the horticulturist
JF-Expert Member
- Aug 24, 2012
- 1,959
- 1,907
Wakulima salama? Mimi ni mkulima mtarajiwa wa nyanya, naomba ushauri wenu na uzoefu, nahitaji kulima nyanya kwny greenhouse, natarajia kuotesha kwny kitalu week mbili zijazo, sasa naomba msaada wa aina nzuri ya mbegu kwa ajili ya kilimo kwny greenhouse, lakini je nikiotesha nyanya kwny kitalu hadi kuvuna kwa mwezi huo wa pili je siwezi kukutana na mavuno ya msimu wa mvua? Hali na bei ya soko itakuwaje? Naomba uzoefu wenu wadau!
Ahsante sana !!
Sent from my HTC Desire 828 using JamiiForums mobile app
Habari
Vipi umepima udongo wa kwenye green house?
Muhimu upime haswa kujua kuhusu magonjwa haswa ya mnyauko bacteria au fungus hii itakuepusha na hasara kubwa sana ya baadae, ili kama kuna matatizo basi ujue utatumia system gani ya kilimo kama utasia direct kwenye udongo au kama utatumia mifuko na udongo wa kutibu.
Ukiwa na udongo usio na matatizo yoyote na ukipata mbegu bora unaweza vuna nyanya kwa miezi sita mpaka nane kwa hapa tunapoenda bei ya nyanya itashuka from mwezi wa nne mpaka wa tisa hivi na wewe ukisia sasa hivi utaanza kuvuna from mwezi wa tano ukiitunza vyema mpaka November au December means wakati bei inapanda na wewe ndio utakua umemaliza kuvuna kama vipi tazama soko kwanza la nyanya, hoho au tango sababu ukiweka tango ni miezi mitatu atleast mpaka kuisha hivyo baada ya kutoa tango unaweza sasa ukaweka nyanya. Tazama soko kabla hujaweka kitu sema pia unalimia mkoa gani wenyeji watakupa details zaidi za uliko pia, mimi niko Arusha kipindi hiki watu wanaandaa mashamba ya nyanya za miradi, huwa zinavuruga soko sana.
Mbegu bora
Tango:
Mydas -rijk zwaan
Massa - rijk zwaan
Tango ya green house lazima iwe parthenocapic yaani isiyohitaji uchavushaji sababu kwenye green house hakuna nyuki ukipanda variety ya tofauti na hizo hapo juu utakua umeotesha maua tu.
Nyanya
Tylka - syngenta
Monteazul -rijk zwaan
Victory -east west seed
Anna f1 etc
Nyanya lazima iwe nyanya ndefu (indeterminate) kwa mavuno ya muda mrefu.
Hoho
Red jet
Pasirella
Ilanga (rijk zwaan)
Balton pia wanazo za rangi
Syngenta pia wanazo
Inabidi ulime za rangi ili usiwe na mzigo sawa na wanaolima nnje