Jifunze kuendesha (ku-control) nafsi ili kujikomboa katika vifungo na kuwa msaada kwa wengine

Mimi nadhani maswali mengine majibu anayajua Mungu mwenyewe,

Huwezi kutoa majibu yaliyonyooka, kwa sababu huyo Mungu hayupo.

Wewe kutojua majibu ya maswali mengine pia ni ushahidi kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Kimantiki iko hivi.

1. Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, anatutakia mema yote na hatutakii mabaya yoyote. Hiyo ndiyo nature yake kimantiki. Mungu huyo kututakia mabaya ni contradiction.

2. Kuna ujinga mwingi sana ambao ni mbaya. Nilikuwa naangalia documentary moja ya kuhusu "The Black Death". Watu walivyokufa sana kqa Bubonic Plague Ulaya na Asia, huku wakishindwa kujua chanzo cha ugonjwa na jinsi ya kuutibu. Tumeshindwa kugundua madawa ya antibiotics kisayansi kwa miaka yote mpaka hapa 1928, that is not even a 100 years ago. Watu walikuwa wanakufa kwa vitu vidogo tu kama vidonda, kwa kukosa antibiotics. Huo ni ujinga mkubwa sana ulious watu wengi sana.

3. Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote, angekuwepo,asingetubania kutupa dawa miaka yote hiyo. Watu wamemuomba sana. Hizo sifa zakw zinatuonesha Mungu wa hivyo si mchoyo.

4. Logical conclusion. Mungu wa hivyo hayupo. In fact ukijisikia umepungukiwa na inahitaji kuomba kitu tu, huo ni ushahidi kwamba Mungu hayupo. Kwa sababu, angekuwepo, angekupa unachohitaji kabla hujamuomba.
 
Uwezo huo anao ndio maana unasikia kuna peponi/paradise.

Mwanzo katika bustani ya Eden Adam na Hawa waliishi waliishi kiroho lakini baada tu ya kukengeuka kwa kumshawishiwa na nyoka gafla walijikuta wame-unlock ulimwengu wa kimwili ndipo wakashtuka kuwa wapo uchi ila katika ulimwengu wa kiroho hawa kuona kua hilo ni tatizo.

Sasa MUNGU kwa kutumia houhuo upendo wake na haki hakutaka kuwafyekelea mbali. Aliwaacha kwa makusudi ya kwamba wao wenyewe watambue wamekosea wapi na nani kati ya MUNGU na shetani ni muongo maana shetani alidai kwamba Mungu ni muongo.(circular argument kwa mara nyingine tena).

Kwahiyo hizi changamoto katika ulimwenguni wa kimwili tulichagua wenyewe kwa kumuasi Mungu.

Mazingira ya peponi na duniani ni tofauti hapa duniani tunaishi kimwili zaidi na ili tuendane na mazingira ya duniani MUNGU alituumbia na miili ambayo physically physiologically (biologically & chemically) psychologically and even behavioural ipo adapted kwa duniani ili tuweze kuishi.

Sasa ukiachana na Community level katika echo-systems ambayo ni much more complex, twende kwenye population level specifically human beings...

Haya mapungufu unayoyaona kutohautiana tabia maumbile upeo na fikra na hata mazingira, ukiwa wise enough ukaya-zoom katika big picture utagundua kua ndio ukamilifu wenyewe huo, eee ndio yaani haya mapungufu ndio ukamilifu wenyewe. Hasa ukizingatia muingiliano within and between population katika community(Balance of nature).

Kuna mfumo mingine unatakiwa iwe negative au positive inhibition katika feedback mechanisms.

Ila ukitaka ukamilifu wa kila kitu basi kwa wanaoamini kuna sehemu inaitwa peponi huko nadhani hakuhitaji miili hii wala hakuhitaji kuadapt mazingira popote una-survive eg katika degree yoyote ya temperature, pH pressure, kiufupi unakua flexible na hakuna mipaka ya muda wala nafasi(ukitaka uwe currently light year au million light years back or future ama unataka kuwa mwezini Mars.
Mimi nakuuliza, kwa nini Mungu kaumba ulimwengu unaoruhusu mabaya wakati aliweza kuumba ulimwengu usioruhusu mabaya?

