Jifunze kuendesha (ku-control) nafsi ili kujikomboa katika vifungo na kuwa msaada kwa wengine

Jifunze kuendesha (ku-control) nafsi ili kujikomboa katika vifungo na kuwa msaada kwa wengine

Kuna watu wamevuruga kabisa uzi na kupoteza uelekeo
Asijali kabisa yanayoendelea, afocus tu kwenye kumalizia mada yake tu, nafsi ya mtu mmoja tu ikifunguliwa ni faida kubwa sana, na hasara kubwa sana upande mwingine, na ndiyo hii vita hapa inatokea.
 
Nimefuatilia mjadala na ukweli sijachukia wala kukwazika kwa kuwa jukwaa hili ni huru na ni haki ya kila mtu kutoa mchango wake na hoja zake kwa uhuru bila bughudha. Na somo bado litaendelea kama kawaida ni muda tu unanibana sana kwa kuwa na majukumu mengi mno ya kufanya. Nilishindwa kushiriki katika mjadala uliokuwa unaendelea hapa,sababu;Ukifuatilia historia ya watu 100 walioonyesha hekima ya juu sana duniani na watu 100 walioonyesha upumbavu mkubwa sana duniani!,makundi haya mawili wote walikubaliana katika jambo moja tu la kuwa "Mungu yupo". Sasa kuuliza Mungu yupo au hayupo,si tu ni swali la kipumbavu bali huo ndiyo upumbavu wenyewe!. Jambo la pili la kutaka kumthibitisha Mungu kimwili (kisayansi),hapa Kiranga ameshinda kwa hoja kwa kuwa ni kweli kuwa Mungu ni "ROHO" na kamwe hauwezi kumthibitisha kisayansi na hata kiroho pia hujithibitisha mwenyewe kadri apendavyo na kwa muda apendao na kwa mtu ampendaye. Nikipata muda mzuri somo litaendelea kama kawaida na kama kuna watu wanataka kuendeleza mjadala hapa,waendelee tu maana hili ni jukwaa huru. Asanteni.
 
Kuna vitu mpaka sasa siwez kuviamini kama vipo...MUNGU NA SHETANI na sielewi nitumie mbinu gani ili niamin kimoja wapo kipo? mana nimesali sana makanisa kibao nimejitaid niwe na imani kweri kwer nilichokipenda huku utulivu wa nafsi huku ukitegemea baadae , kwa upande wa shetani nimeroga sana sijui njombe, sumbawanga, malawi, zambia, nijeri nimetoa mpaka kafara za damu.,, lakini sijaona uwepo wa hivi vitu majini sijui msukule nk baada ya kufanya hayo nikajigundua sikustaili kuwepo hapa dunian labda kuna sehemu yangu ya kuish mana sion tena umuhimu wa haya maisha yaan dunian nilikuja tafuta pesa, kujenga kuoa na kufa how? labda mtoa mada ungenieleza kiundan na kama kuna sehemu naweza ona majini hata ndondocha polepole nirudishe iman ila kwa sasa meng naona janja janja japo kuwa nina kipawa ndan yangu
uwepo wa majini nilisha yashuhudia, sitamani hata kuyasikia wala kujihusisha nayo
 
Ndiyo hivyo nasema inawezekana kuna sehemu ulipata taarifa za msiba au mtu anayekaribia sana msiba uka zi register subconsciously, huku zi register consciously. Baadaye ukaenda kuota. Ndoto huwa hatuoti tu, zinatokana na mawazo.

Pia, inawezekana ni coincidence tu umeota msiba halafu ukapata habari za msiba. Ikitokea hivyo kama unaamini ndoto zinatabiri utaona huu utabiri.

Pia, huwa tunaota ndoto nyingi sana, tunazokumbuka ni chache tu, sasa mara nyingine inawezekana tunaota ndoto za msiba mara nyingi hatuzikumbuki, tukipata habari za msiba ndiyo tunakumbuka ndoto za msiba.

Kitu cha msingi ni kwamba, jinsi ubongo unavyofanya kazi, consciousness, mawazo, ndoto kuna mambo mengi sana bado hatujayaelewa vizuri, na kabla ya kukimbilia kusema tunaweza kutabiri mambo ya mbele kwa ndoto, na habari za "mambo ya kiroho" ambayo hayana ushahidi, inatupasa tufanye uchunguzi wa kisayansi wa kina kwanza.

