Ghost MVP
JF-Expert Member
- May 19, 2022
- 439
- 736
Siku hizi kumekuwa na utapeli mkubwa sana kwa njia ya mtandao, leo nitaelezea njia ya biashara na namna unavyoweza tapeliwa.
Biashara ni nyingi sana mtandaoni kama biashara ya nguo, viatu, simu, laptop na nyingine nyingi. Wapo wafanyabiashara ambao siyo matapeli na wapo matapeli.
Namna ya kujua mfanyabiashara ni tapeli fuata njia hizi:
Ukijaribu kumtafuta kwa namba tofauti anaweza kukupa maelezo tofauti kabisaa, na hawaweki location ya link kwenye account zao, ili usiweze jua wapo wapi.
Hivyo unapotaka nunua kitu mtandaoni usikubali kutuma pesa kwanza hata iweje, mwambie akuletee mzigo umpe pesa yake, kwasababu unaweza tapeliwa au kuletewa bidhaa feki/isiyo na kiwango.
Kwenye picha ni mmoja wa watu hao ambapo amejichanganya na kusema yupo sehemu tofauti kwasababu alijua ni mteja mwingine.
Weka comment majina ya wafanya biashara matapeli, user name zao za mitandaoni na useme walikufanyaje ukajua ni tapeli ili waweze komeshwa.

- Wengi wao huwa wanatumia bei ambayo itakushawishi kununua, ambayo ni rahisi kulinganisha na bei halisi.
- Baadhi husema wapo Zanzibar wakijua mteja lazima atakuwa Bara na huwezi kwenda dukani kwao.
- Ni wepesi sana kukushushushia bei ila ni wazito kukuelekeza mahala sahihi wanapopatikana.
- Namba zao huwa za WhatsApp tu, hawapatikani kwa kuwapigia kwasababu wanaepuka ku-trackiwa.
- Picha za ushahidi wa kutuma mzigo huwa hazioneshi sura zao wala picha ya duka vizuri, wala jina la duka, na picha huwa za mikono tofauti.
- Wanataka uwatumie pesa ndiyo wakutumie mzigo, au ulipie nusu ndiyo upokee mzigo wako, na ukituma tu umekwisha.
- Namba ya kutuma pesa huwa ni tofauti na anayotumia WhatsApp.
- Huwa wanakuuliza mahala unapopatikana ili waweze kukutajia mbali ambapo huwezi kwenda.