Wewe unajibu uwezo huo anao ndiyo maana unasikia peponi.

Kwanza peponi hakuna mtu mwenye ushahidi kwamba kupo.

Pili, hujaelewa swali. Siongelei peponi ambako hatuna ushahidi kwamba kupo, naongelea ulimwengu huu ambao tuna ushahidi kwamba upo.

Kwa nini Mungu kaumba ulimwengu unaoruhusu mabaya wakati aliweza kuumba ulimwengu usioruhusu mabaya?

Unaandika Adamu na Hawa walikengeuka kwa kushawishiwa na nyoka, kwa nini Mungu aliumba ulimwengu ambao kukwngeuka kunawezekana kufanyika badala ya kuumba ulimwengu ambao kukengeuka hakuwezekani?
 
Mkuu hizo contradiction nyingi unazozisema majibu yake yapo hapa👇👇👇
**Ona hekima ya MWENYEZI MUNGU mambo yote yako ndani ya uwezo wake lakini kwa kuwa yeye ni MUNGU wa haki hataki/haoni kama ni busara kukulazimisha wewe umfuate yeye wala hataki kukushawishi wala kukutisha kwa namna yoyote ile umpende yeye... anachotaka wewe mwenyewe kwa uhuru wako kutoka Moyoni mwako uamue kumfuata (yaani kwa hiari yako)
Kuna ulimwengu wa kiroho na ulimwenguni wa kimwili huu ulimwenguni wa kimwili sisi binadamu ndio tu naona issue lakini kwa Mungu haoni kama ni Big deal kwake ndio maana tunakufa (yaani duniani tunapita (NI kama tupo kwenye mchujo fate ya wewe utakua wapi baada ya kifo unaiamua mwenyewe kwa utashi wako (NI haki yako umepewa uhuru huo))) kati ya ulimwenguni wa kiroho wa nuru na giza.

Na Kwakua hauutilii manani ulimwengu wa kiroho na nakushauri umtafute Mungu mwenyewe unaona kama nakupiga chenga basi mimi nitakua sina la ziada kwasababu najua kuyaelezea kimwili mwili haya mambo hatutoboi hapa tutakesha.

Nilishakuweka wazi kuwa kuyaelezea mambo ya kiroho kwa kanuni za kimwili ni changamoto. Unaweza ukahisi watu wamewehuka kumbe Hapana.

Usiishie kupinga tu jaribu kumtafuta sio lazima uende kwenye nyumba za ibada dhamilia wewe kama wewe.
 
Kwani Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya ambao pia hakulazimishi umfuate yeye?

Ukishaona unahitaji kumtafuta Mungu tu, ujue Mungu huyo hayupo.

Mungu angekuwepo, kusingekuwa na haja ya kumtafuta, angejidhihirisha kwa kila mtu, kwa uhakika kabisa, hata mjadala wa kuuliza kama Mungu yupo usingewezekana.

Kwa hivyo, wewe kuniambia nimtafute Mungu, na majadala wa kuwepo Mungu kuwezekana, ni ushahidi kwamba Mungu hayupo.
 
"Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote, angekuwepo,asingetubania kutupa dawa miaka yote hiyo. Watu wamemuomba sana. Hizo sifa zakw zinatuonesha Mungu wa hivyo si mchoyo."

Mungu aliumba kila kitu, Aliumba mimea mbali mbali kwajili ya matumizi mbali mbali ikiwemo dawa, Hivyo madai yako kuwa anatubania si kweli.
 
Kwani Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya ambao pia hakulazimishi umfuate yeye?

Ukishaona unahitaji kumtafuta Mungu tu, ujue Mungu huyo hayupo.