Wazungu walikuja na elimu ya kutabiri kupatwa kwa jua na mwezi, down to the minute. Waafrika ambao hawakujua hiyo elimu walivyoona hivyo, wakaona huu uchawi, mtu atawezaje kutabiri kupatwa kwa jua?

Naam, kama una mawazo ya kusema uwezo wa kutabiri yajayo ni mambo ya kiroho, uchawi, clairvoyance, unaweza kukubali hivyo kirahisi tu.

But is that the case? No.

Leo tumeelewa sayansi ya kupatwa kwa jua na mwezi (eclipses), hatuhitaji kutaja uchawi wala mambo ya kiroho kuelezea hilo.

Kuna charts zinazoelezea kupatwa kwa jua kwa maelfu ya miaka in the future.

Follow the science. Haya mambo ya mumbo jumbo za roho ni maneno ya enzi za giza hayo tunatakiwa kuyapita kwenye ulimwengu huu wa sayansi.

Yani hata kama hatuna jibu, tunatakiwa tulitafute kisayansi, sio kuanza kupiga ramli kuhusu mambo ya kiroho hapa.
Niseme hongera kwa ukijuacho...
Ila upande wa pili nakupa Pole sana.
 
Kuna vitu mpaka sasa siwez kuviamini kama vipo...MUNGU NA SHETANI na sielewi nitumie mbinu gani ili niamin kimoja wapo kipo? mana nimesali sana makanisa kibao nimejitaid niwe na imani kweri kwer nilichokipenda huku utulivu wa nafsi huku ukitegemea baadae , kwa upande wa shetani nimeroga sana sijui njombe, sumbawanga, malawi, zambia, nijeri nimetoa mpaka kafara za damu.,, lakini sijaona uwepo wa hivi vitu majini sijui msukule nk baada ya kufanya hayo nikajigundua sikustaili kuwepo hapa dunian labda kuna sehemu yangu ya kuish mana sion tena umuhimu wa haya maisha yaan dunian nilikuja tafuta pesa, kujenga kuoa na kufa how? labda mtoa mada ungenieleza kiundan na kama kuna sehemu naweza ona majini hata ndondocha polepole nirudishe iman ila kwa sasa meng naona janja janja japo kuwa nina kipawa ndan yangu
Wewe ni tapeli tu. Na zaidi nenda katibiwe yawezekna una ugonjwa wa kurukwa na akili.
 
Mungu hawezi kujibu, kwa sababu hayupo.

Mungu ambaye hayupo atajibu vipi?

Ndiyo maana watu wanahangaika sana kumjibia.

Ukiona watu wanahangaika kumjibia Mungu, ujue huyo Mungu hayupo.

Vinginevyo angejibu mwenyewe kama ulivyosema.
Mungu yupo
1.alisema hakika tutakufa, na watu wanakufa tunaona. hili halina ubishi
2.nature pia inatangaza uwepo wa Mungu-hakuna kitu kinaweza kuwepo bila kuwepo mtengenezaji wake
kuna vitu tunaamini vipo ,mojawapo ni akili, tunaamini tunazo japo hatuzioni, we just believe kutokana na matokeo fulanifulani, the same kwa Mungu
 
Mkuu acha ubishi

Kusoma teolojia haikupi kibali kwamba unajua kila kitu

Neno Mungu au MUNGU linawakilisha Mungu mkuu muweza wa yote asiye na mwanzo wala mwisho

Neno mungu linawakilisha sisi binadamu (miungu)

Mambo ya kwamba ulisoma theology yaache kwanza pembeni
Mimi ni muamini,

Na nnapenda kusema kwamba.

Msomi akizungumza, msikilize. Maana hakuna fida yoyote ya kuukataa UKWELI.

Utafanya vyema kukubaliana naye masuala ya herufi. Halafu uje na majibu sasa
 
Mkuu umejibu Vyema kuwa Huna Uhakika..

Je Hii Unaijua Mkuu!..

Zaburi 82:6

"Mimi nimesema, Nyinyi ni miungu,
Na wana wa Aliye juu, nyote pia.


I have said, Ye are god; and all of you are children of the most High."

Na unakumbuka Pia Andiko hili Yesu aliwahi kulirudia walipomwambia kwanini anajiita mwana wa aliyejuu..

Yohana 10:30-35

[30]Mimi na Baba tu umoja.

[31]Basi Wayahudi wakaokota mawe tena ili wampige.

[32]Yesu akawajibu, Kazi njema nyingi nimewaonyesha, zitokazo kwa Baba; kwa ajili ya kazi ipi katika hizo mnanipiga kwa mawe?

