Hapana inatosha ahsante kwa kunifahamisha na mengine ambayo nlikua sifahamu.
Nna swali ambalo miaka ya nyuma nlikua sielewi vizuri, Lakini sasa naelewa ila napenda kufahamu watu wengine wana mtazamo gani/wanajua nini kuhusu hilo
Ni hivi; Kuna ndoto ambazo huwa naota ( Na wengine wengi huota )
Naota jambo ambalo halichukui siku nyingi linatokea,,
Nmekumbuka kukuuliza baada ya tukio lililotokea jana
Ni tukio ambalo nmeota week iliyopita tu na jana majira ya saa1 jioni likatokea.
Kabla ya hili tukio kuna tukio lingine lilitokea mwezi uliopita ambalo na hilo nliota week kadhaa kabla halijatokea.
Swali; Mara nyingi huwa unasema mambo yanapimwa au kutafsiriwa kwa misingi ya kisayansi
Je unaweza kunielezea kuhusu haya kwa misingi ya kisayansi ? Au unafahamu nini kuhusu haya ?
Ndoto ni mkusanyiko wa mawazo yetu.
Mawazo yetu yanachangiwa na vitu vingi sana, vingine tuna vi process katika level ya conscious, vingine tuna vi process katika level ya subconscious.
Hivi vya level ya subconscious ni vigumu sana kuvielewa na kuvitrack. Tunaweza kuwa tunajua kitu, tumekiona, tumekisikia, lakini kipo katika subconscious mind, hatujui kwamba tunakijua.
Nitakupa mifano miwili.
Mimi napenda sana muziki. Tena awali nilikuwa nafuatilia sana mwanamuziki gani katoa muziki gani, nk.
Muda mrefu nilimfuatilia mwanamuziki Norah Jones, alishinda grammy nyingi sana katika jazz kuanzia mwaka 2003 mpaka mwaka 2008.
Halafu akawa kama kapotea.
Sasa wiki iliyopita, nikajikuta tu najiuliza, hivi, Norah Jones yuko wapi siku hizi? Mbona miaka mingi sijamsikia?
Kuja kuangalia habari, nikakuta wiki hiyo hiyo niliyomkumbuka Norah Jones ndiyo wiki ambayo Norah Jones ana release album mpya. March 8 2024.
Sasa, hapo kama mtu amekaa kwenye kuamini clairvoyance, kujua mambo ya mbali bila kuambiwa, anaweza kuamini kuwa yeye ni clairvoyant, kajua hii habari bila kuambiwa.
Kwangu mimi, hapo naona kuwa ni suala la subconscious memory tu. Kuna sehemu nilisikia au kuona in passing kwamba Norah Jones anatoa album wiki hii. Halafu ile habari sikuitilia maanani sana, siku i register kama nimeipata. Halafu ile habari ika play back, nikajiona kama mimi ndiye naanza kuifikiria, nikaona kama mimi ndiye naanza kumkumbuka Norah Jones.
Kuja ku Google, nakuta Norah Jones ana release album wiki hiyo hiyo niliyomkumbuka na kum Google, baada ya miaka mingi ya kusahaulika.
Nitakupa mfano mwingine ambao mimi huwa unanitokea sana. Na hili jambo linaweza kuwa linawatokea watu wengi ila hawajui tu.
Mimi napenda sana kufuatilia habari. Mara nyingine nalala nikisikiliza habari, hususan BBC. Sasa, mara nyingine, ninapolala huku nasikiliza habari, zile habari zinajipenyeza kwenye ndoto zangu, zinakuwa kama ndoto naota.
So, lets say kuna tetesi za machafuko yanayoanza kutokea huko Sierra Leone. Mimi nimelala nasikiliza BBC. Zile habari nazisikia kwenye masikio yangu, lakini kwa sababu nimelala, zinaingia kwenye ndoto. Naona naota wanajeshi wa Sierra Leone wanaanzisha machafuko ya kupindua nchi. Naamka, nakumbuka sehemu ndogo za hiyo ndoto, naipotezea tu.
Baada ya wiki, zile tetesi zinakamilika, wanajeshi wanapindua nchi.
Hapo kama mimi ni mtu wa kuamini kuwa ndoto zinatabiri mambo, nitaamini nililala, niliota hili jambo, ndoto zangu zimeniwezesha kujua hili jambo.
Kumbe ndoto zenyewe zimetokana na taarifa ya habari ya BBC iliyoanza kuripoti machafuko hayo, na mtu yeyote ambaye anafuatilia habari angeweza kubashiri kwamba mapinduzi ya kijeshi yanaweza kutokea huko Sierra Leone.
Kwa hivyo, huwa kuna namna ambayo tunapata ku process habari na kuziota, halafu, zikitimia, tunaweza kujiona tumetabiri kikichotokea kwa ndoto zetu.