Mungu angekuwepo, kusingekuwa na haja ya kumtafuta, angejidhihirisha kwa kila mtu, kwa uhakika kabisa, hata mjadala wa kuuliza kama Mungu yupo usingewezekana.

Kwa hivyo, wewe kuniambia nimtafute Mungu, na majadala wa kuwepo Mungu kuwezekana, ni ushahidi kwamba Mungu hayupo.
Siku moja utabadilika mkuu, Nnae rafiki yangu alikua atheist na hoja kali kali alizoziunda kuthibitisha madai yake, hizi hoja zako zote si ngeni kwangu.

Alibadilika, Alikutana na mkasa ambao haukua wa hali ya kawaida.

Hata wewe ni swala la muda tu hakuna atakaekuja kukuthibitishia kuhusu uwepo wake ila atakuja yeye mwenyewe kwenye maisha yako na utamjua,,

Utakua mwalimu mzuri sana kwa wengine.
 
Mimi kubadilika si hoja.

Hoja ni Mungu yupo au hayupo?

Sasa, mimi nikibadilika na kukubali Mungu yupo, kama hayupo, huko kubadilika kwangu ndiko kutafanya Mungu awepo?

Mbona unashindwa kujadili hoja kubwa na muhimu, kimantiki, kidhahania, kwamba Mungu yupo au hayupo?

Mbona unashindwa kuthibitisha Mungu yupo?

Mbona unakwenda kwenye hoja ndogo, isiyo na umuhimu, ya imani yangu mimi binafsi?

Usinifanye mimi kuwa hoja, mimi ni mtu mmoja tu, mdogo tu. Mimi si hoja hapa.

Jikite kwenye hoja kubwa yenye umuhinu kwa watu wote ambayo ilikuwa na umuhimu kabla mimi sijazaliwa na itaendelea kuwa na umuhimu hata baada ya mimi kufariki.

Thibitisha Mungu yupo.

Ukianza kuacha hiyo kazi ya kuthibitisha Mungu yupo, na kujikita kwenye kuniambia mimi nitaamini tu siku moja, unanionesha kuwa huwezi kuthibitisha Mungu yupo na unaleta distraction tu kusema siku moja nitaamini Mungu yupo.

Umeshindwa hoja, unaleta viroja.
 
Nianze na salamu za mwaka huu wa 2024 kwa wanajukwaa wote,nilibanwa kidogo na shughuli nyingi mwaka huu ila sasa nimerudi tena jukwaani.

Tunaanza; Tambua kuwa nafsi ndiyo sehemu ya mtu iliyobeba hatma yake yote awapo hapa duniani. Kazi ya roho ni kutia nguvu tu vilivyopo kwenye nafsi ili mtu aweze kuishi katika kiwango chake cha maisha.

Sasa, ili uweze kufanikiwa katika haya maisha na watu wote ambao tayari wameshafanikiwa, ni lazima uwe na uwezo mkubwa wa ku control (kuendesha) nafsi za wengine ili zikutumikie kwa vipawa vilivyopo ndani yake ndipo ufanikiwe.

Namaanisha kuwa unaweza kuishi hapa duniani na ukawa unatumikia watu wengine maisha yako yote kwa nafsi yako kukamatwa na kuendeshwa na watu hao.

Hapa tunazungumzia masuala ya kiroho. Katika ulimwengu wa kiroho upande wa nuru na upande wa giza,wote huvuta watu,kuwafunga na kuwaendesha kwa namna watakavyo wao ili wao waweze kufikia hatma zao.

Tuangalie mifano kidogo, wafanyabiashara; ili bidhaa zao ziuzike lazima wavute na ku control nafsi za watu, usije ukaona unapendelea kununua bidhaa zako sehemu fulani ukafikiri ni kawaida tu!,nafsi imekamatwa hapo. Watu wengine ni wanasiasa, kwenye mipira,kwenye uongozi, kwenye kuvuta wateja kwenye taasisi na mashirika mbalimbali hususani sekta binafsi na wahubiri wakubwa.