[33]Wayahudi wakamjibu, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu.

[34]Yesu akawajibu, Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu?

[35]Ikiwa aliwaita miungu wale waliofata na kutii neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka);
Daktari eeeh.

Sisi ni miungu.

Tena kwa seli zetu za ndani ya miili yetu zinaishi zikijua sisi (watu) ndio MUNGU wazo. Na ndio kila kitu kwao.

Na kwa mizania ya seli na maisha yao, mtu wao ni MUNGU kweli.

Na hizo seli pia ni mungu au sehemu ya mungu kama zikiishi kwa TAKWA kuu la kuumbwa kwake na mwili (God's will) nazo ni mungu.

Na ribosomu na mitochondria zinajuaga seli husika ni Mungu wao, nazo ni sehemu ya Mungu yaaani ukikagusa kamoja n.......... aaah bhana tuishie hapa kwanza.


Wanaadamu wafuatao matakwa ya Mungu. Ni Mungu maana ukimgusa mmoja wao, umegusa sehemu ya Mungu kabisa. Sisi ni Mungu naaaam wana wa mungu Aliye juu
 
Niseme hongera kwa ukijuacho...
Ila upande wa pili nakupa Pole sana.
Hujataja upande wa pili gani, hujataja mapungufu yangu, weka vitu wazi au kaa kimya.

Hivi vi criticism vya nusunusu ni kama hujiamini kuja front tujadili hoja zako.
 
Wakuu namimi naweka maono niliyoyaona kupitia ndoto. Lakini kabla sijaelezea ngoja nitoe maoni yangu.

=>Sayansi ni zao la uumbaji alioufanya MUNGU. Sisi binadamu tukiwa kama sehemu ya uumbwaji pamoja na viumbe na materials nyingine, sisi binadamu tunasoma (study), tunachambua(analysis) materials na mifumo mbalimbali aidha ya kibiolojia kemia ama fizikia, tunachambua viambata vilivyohusika kuunda kitu na mwishowe tunausoma ni namna gani mfumo husika katika kiumbe husika unafanya kazi(mechanism) harafu tunatunza kumbukumbu kwa matumizi mbalimbali. Mfano mashine za vyombo vya moto zimeunda kwa kutumia applicability ya ile knowledge(maarifa) waliyoyapata katika/ kuiga muundo(anatomy) na utendajikazi wake(physiology).

Kwahiyo binadamu ni Co creator anavumbua na kuunda vitu/teknolojia mbalimbali kwa kutumia malighafi zilizoumbwa na MUNGU from the scratch(yaani ile smallest particle(matter)).

Na wanasayansi walio wengine wamefanikisha uvumbuzi wao kwa kuvuviwa/kupewa maono na MUNGU.

Kwa maana nyingine sayansi ni mkusanyiko wa baadhi wa fact/maarifa waliyofanikiwa kuyang'amua katika chunguzi/tafiti zao katika baadhi ya vitu kati ya vitu vingi sana vilivyoumbwa na MUNGU

VITU VILIVYOUMBWA NA MUNGU KATIKA ULIMWENGU WA MWILITUNAWEZA TUKAVIPANGILIA KAMA IFUATAVYO.

i) Vitu vinavyoonekana na tunaweza tukavitumia moja kwa moja(actual things). Mfano; maji.

ii) Vitu vimejificha ndani ya vinavyoonekana (potential) na ili vionekane vinahitaji mchakato fulani ufanyike. Mfano;
a) Umeme ulikuepo lakini umekuja kugundulika na kutumikia baadae sana.
b) Mbegu, kupitia mbegu moja kama ni ya ngano unaweza ukailisha dunia nzima kama ni ya miti basi unaweza ukapata msitu kama wa amazon.

iii) Vitu ambavyo havionekani ila vina ishi kama (vina-exist actual na potential way). Mfano; hewa/gas mbalimbali kama oksijeni nitrogen.

Kwahiyo wanasayansi wanachokifanya ni documentation ya kile walichoambulia kutoka katika uumbaji wa MUNGU kwani ni wazi hawawezi kuunda hata state mojawapo ya matter kati ya solid liquid na gas ni MUNGU pekee ndio aliezileta kwenye uwepo kotoka kwenye kutokuwepo,

Hawa wanasayansi inatakiwa watueleze kinagaubaga kua zile matter zilizobanguka katika nadharia ya Big bang zilitoka wapi kama wanapiga uwepo wa MUNGU.

