Jifunze kumpa mwanamke wako hela bila sababu, utanishukuru baadaye

Jifunze kumpa mwanamke wako hela bila sababu, utanishukuru baadaye

😆😆😆 kuna watu mnajidanganya.
Mwanamke hata umuonge dunia, sio kwamba ndio atatulia. Mwanamke huwa hathamini fadhila, yeye huthamini tu hisia zake, jinsi hisia zake zitakapomtuma ndio hufanya.
Mwanaume, ukitaka uje uishi kwa majuto hapa duniani, basi wekeza pesa zako, nguvu zako, akili yako kwa wanawake, ututajuta.
Hii imeenda! 👏👏👏
 
Ukishamtumia hiyo hela anaenda kumgawia mpenzi wa moyo wake. Enzi nikiwa mpumbavu sana nilishawahi kumpeleka shopping ya nguo mwanamke niliyempenda ila jioni yake akazivaa zile nguo na kutoka na mpenzi wa moyo wake. Niliumia sana. Bahati nzuri KARMA huwa inasahau address ya CCM tu... huyo manzi kwa sasa ni single mama mwandamizi.
 
Kindly refer to the heading above..


Na hii sio mwanamke wako tu, hata yule ambaye unamtaka. Kwa mfano; [emoji116]

Money transfer successful! TSH 200,000.00 was sent to NMB Bank account no 41510040XXX (MILLICENT MZURI) ref:XXX4298373. Thanks for using Exim Mobile, call 0800 780 111 for any assistance needed.

Au,

AirtelMoney
Umetuma Tsh270,000.00 kwenda kwa MILLICENT MZURI. Salio lako jipya ni Tsh2,100,000.00. Muamala No: CI240503.1856.N57337

Hiyo miamala yote uwe umemtumia hata bila kuombwa. Kwa mfano huo muamala wa kwanza unakuwa umeutuma jana usiku wa saa saba wakati amelala, akiamka asubuhi anakutana na notification tu. Aisee, mapenzi utayasimulia katika muktadha wa tofauti sana.

Pengine huo muamala wa pili uwe umemtumia leo week end baada ya binti kukwambia anaenda kwenye birthday ya rafiki yake. Halafu muamala unafuatiwa na SMS hii, "baby pls manage that little token from me. Love always" [emoji4] .

Hawa wanawake tunawalaumu bure tu. Tatizo ni kwamba hatuwapi PESA. Kwao pesa ndio kila kitu; nguvu za kiume, uaminifu, utulivu, upole, utu wema, usikivu, unyenyekevu n.k (mengine ongezea mwenyewe).

Sasa wewe hela hutumi, binti anajikaza anakuomba unaanza stori, sijui "ooh bay nipo mbali msibani huku tandahimba ndanindani nina cash tu na mawakala wako mbali" [emoji23], wakati siku hizi kuna sim banking, mobile money transfer n.k

Hata kama huna sim banking, mwanaume unakosaje akiba kidogo kwenye simu kwa ajili ya dharura?!!! Kwanza siku hizi kutembea na cash ni ushamba.

Wanaume tutafuteni pesa. Dunia haina huruma kwa masikini wote lakini hasa sisi WANAUME.

N:B
'MILLICENT MZURI' NI JINA LA KUSADIKIKA TU.
Hujawajua Wanawake, kadri unavyokua utaelewa.,.!

Nini laki 3 na maneno matamu...!

Mnunulie Mwanamke Mwezi uwe Mali yake, mpeleke Paris, Norway kila week, mpelekee Moto mpaka huko chini kuwe kunatoa Moshi..

Lakini Mwanamke wako ama Mke wako anaweza kukubebea Mimba ya Muuza Genge.
 
Unatudanganya mkuu.

Hapa unatafuta likes za wanawake tu na utafanikiwa kuwadanganya ila sio sisi watu wazima na midevu yetu.
Watu wenye midevu like zenu za nini au na nyi mnataka mpewe hela mgongwe
 
Back
Top Bottom