Wote hawa wakikosa nguvu za kuvuta na ku control nafsi za watu ili ziwatumikie,kamwe hawataweza kufanikiwa!. Sasa kazi itaanzia hapa kwa kujifunza vitu wanavyotumia kuvuta na ku control nafsi za watu katika pande zote za nuru na za giza. Vitu vinavyotumika ni;

1. Kiapo (maneno yenye ahadi kamili).

2. Sadaka (fedha au chochote kwa lengo maalumu).

3. Maneno/Maombi (yenye roho ndani yake).

4. Kiwakilishi chako chochote (mfano nguo au picha).

Nitakuwa nachambua kimoja kimoja kadri muda utakavyokuwa unapatikana na ninaimani watu wengi sana watajikomboa kutoka kutumikishwa na watu wengine na watajua mengi sana na siri nyingi sana na kuwa huru kuendesha maisha yao.

NB; Hakuna nafsi yoyote ya mwanadamu isiyokuwa na thamani,kama unataka kuamini we nenda kwa Mungu au kwa shetani ukiwa hali yoyote uone kama atakukataa!,na ukifuata masharti yao kikamilifu utakuwa milionea pasipo kujali ulikuwa katika hali gani ya nafsi yako.
Mkuu karibu sana naona umekuja kivingine huwa nakuelewa sana uwezo wako kimaarifa na kwa wanaozingatia matokeo yanajitokeza wazi wazi mimi nikiwa mmoja wamashuhuda kwenye lile andiko la Damu katika ulimwengu wa nuru...tupo pamoja[emoji120]
 
Mimi kubadilika si hoja.

Hoja ni Mungu yupo au hayupo?

Sasa, mimi nikibadilika na kukubali Mungu yupo, kama hayupo, huko kubadilika kwangu ndiko kutafanya Mungu awepo?

Mbona unashindwa kujadili hoja kubwa na muhimu, kimantiki, kidhahania, kwamba Mungu yupo au hayupo?

Mbona unashindwa kuthibitisha Mungu yupo?

Mbona unakwenda kwenye hoja ndogo, isiyo na umuhimu, ya imani yangu mimi binafsi?

Usinifanye mimi kuwa hoja, mimi ni mtu mmoja tu, mdogo tu. Mimi si hoja hapa.

Jikite kwenye hoja kubwa yenye umuhinu kwa watu wote ambayo ilikuwa na umuhimu kabla mimi sijazaliwa na itaendelea kuwa na umuhimu hata baada ya mimi kufariki.

Thibitisha Mungu yupo.

Ukianza kuacha hiyo kazi ya kuthibitisha Mungu yupo, na kujikita kwenye kuniambia mimi nitaamini tu siku moja, unanionesha kuwa huwezi kuthibitisha Mungu yupo na unaleta distraction tu kusema siku moja nitaamini Mungu yupo.

Umeshindwa hoja, unaleta viroja.
Sawa mimi nna maswali baada ya swali ambalo nataka kukuuliza,

Swali: Unaamini/Kufahamu chochote kuhusu "Kiroho" ( Spirituality ) ?
 
Roho/Spirituality ni dhana pana sana.

Wiki iliyopita kuna mtu ali post uzi akielezea habari za roho za umasikini kwenye famikia na jinsi ya kuziondoa.

Nikawa kama nimemuelewa kwa upande fulani.

Kuna mtu akaja akawa kama kanishangaa hivi, akaniuliza, hata wewe unaamini haya mambo ya roho?

Nikamuelewesha kwamba mimi siamini katika kuwapo kwa roho inayoendelea kuishi baada ya kifo, ila, neno roho ni pana sana, mtu anaweza kuelezea roho ya ubepari, the spirit of capitalism, that is a real thing. Hilo ni jambo la utamaduni, ni jambo la kisaikolojia. Max Weber kaandika kitabu "The Protestant Ethic and The Spirit of Capitalism".

