Zee Real
Member
- May 2, 2021
- 50
- 54
Karibu Kwa muendelezo.UTANGULIZI SEHEMU B;MAANA YA NAFSI. Leo tunaendelea na somo baada ya upepo kutulia na wote kuishia mitini. Nafsi ni mtu halisi na ana vitu vyote vya mtu wa nje. Mtu wa nje (mwili) ni kama kivuli cha mtu wa ndani (nafsi). Vitu vikuu vinavyofanya nafsi ifanye kazi vizuri ni, Akili ambayo inabeba milango yote ya fahamu, utambuzi, fikra, maarifa; Hisia ambayo inabeba furaha, upendo, huzuni na chuki. Nafsi inaweza kuingia katika mwili wowote hata wa mnyama bila shida. Ukiona mchawi anajigeuza paka au nyoka tambua ni nafsi yake ameivalisha kwenye mwili huo. Mtoto anaweza kurithi vitu vilivyopo kwenye nafsi ya mama yake na baba yake ila roho anarithi kwa baba tu. Kazi ya roho ni kuitia nguvu nafsi ili ifanye kazi yake halisi iliyoumbiwa. Roho haiwezi kufanya kazi na nafsi iliyovurugwa maana nafsi iliwekwa iende automatic katika kazi yake. Kipawa 'nyota' cha mtu kimewekwa ndani ya nafsi na siyo rahisi akijue mpaka afuate hatua muhimu. Huwezi kuiba kipawa cha mtu maana hata shetani mwenyewe hakijui, bali ni nafsi tu ya mtu inavurugwa na kuipotezea mwelekeo na kutumikishwa kwa faida ya mtu mwingine. Nafsi inaweza kufungwa kwenye mti, inaweza kuwekwa ndani ya chupa, inaweza kufungwa chini ya bahari inaweza kufungwa ofisini au kwenye nyumba za ibada na sehemu yoyote ile kulingana na matakwa ya mfungaji na kuitumikisha kadri apendavyo. Njia rahisi sana ya kujua nafsi yako imefungiwa wapi ni kwa kupitia ndoto. Angalia unaota sana upo maeneo gani na unafanya nini. Ili unase na kuendesha nafsi ya mtu/watu kadri upendavyo inategemea sana na nguvu (roho) inayoipa nafsi hiyo nguvu. Lazima uwe na roho yenye nguvu zaidi. Na kuna vitu ambavyo nimeviorodhesha hapo juu ambavyo hutumika kukamata na kuendesha nafsi na tutavijadili mbeleni. Sasa embu jiulize kidogo itakuaje endapo unataka kufungua biashara yoyote au kuingia katika uongozi au siasa au huduma za kiroho na hauwezi kuvuta nafsi za watu!, ukweli ni kuwa hauwezi kupata watu wowote maana kunawenzako wanatumia sala au dua au uchawi kuvuta watu (nafsi). Fikiria kwenye kuoa uwe msichana au mvulana na unapendwa na wengi, kila mtu atakuvuta kwa njia yake na mwisho mwenye nguvu atashinda. Watu wengi wanachanganyikiwa kwa nafsi zao kuvutwa na watu na mwisho wanabaki katikati na kushindwa kujua waelekee wapi. Ni kama kuchukua sumaku mbili na kuweka chuma katikati na kuivuta huku na huku, chuma itacheza tu hapo katikati hadi ipate sumaku yenye nguvu zaidi. Mwisho, Nafsi haitakiwi kurudi nyuma bali inatakiwa kwenda mbele tu, ikirudi nyuma mtu atakuwa nyuma ya muda na siku zote mtu anatakiwa awe mbele ya muda ili atayarishe mazingira ya mbeleni. Na hapa ndipo wazungu wanapotushinda tu kwa kuwa mbele ya muda. Ukikomboa nafsi yako, umekomboa maisha yako na utaishi kwa uhuru wote na kwa mafanikio ya uhakika.