Sayansi na wanasayansi naweza nikawafananisha na mtu ambaye anaokota pesa ndani ya nyumba ya mtu na ana-claim kwamba ni ya kwake.
Ama wale wazee waliogundua mlima kilimanjaro au ziwa victoria unagundua vipi kitu kilikuepo Miak mingi tu.(anyway najua mantiki yao)

😀😀😀Japo nawa-apprentice kwa mchango wao mpaka tuna-interact kama hivi.
Wakuu mmegusia masuala ya ndoto na Mtaalam @Kiranga katolea uchambuzi wa kisayansi Kuhusu experience yake katika ndoto, subconscious mind & clairvoyance mchango wenu nzuri sana na_ appreciate👍.
 
Ilikuwa mwaka jana mwezi wa nane 8/2023. Tarehe nimesahau ila ilikua katikati ya mwezi wa 8.

1:Usiku mmoja niliota ndoto. Moja yenye mfulurizo wa mmatukio yasiyofanana. Ndoto ilikuwa hivi;

a). Nilikuwa napita njia kijiji hadi kijiji, njia zile za vjijini ilikua pori kwa pori maeneo niliyopita haykua msititu. mnene bali ni miti ya kimo cha kati ya hapa na pale(scattered) ikiambatana na vichaka na nyasi.

Nikafika sehemu ni kama pamezoeleka kuwa na maji huwa yanappita ila kwa wakati ule ni kama ule mto umekauka pamebaki mkondo wa mto usio na maji mchanga miamba na ufo go wa ule mto ndio vinaonekana. Mimi nikiwa sehemu ya chini uku ya mkondo wa mto nikitizama juu ulikotokea mto.


Niligaiiri kutumia njia ya poli kwa poli nikarudi juu kule nikachukua njia kuu yanayoweza kupita hata magari gafra nikajikuta nipo na mtu mwingine akiwa anaendessha bodabda mimi Nyuma kama abilia wake tuliendelelea na safari mbele tukakutana na checkpoint bala bala ikiwa imezuiwa na kamba na ilionekana ni kama sio rasmi na ipo kwa muda tu, na wakaguzi wawili vijana walionekana kama hawako pale kihali na kwa muonekano wao ni kama wana agenda za siri (wakutiliwa mashaka) yaani kama walikua wanapiga surveillance kila kitu kinachpita njia ile tukapewa maelekezo na wale vijana kua tusipite ile njia moja ka moja bali tuzunguke tukaondoka.

b). Nikajikuta nipo mahali pengine kabisa nikawakuta watu w anapanga mipango huku wakiwa na pilika pilika nyingi na wako bize (very serious) kwa mazingira yale ni wazi yaliakisi kuwa ni kambi ya jeshi, mgambo, waasi ama magaidi maana hawakua na safe yoyote.
Mazingira ya kijijini yasiyokua na miundombinu bora. Njia za polini bala bala ni vumbi tupu.

Nikajikuta tena nipo njiani kuelekea eneo/ kijiji kingine huko pia nikakuta kundi la Wanajeshi wakipanga mikakati wengine walionekana wakitoka kwenye vikao na kwa usiriazi ule ni kama kulikua na jambo nyeti na ladharura lilikua linajadiliwa. Ilikua mida ya jioni jua la usoni linalokaribia kuzama wale Wanajeshi walionekana wanalijea mahali pao pa kupumzika /kambini.

Nikaendelea na safari nikakutana na wanaume kadhaa nje kidogo na makazi ya watu walikua na harakati za kawaida tu, Sasa katika ile njia ya polini nikiwa nimesonga mbele kidogo huku wale wanaume nimewaacha. Hatua chache Nyuma, nikaona mti/kichaka kimo cha kuifikia urefu wa mtu Mzim kile kichaka kilikua kimestawi kuliko miti mwingine pale kikiwa na matawi huku na huku kama nanga katika mawazo yangu nilitaka nikate lile tawi nikatengeneze kifaa kama mwiko wa kupikia mboga aina ya mrenda, kile kifaa kinafanana kama nanga kwa chini kinatumika kuchanganyia mrenda wakati wa kupikia (unapekecha) nikagaili kukata nikapitiliza kufika mbele giza likiwa linaingia nikakutana na wanajeshi tena walikuwa watatu wakiw mbalimbali hawajakaribiana, wakiwa wanatokea polini ni kama walikua wametoka mbali kidogo na giza limewakutia wakiwa njiani wanarudi kambini na walionekana wametoka kwenye kikao kilichofanyika msituni.
Nikakumbuka ule mti nakarudi ili nikate lile tawi nikakuta wale wazee niliokua nimewaacha Nyuma wameshakata ndio wanaondoka nacho.