Sasa, unapoandika "kiroho" unamaanisha nini?

Kama kusoma uwepo wa roho na mambo ya dini, mimi nimesoma.

Nimesoma Biblia, kwetu pande zote mbili ni kanisani.

Nimesoma Quran.

Nimesoma Dhammapada, nimeitafsiri kwenda Kiswahili. Nenda Upanga Buddhist Temple Mindu St utaikuta.

Nimesoma Tripitaka.

Nimesoma The Uppanishads.

Nimesoma Bhagavad Gita.

Nimesoma Rig Vedas.

Nimesoma Tibetan Book of The Dead.

Nimesoma Egyptian Book of the Dead.

Nimesoma Talmud.

Ninesoma Philosophy of Religion, an Anthology.

Nimesoma The Norton Anthology of World Religions.

Hivyo vinatosha, au niongeze kuorodhesha vingine?

20240310_110548.jpg
 
Roho/Spirituality ni dhana pana sana.

Wiki iliyopita kuna mtu ali post uzi akielezea habari za roho za umasikininkwenye famikia na jinsi ya kuziondoa.

Nikawa kama nimemuelewa kwa upande fulani.

Kuna mtu akaja akawa kama kanishangaa hivi, akaniukiza, hata wewe unaamini haya mambo ya roho?

Nikamuelewesha kwamba mimi siamini katikankuwapo kwa roho inayiendelea kuishi baada ya kifo, ila, neno roho ni oana sana, mtu anaweza kuelezea roho ya ubwpari, tge spirit of capitalism, that is a real thing. Hilo ni jambo la utamaduni, ni jambo la kisaikolojia. Max Weber kaandika kitabu "The Protestant Ethuc and The Spirit of Capitalism".

Sasa, unapoandika "kiroho" unamaanisha nini?

Kama kusomanuwepo wa roho na mambo ya dini, mimi nimesoma.

Nimesoma Biblia, kwetu pande zote mbiki ni kanisani.

Nimesoma Quran.

Nimesoma Dhammapada, nimeitafsiri kwenda Kiswahili. Nenda Upanga Buddhist Temple Mindu St utaikuta.

Nimesoma Tripitaka.

Nimesoma The Uppanishads.

Nimesoma Bhagavad Gita.

Nimesoma Rig Vedas.

Nimesoma Tibetan Book of The Dead.

Nimesoma Egyptian Book of the Dead.

Nimesoma Talmud.

Ninesoma Philosophy of Religion, an Anthology.

Nimesoma The Norton Anthology of World Religions.

Hivyo vinatosha, au niongeze kuorodhesha vingine?
Hapana inatosha ahsante kwa kunifahamisha na mengine ambayo nlikua sifahamu.

Nna swali ambalo miaka ya nyuma nlikua sielewi vizuri, Lakini sasa naelewa ila napenda kufahamu watu wengine wana mtazamo gani/wanajua nini kuhusu hilo

Ni hivi; Kuna ndoto ambazo huwa naota ( Na wengine wengi huota )

Naota jambo ambalo halichukui siku nyingi linatokea,,

Nmekumbuka kukuuliza baada ya tukio lililotokea jana

Ni tukio ambalo nmeota week iliyopita tu na jana majira ya saa1 jioni likatokea.

Kabla ya hili tukio kuna tukio lingine lilitokea mwezi uliopita ambalo na hilo nliota week kadhaa kabla halijatokea.

Swali; Mara nyingi huwa unasema mambo yanapimwa au kutafsiriwa kwa misingi ya kisayansi
Je unaweza kunielezea kuhusu haya kwa misingi ya kisayansi ? Au unafahamu nini kuhusu haya ?
 
Ndoto ni mkusanyiko wa mawazo yetu.

Mawazo yetu yanachangiwa na vitu vingi sana, vingine tuna vi process katika level ya conscious, vingine tuna vi process katika level ya subconscious.

