Kwa nini hatuanzi, na tukitaka kuanza tunaghairi? Moja ni ‘laana’ ya kuwa na uwezo. Unajua unaweza, ukitulia siku moja tu kazi ya mwezi mzima utaifanya ndani ya siku mbili na hakuna tatizo. Kwa nini uanze mapema kama unaweza kuanza siku moja kabla? Unaahirisha upumzike kwanza.
Pili, imani kuwa muda unao. Haya nayo ni marupurupu ya ‘laana’ ya uwezo. Uwezo unakufanya uamini muda upo. Ukishaamini una muda na utafanya vizuri huwezi kuona sababu ya kuanza. Wakati wenzio wanaojijua hawana uwezo wana hofu ya kuharibu na hawaamini wana huo muda wa kujiandaa, wewe mwenye uwezo hiyo hofu huna. Unajua kazi inayohitajika kesho utaianza leo usiku na itakamilika kwa viwango ambavyo mwenzio asiye na uwezo ametumia wiki mbili kuhangaika nayo.
Ukifanikiwa kupata matokeo uliyotarajia, akili inaanza kukuaminisha kuwa uvivu sio tatizo. Kwamba unaweza kupoteza muda, ukaanza kwa kuchelewa na bado utafanikisha jambo lako. Shida ni kwamba wenzio wasiojiamini sana, wasio na uwezo kama wewe, wanaanza mapema na hivyo wanapata muda wa kutosha kujifunza mambo mapya na kuyaelewa kwa kina. Ingawa ni kweli bado unaona unapata matokeo, baada ya muda kidogo utabaki kuwa wa kawaida. Uwezo wako utaanza kuacha kukulipa.
Lakini pia, muda kwa hakika haupo kama unavyodhani. Kesho haitabiriki na huenda isikupe nafasi ya kufanya kitu kwa dharura kama ulivyozoea. Ulichozoea kinakupa matokeo kinaweza kukubabishia aibu kubwa usiyoitarajia na uwezo wako usikusaidie. Ukipata aibu inayokutosha, ukadhalilika, ukapotea heshima kwa kosa la kutokufikia makataa, hutahitaji ushauri wa ‘mbinu za kutokuahirisha mambo.’ Maumivu ya uvivu yatakufundisha kufanya maamuzi ya kuanza na kuanza kwa wakati.