c). Nikajikuta sehemu nyingine kabisa huku niliona wingu zito(nene) angani lile wingu lilikua na vimulimuli vya radi vikimulika bila kutoa muungurumo kutokea ndani ya wingu huku likionyesha muda wowote mvua kubwa itanyesha.

d). Nikajikuta tena sehemu Nyingine niko juu ya ngema chini kuna njia kuu (highway) nikatazama chini ya ile ngema nikaona balabala haina magari isipokua kuna kifaru cha jeshi kikiwa na askari wawili mmoja yupo ndani mwingine yupo juu ya kifaru kile huku ule mtutu wa kifaru ukiwa uanaangaza huku na huku(haujatulia) kana kwamba aliyekua anaongoza alikua anawasiwasi sana asijue alenge wapi. , wale askari walikua wamevaa gwanda zilizofanana na rangi ya kifaru ulikua ni kaki inayoelekea kwenye ukijani flani hivi.
Mwisho wa ndoto.

Kuna baadhi ya mazingira sikuyaelewa kabisa kwenye hii ndoto ila baada ya kutimia moja baada ya jingine ndio ufahamu ukaanza kufunguka.

Note: Wz spfc 2ew.
 
Tukio moja wapo ni yale mafuriko ya hanang katesh manyara.

Nilipata Habari nikaangalia na video na picha kazaa zikionesha balabala mitaro nyumba zilivyosombwa na kufukiwa na tope lile, sikuzinduka nikahuzunika tu. lakini baadae nikakutana na picha zingine zikionesha mafuriko yalivyoasili zile picha nivyoziona mazingira yake yalikuwa yaleyale niliyoyaona ndotoni yaani ni vilevile ndio ufahamu ukanijia kua inamaana yale mazingira ndotoni yalikusudia tukio hili.

Hikindio nilikiona ndotoni na tokea nizaliwe sijawahi kufika manyara.
_20240313_145454.JPG
_20240313_145719.JPG
_20240313_145638.JPG

a). Nilikuwa napita njia kijiji hadi kijiji, njia zile za vjijini ilikua pori kwa pori maeneo niliyopita haykua msititu. mnene bali ni miti ya kimo cha kati ya hapa na pale(scattered) ikiambatana na vichaka na nyasi.

Nikafika sehemu ni kama pamezoeleka kuwa na maji huwa yanappita ila kwa wakati ule ni kama ule mto umekauka pamebaki mkondo wa mto usio na maji mchanga miamba na ufo go wa ule mto ndio vinaonekana. Mimi nikiwa sehemu ya chini uku ya mkondo wa mto nikitizama juu ulikotokea mto.


Niligaiiri kutumia njia ya poli kwa poli nikarudi juu kule nikachukua njia kuu yanayoweza kupita hata magari gafra nikajikuta nipo na mtu mwingine akiwa anaendessha bodabda mimi Nyuma kama abilia wake tuliendelelea na safari mbele tukakutana na checkpoint bala bala ikiwa imezuiwa na kamba na ilionekana ni kama sio rasmi na ipo kwa muda tu, na wakaguzi wawili vijana walionekana kama hawako pale kihali na kwa muonekano wao ni kama wana agenda za siri (wakutiliwa mashaka) yaani kama walikua wanapiga surveillance kila kitu kinachpita njia ile tukapewa maelekezo na wale vijana kua tusipite ile njia moja ka moja bali tuzunguke tukaondoka.
 
Tukio jingine baadae kabisa nikiwa maeneo nilopokua natafutia riziki pale fire Morogoro baada ya kufanya usafi wa ofisi mida ya asubuhi sina hili wala lile naona POLISI wanaandamana huku wakiimba nyimbo(chenja) huku wakiwa wameongozana na magari yenye silaha nzito gari moja lilikua kubwa hivi lina mtutu mzito mbele kwa juu, Sasa ule mtutu ndio ulionikumbusha kua mbona hiki kitu nilikiona, tofauti ni kwamba kwenye yale maandamano walikua askari wengi sana wakiwa na gwanda rangi sawa na nilichokiota ila lile gari lilikua la dark blue kama sio nyeusi na mtutu ulikua umetulia tu, tofauti na huku kwenye ndoto ambayo niliona askari wawili tu wakiwa na gwanda zilizofanana na kifaru huku mtutu wa kifaru ukiwa inageuka hukunahuku. Hili tukio sikumbuki ilikua lini.