Hivi vya level ya subconscious ni vigumu sana kuvielewa na kuvitrack. Tunaweza kuwa tunajua kitu, tumekiona, tumekisikia, lakini kipo katika subconscious mind, hatujui kwamba tunakijua.

Nitakupa mifano miwili.

Mimi napenda sana muziki. Tena awali nilikuwa nafuatilia sana mwanamuziki gani katoa muziki gani, nk.

Muda mrefu nilimfuatilia mwanamuziki Norah Jones, alishinda grammy nyingi sana katika jazz kuanzia mwaka 2003 mpaka mwaka 2008.

Halafu akawa kama kapotea.

Sasa wiki iliyopita, nikajikuta tu najiuliza, hivi, Norah Jones yuko wapi siku hizi? Mbona miaka mingi sijamsikia?

Kuja kuangalia habari, nikakuta wiki hiyo hiyo niliyomkumbuka Norah Jones ndiyo wiki ambayo Norah Jones ana release album mpya. March 8 2024.

Sasa, hapo kama mtu amekaa kwenye kuamini clairvoyance, kujua mambo ya mbali bila kuambiwa, anaweza kuamini kuwa yeye ni clairvoyant, kajua hii habari bila kuambiwa.

Kwangu mimi, hapo naona kuwa ni suala la subconscious memory tu. Kuna sehemu nilisikia au kuona in passing kwamba Norah Jones anatoa album wiki hii. Halafu ile habari sikuitilia maanani sana, siku i register kama nimeipata. Halafu ile habari ika play back, nikajiona kama mimi ndiye naanza kuifikiria, nikaona kama mimi ndiye naanza kumkumbuka Norah Jones.

Kuja ku Google, nakuta Norah Jones ana release album wiki hiyo hiyo niliyomkumbuka na kum Google, baada ya miaka mingi ya kusahaulika.

Nitakupa mfano mwingine ambao mimi huwa unanitokea sana. Na hili jambo linaweza kuwa linawatokea watu wengi ila hawajui tu.

Mimi napenda sana kufuatilia habari. Mara nyingine nalala nikisikiliza habari, hususan BBC. Sasa, mara nyingine, ninapolala huku nasikiliza habari, zile habari zinajipenyeza kwenye ndoto zangu, zinakuwa kama ndoto naota.

So, lets say kuna tetesi za machafuko yanayoanza kutokea huko Sierra Leone. Mimi nimelala nasikiliza BBC. Zile habari nazisikia kwenye masikio yangu, lakini kwa sababu nimelala, zinaingia kwenye ndoto. Naona naota wanajeshi wa Sierra Leone wanaanzisha machafuko ya kupindua nchi. Naamka, nakumbuka sehemu ndogo za hiyo ndoto, naipotezea tu.

Baada ya wiki, zile tetesi zinakamilika, wanajeshi wanapindua nchi.

Hapo kama mimi ni mtu wa kuamini kuwa ndoto zinatabiri mambo, nitaamini nililala, niliota hili jambo, ndoto zangu zimeniwezesha kujua hili jambo.

Kumbe ndoto zenyewe zimetokana na taarifa ya habari ya BBC iliyoanza kuripoti machafuko hayo, na mtu yeyote ambaye anafuatilia habari angeweza kubashiri kwamba mapinduzi ya kijeshi yanaweza kutokea huko Sierra Leone.

Kwa hivyo, huwa kuna namna ambayo tunapata ku process habari na kuziota, halafu, zikitimia, tunaweza kujiona tumetabiri kikichotokea kwa ndoto zetu.
 
Kuja ku Google, nakuta Norah Jones ana release album wiki hiyo hiyo nikiyomkumbuka na kum Google, baada ya miaka mingi ya kusahaulika.

Nitakupa mfano mwingine ambao mimi huwa unanitokea sana. Na hili jambo linaweza kuwa linawatokea watu wengi ila hawajui tu.

