Wakuu namimi naweka maono niliyoyaona kupitia ndoto. Lakini kabla sijaelezea ngoja nitoe maoni yangu.
=>Sayansi ni zao la uumbaji alioufanya MUNGU. Sisi binadamu tukiwa kama sehemu ya uumbwaji pamoja na viumbe na materials nyingine, sisi binadamu tunasoma (study), tunachambua(analysis) materials na mifumo mbalimbali aidha ya kibiolojia kemia ama fizikia, tunachambua viambata vilivyohusika kuunda kitu na mwishowe tunausoma ni namna gani mfumo husika katika kiumbe husika unafanya kazi(mechanism) harafu tunatunza kumbukumbu kwa matumizi mbalimbali. Mfano mashine za vyombo vya moto zimeunda kwa kutumia applicability ya ile knowledge(maarifa) waliyoyapata katika/ kuiga muundo(anatomy) na utendajikazi wake(physiology).
Kwahiyo binadamu ni Co creator anavumbua na kuunda vitu/teknolojia mbalimbali kwa kutumia malighafi zilizoumbwa na MUNGU from the scratch(yaani ile smallest particle(matter)).
Na wanasayansi walio wengine wamefanikisha uvumbuzi wao kwa kuvuviwa/kupewa maono na MUNGU.
Kwa maana nyingine sayansi ni mkusanyiko wa baadhi wa fact/maarifa waliyofanikiwa kuyang'amua katika chunguzi/tafiti zao katika baadhi ya vitu kati ya vitu vingi sana vilivyoumbwa na MUNGU
VITU VILIVYOUMBWA NA MUNGU KATIKA ULIMWENGU WA MWILITUNAWEZA TUKAVIPANGILIA KAMA IFUATAVYO.
i) Vitu vinavyoonekana na tunaweza tukavitumia moja kwa moja(actual things). Mfano; maji.
ii) Vitu vimejificha ndani ya vinavyoonekana (potential) na ili vionekane vinahitaji mchakato fulani ufanyike. Mfano;
a) Umeme ulikuepo lakini umekuja kugundulika na kutumikia baadae sana.
b) Mbegu, kupitia mbegu moja kama ni ya ngano unaweza ukailisha dunia nzima kama ni ya miti basi unaweza ukapata msitu kama wa amazon.
iii) Vitu ambavyo havionekani ila vina ishi kama (vina-exist actual na potential way). Mfano; hewa/gas mbalimbali kama oksijeni nitrogen.
Kwahiyo wanasayansi wanachokifanya ni
documentation ya kile walichoambulia kutoka katika uumbaji wa MUNGU kwani ni wazi hawawezi kuunda hata state mojawapo ya matter kati ya solid liquid na gas ni MUNGU pekee ndio aliezileta kwenye uwepo kotoka kwenye kutokuwepo,
Hawa wanasayansi inatakiwa watueleze kinagaubaga kua zile matter zilizobanguka katika nadharia ya Big bang zilitoka wapi kama wanapiga uwepo wa MUNGU.
Sayansi na wanasayansi naweza nikawafananisha na mtu ambaye anaokota pesa ndani ya nyumba ya mtu na ana-claim kwamba ni ya kwake.
Ama wale wazee waliogundua mlima kilimanjaro au ziwa victoria unagundua vipi kitu kilikuepo Miak mingi tu.(anyway najua mantiki yao)
😀😀😀Japo nawa-apprentice kwa mchango wao mpaka tuna-interact kama hivi.
Wakuu mmegusia masuala ya ndoto na Mtaalam @Kiranga katolea uchambuzi wa kisayansi Kuhusu experience yake katika ndoto, subconscious mind & clairvoyance mchango wenu nzuri sana na_ appreciate👍.