Sasa tarehe 7 mwezi wa 10 nikasikia Hamasi wamevamia Israel wameua watu na kuteka wengine. kwasababu jeshi la Israel nazijua rangi za nguo zao na vifaru vyao haikuhitaji kuangalia picha wala video zao nikajua tu kumbe ile sehemu ya ndoto ililenga operation ya Israel kule Gaza baada ya kushambuliwa na hamasi.

Sasa Wasiwasi wangu ukaniondoa kwenye msingi wa ile sehemu ya ndoto iliyohusu wingu zito na nene, kutokana mapambano ya Israel na hamasi kupamba moto nikahisi labda lile wingu sio wingu bali ni mripuko mkubwa wa bomu nzito litakalo sababisha moshi na moto kutanda angani (kwamba Israel inaweza kupigwa na bomu la nyuklia na mahasimu wake(Iran) watakapo ivamia Gaza au Israel itatumia bom hilo kwa watakaoingilia).

Ila Sasa naona msingi wa ile ndoto ilikua ni mvua kubwa zilizosababisha maafa na pengine zikaendelea na masika hii.
d). Nikajikuta tena sehemu Nyingine niko juu ya ngema chini kuna njia kuu (highway) nikatazama chini ya ile ngema nikaona balabala haina magari isipokua kuna kifaru cha jeshi kikiwa na askari wawili mmoja yupo ndani mwingine yupo juu ya kifaru kile huku ule mtutu wa kifaru ukiwa uanaangaza huku na huku(haujatulia) kana kwamba aliyekua anaongoza alikua anawasiwasi sana asijue alenge wapi. , wale askari walikua wamevaa gwanda zilizofanana na rangi ya kifaru ulikua ni kaki inayoelekea kwenye ukijani flani hivi.
Mwisho wa ndoto.
_20240313_153437.JPG

Sasa rangi ya hiki kifaru ifanane na hizo sare walizovaa.
 
“JE ? KAMA MUNGU WETU MKWELI ANAIJUA KESHO YAKO/YETU, YANI ALIJUA WEWE UTAFANYA HAYO YOTE ULIOFANYA KABLA ATA HUJAANZA KUFANYA, KWANINI ATAKUCHOMA MOTO/ KWANINI ATAKUANGAMIZA”

Kiranga Tafadhali mkuu pita huku kidogo wasaidie ndugu zetu
Free will au choice ndio itakayokuangamiza. Chagua chama ili uishi ila ukichagua mabaya au mauti utakufa tuu
 
Biblia haijasema binadamu ni Mungu

Biblia imesema binadamu ni mfano wa Mungu

Pia utatakiwa ufahamu neno Mungu au MUNGU lina maana tofauti na neno mungu.
Kuelezea kuhusu Mungu ilhali haujui kitu ni kukosea sana..unaikosea nafsi yako na pia unawakosea wenye ulimwengu wa roho, unamkosea hadi creator ambaye haumjui ni nani.

Hakuna mwanadamu Anayejua mambo ya sayansi ya Ulimwengu wa roho..na namna inavyofsnya kazi, imetoka wapi, inaendajeendaje...zaidi ya yote utapata readers tuu na wale wanao uelewa wa kuendana na flow yake. Nothing more.

Na hii ni kwa sababu vazi lako haliwezi kuhimili hayo yote, na mengine hayachakatwi na akili yako kamwe.

Ni sawa na kusema una ufahamu wa vichachevichache tuu..mpaka ukishakuwa immortal ndio utajua namaanisha nini.

Vitu vya kiroho vingine vinaopareti kirohoroho...ambapo akili haina haja ya kufanya kazi

AU

akili inafanyishwa kazi kwa dimensions zingine tofauti na hizi za 3D+TIME. Hapa hautopata majibu ya kutosha kuhusu Mungu, nguvu zake na uwezo alionao, nguvu za mwanadamu na mengineyo, mpaka uweze kujua namna ya ku accces higher dimensions.

Dini zinasaidia angalau kwa urahisi kukujuzs mambo haya ya higher dimensions ila kwa uangalizi maalum na mfumo unaoendana na imani husika

Sasa busara ni kujifunza kwanza, ukaelewa, kisha baadae ndio ujue nini cha kufanya..ila mtu ukiendelea kubwabwaja..unajikosea sana hata wewe mwenyewe

Asanteni
 
Back
Top Bottom