Mimi napenda sana kufuatilia habari. Mara nyingine nalala nikisikiliza habari, hususan BBC. Sasa, mara nyingine, ninapolala huku nasikiliza habari, zile habari zinajipenyeza kwenye ndoto zangu, zinakuwa kama ndoto naota.

So, lets say kuna tetesi za machafuko yanayoanza kutokea huko Sierra Leone. Mimi nimelala nasikiliza BBC. Zile habari nazisikia kwenye masikio yangu, lakini kwa sababu nimelala, zinaingia kwenye ndoto. Naona naota wanajeshi wa Sierra Leone wanaanzisha machafuko ya kupindua nchi. Naamka, nakumbuka sehemu ndogo za hiyo ndoto, naipotezea tu.

Baada ya wiki, zile tetesi zinakamilika, wanajeshi wanapindua nchi.

Hapo kama mimi ni mtu wa kuamini kuwa ndoto zinatabiri mambo, nitaamini nililala, niliota hili jambo, ndoto zangu zimeniwezesha kujua hili jambo.

Kumbe ndoto zenyewe zimetokana na taarifa ya habari ya BBC iliyoanza kuripoti machafuko hayo, na mtu yeyote ambaye anafuatilia habari angeweza kubashiri kwamba mapinduzi ya kijeshi yanaweza kutokea huko Sierra Leone.

Kwa hivyo, huwa kuna namna ambayo tunapata ku process habari na kuziota, halafu, zikitimia, tunaweza kujiona tumetabiri kikichotokea kwa ndoto zetu.
Ulianza kueleza vizuri na tulikua tunaenda sambamba hadi ulipofika kwenye mifano yako ya kusikiliza sauti kutoka kwenye vifaa kama hiyo tv au Radio na athari zake kwenye ndoto hapo umeniacha,

Hata mimi nimeota ndoto za namna hiyo na naelewa namna ya kutofautisha hivyo nlichoomba unipe ufafanuzi hakihusiani na majibu ya kuanzia hapo kwenye mifano uliyoitoa.

Maelezo yangu na ulichojibu naweza nikasema bado haujanijibu,

Pengine jibu lako lilipaswa kuishia ulipozungumzia kuhusu ugumu wa kutrack baadhi ya mambo yanayohusu subsconsious.

Matukio yote mawili nliyoyaota na yakatokea hayahusiani na mifano yako kabisa, Ni mambo ya kufikirisha kama nsingekua nna uelewa kuhusu ufahamu wangu kuyahusu.

Na niongezee, hili tukio la jana nliota siku mbili mfululizo week hiyo iliyoisha, Na jana baada ya kutokea baadae ndio nikawa nakumbuka kuhusu zile ndoto.
 
Mkuu,

Sasa kama ni vigumu kujua kipi unakiota kwa kusikia taarifa ya habari na kipi ni ndoto tu, utajuaje ndoto ipi ni ndoto tu na ndoto ipi imechagizwa na mambo yanayokuzunguka?

Mifano yangu ina illustrate point, sijasema kuwa ndoto zako zimetokea kama kwenye mifano yangu, how is that not valid?
 
Wakuu mmegusia masuala ya ndoto na Mtaalam Kiranga katolea uchambuzi wa kisayansi Kuhusu experience yake katika ndoto, subconscious mind & clairvoyance mchango wenu nzuri sana na_ appreciate👍.

Mambo mengi muda mchache ninatamani na mimi nichangie uzoefu wangu katika hizi ndoto kwani nishaota matukio kadhaa kabla hayajatokea katika namna isiyo ya kawaida.

Tushamkosea sana huyu mwenzetu alietenga muda kuandaa uzi itakuwa sio busara kuendelea na mada ingawa imezaliwa humuhumu.

Mkuu Walker Water tunaomba radhi kwa yaliyoendelea humu, pia Karibu kwa kuliendeleza somo kwani tunalihitaji kwa shauku kubwa.

Asante.
 
