaenda ebay kwanza, hadi upate ulichotumiwa ndio analipwa muuzaji sasa akuibie vipi hapo? hata ukikuta mali mbovu unarudisha refund inafanyika
 
Jamani tunaomba feedback kwa wale walionunua vitu hivi karibuni kwa njia ya Posta,vipi gharama?
Inategemeana na aina ya kitu ukichonunua maana ushuru unatofautiana. Lakini gharama nyingine za ziada hakuna.

Binafsi niliagizaa camcoder Sony Z1U pamoja na tripod yake vilifika haraka na nila shida.

Nilitumia P. O. BOX
 
haina haja ya kuogopa ebay.. ukilipa hela haiendi kw muuzaji, inaenda ebay kwanza, hadi upate ulichotumiwa ndio analipwa muuzaji sasa akuibie vipi hapo? hata ukikuta mali mbovu unarudisha refund inafanyika
Pesa haiendi E bay bali kwa seller na seller wengi hawashipi bila kupata clear payment.

Sema E bay kuna kitu kinaitwa E bay protection kina coverage. Lakini malalamiko yote ya kutokupokea mzigo unayapeleka paypal nao wana kuguarentee buyer na ufedhuli wa maseller japokuwa si occusioj nyingi kwa E bay.
 
Inategemeana na aina ya kitu ukichonunua maana ushuru unatofautiana. Lakini gharama nyingine za ziada hakuna.

Binafsi niliagizaa camcoder Sony Z1U pamoja na tripod yake vilifika haraka na nila shida.

Nilitumia P. O. BOX

Ulilipa ushuru mkuu?
 
1. nenda ebay.com kisha register chagua customer au kama wewe ni muuzaji chagua akaunti ya merchant.

2. kujiunga inabidi kadi yako ya benki (visa/mastercard) iwe imesajiliwa kwanza kununua mtandaoni, kisha nenda paypal.com weka details zako na za kadi yako kisha watakutumia verification code (yangu nilichukua crdb) hapo kadi yako itakuwa verified tayari na paypal.

3. nenda sehemu yoyote. wanayokubali paypal nunua chochote, ingiza. detail za paypal, watakata gharama za icho kitu basi umemaliza

very easy

Naanza elewa somo sasa, wacha niusome uzi wote mpaka mwisho naamini ntapata mengi.
 
Usikute wanaodai kuwa wanapata vitu vyao kwa njia ya posta ndo WALEWALE.

Mwamba ngoma ngozi huvutia kwake. Akili kumkichwa.
Mkuu,inaweza kuwa ndivyo sivyo.
Mimi siyo mfanyakazi wa posta,lakini bidhaa nyingi huwa nazipata kupitia posta na ambazo sipati nakuwa-refunded. Ukitaka kujua utamu wa ngoma, ingia ucheze. Sijawahi kupata hasara kwa kununua bidhaa online.
 
Baada ya kuwasiliana naye na kusahihisha shipping address, amenitumia swali lifiatalo " IS THIS THE CORRECT ZIP CODE? +255

Sasa hapo nimjibuje?
Habari za siku nyingi eBayers.
Kama unanunua bidhaa online na seller aka-ship kwa njia tofauti na Courier Services kama DHL,FEDEX,UPS,TNT au EMS ya posta, mzigo lazima utumwe kwa njia ya posta na unapokelewa kupitia sanduku lako la posta. Sasa kwenye address yako kama Postalcode umeweka tofauti na sanduku lako posta, mzigo uko likely kupotea, maana unakosa pa kwenda,hivyo hata kama haukuwa wa kupotea,ni lazima upotee. Kama ukiwa umeweka namba yako ya simu kwenye address yako, wakikuonea huruma wanaweza kukupigia simu, ingawaje si rahisi maana wewe si mteja wao kama hakuna sanduku la barua kwenye address yako.

Ili kupunguza upotevu wa mizigo, ni vizuri utumwe kwa Registered Mail ili uweze kuu-track na ku-sign wakati wa kupokea.
Hawa wa Courier Services, hutumia Residential address na namba ya simu hivyo kwa kuwa kwa Tz japo postacodes tayari zimetolewa na TCRA, sidhani kama zimeshaanza kutumika, hivyo hata kama kwenye postalcode umeandika madudu, mzigo ukifika kwa ajenti wao, unapigiwa simu kwenda kupokea. pia unakuwa na tracking number.

ANGALIZO:
Huu uzi una majibu mengi sana ya maswali yanayojirudia mara kwa mara, hivyo GT anayetaka kuuliza swali au anahitaji msaada kwenye uzi huu, asome uzi kuanzia mwanzo.

Kw masuala yanayohusiana na posta, yako mwanzoni mwa uzi hasa post #81 na kuendelea.
 
Mimi sina sanduku la posta. Nikinunua bidhaa pale ebay ntapokelea wapi mzigo?
 
Mimi sina sanduku la posta. Nikinunua bidhaa pale ebay ntapokelea wapi mzigo?
Unaweza kutumia sanduku la posta la mtu wako wa karibu. Ila kwenye anuani ni vizuri uweke namba ya simu. Kama ukinunua bidhaa ambazo zina thamani kubwa,si mbaya ukitumia Courier Service Companies,mzigo hautapitia kwenye sanduku la posta,isipokuwa kwa ajenti wa kampuni husika.
 
Back
Top Bottom