Mkuu Walker water kama ujapendenzwa na kinacho endelea hapa nakuomba unaweza kuanzisha uzi upya ili tujifunze zaidi

Kuna uzi nyingi sana hapa JF ambazo zinazungumzia mambo ya kuwepo kwa Mungu yupo au hayupo mnaweza kwenda huko kuliko kupoteza maana ya kinachotakiwa kuzungumziwa humu

Ahsanteni.
 
Uwezo huo anao ndio maana unasikia kuna peponi/paradise.

Mwanzo katika bustani ya Eden Adam na Hawa waliishi waliishi kiroho lakini baada tu ya kukengeuka kwa kumshawishiwa na nyoka gafla walijikuta wame-unlock ulimwengu wa kimwili ndipo wakashtuka kuwa wapo uchi ila katika ulimwengu wa kiroho hawa kuona kua hilo ni tatizo.

Sasa MUNGU kwa kutumia houhuo upendo wake na haki hakutaka kuwafyekelea mbali. Aliwaacha kwa makusudi ya kwamba wao wenyewe watambue wamekosea wapi na nani kati ya MUNGU na shetani ni muongo maana shetani alidai kwamba Mungu ni muongo.(circular argument kwa mara nyingine tena).

Kwahiyo hizi changamoto katika ulimwenguni wa kimwili tulichagua wenyewe kwa kumuasi Mungu.

Mazingira ya peponi na duniani ni tofauti hapa duniani tunaishi kimwili zaidi na ili tuendane na mazingira ya duniani MUNGU alituumbia na miili ambayo physically physiologically (biologically & chemically) psychologically and even behavioural ipo adapted kwa duniani ili tuweze kuishi.

Sasa ukiachana na Community level katika echo-systems ambayo ni much more complex, twende kwenye population level specifically human beings...

Haya mapungufu unayoyaona kutohautiana tabia maumbile upeo na fikra na hata mazingira, ukiwa wise enough ukaya-zoom katika big picture utagundua kua ndio ukamilifu wenyewe huo, eee ndio yaani haya mapungufu ndio ukamilifu wenyewe. Hasa ukizingatia muingiliano within and between population katika community(Balance of nature).

Kuna mfumo mingine unatakiwa iwe negative au positive inhibition katika feedback mechanisms.

Ila ukitaka ukamilifu wa kila kitu basi kwa wanaoamini kuna sehemu inaitwa peponi huko nadhani hakuhitaji miili hii wala hakuhitaji kuadapt mazingira popote una-survive eg katika degree yoyote ya temperature, pH pressure, kiufupi unakua flexible na hakuna mipaka ya muda wala nafasi(ukitaka uwe currently light year au million light years back or future ama unataka kuwa mwezini Mars.
Yaani mtu na dadaye wangonoke kwenye nyumba ya baba yao,halafu wafukuzwe na kukimbilia nchi ya jirani,na huko waanzishe maisha mapya ya ku-hussle then watu waibinue story chini juu na watu tuiamini na kuifuata katika maisha yetu yote!!!!!!!

...........gwa na kitu kizito since then. Kile kitabu ukikifungua unaanza kusoma historia ya vizazi vya familia za ulaya.
Bado natafakari na kutafakuri.
 
Mkuu,

Sasa kama ni vigumu kujua kipi unakiota kwa kusikia taarifa ya habari na kipi ni ndoto tu, utajuaje ndoto ipi ni ndoto tu na ndoto ipi imechagizwa na mambo yanayokuzunguka?

Mifano yangu ina illustrate point, sijasema kuwa ndoto zako zimetokea kama kwenye mifano yangu, how is that not valid?
Mimi nalala bila sauti za music wala taarifa ya habari, na mazingira yangu ni ya ukimya hata wakati wa mchana tu,

Bado swali langu ni; Unaweza kuelezea ndoto ambazo zinakuja kwenye uhalisia ?

Au hadi nizielezee hizo ndoto utaelewa nini hasa namaanisha ?
 
Back
Top Bottom