Jifunze kumuacha aende

Jifunze kumuacha aende

Na ukiniacha nikikubaliana na hali halisi ujue ndo hatuongei tena. Sasa jichanganye unisalimie...
wewe mtu umenifanya nicheke hapa barabarani naonekana chizi
 
So painful... Dah!!! Ushampenda mtu? Dah ngumu saäana kumuachia aende....
 
hahaha haya maswali mengine ni chonganishi ok yeye ndiye aliyeniacha akaenda
Kama alikuacha uende nawe mwache aende

Thamani yako ataiona msamehe tu ishi maisha yako

Habari za ex wako tuishie hapa, kila mtu ni ex wa mtu, na huwez kua unaendelea kusoma kurasa mpya kila siku ukiwa bado unarudi kusoma za zamani hata nusu kitabu hautafika
 
Kama alikuacha uende nawe mwache aende

Thamani yako ataiona msamehe tu ishi maisha yako

Habari za ex wako tuishie hapa, kila mtu ni ex wa mtu, na huwez kua unaendelea kusoma kurasa mpya kila siku ukiwa bado unarudi kusoma za zamani hata nusu kitabu hautafika
najua unajua nipo katika maisha yangu,
 
JIFUNZE KUMUACHA AENDE

• Kamwe usihisi kama ulimwengu ndio unakaribia mwisho pale akupendae anapokuacha.

MUACHE AENDE !

• Kujaribu kumlazimisha mtu akupende ni sawa na kujaribu kumlazimisha Nguruwe kutambua usafi na uzuri. Usimlazimishe akupende, mwache mwenyewe akupende, kama hakupendi...

MWACHE AENDE !

• Wewe ni wa thamani mno kulilia penzi. Mtu ambae anakupenda kweli atakuheshimu na hataku 'treat' kama uchafu. Kama atakuchukulia wewe kama uchafu...

MUACHE AENDE !

• Usipoteze muda wako wa thamani kujaribu kumshawishi au kuomba mapenzi. Mtu mwingine pembeni anakupenda wewe kwa dhati, ila wewe uko busy mno kumuogesha nguruwe! Kwanini?

MUACHE AENDE !

• Usikasirike pale mtu wako anapompenda mwingine tofauti na wewe. Siku zote hua ni vigumu kumshawishi NYANI kwamba Asali ni tamu kuliko ndizi...

MUACHE AENDE !

• Mwanamke/mwanaume yeyote anaekuchukulia kirahisi siku zote atachukulia faida kwako, atakugeuza atakavyo kama chapati akijua hufurukuti, yeye sio Mungu wa kukufanya atakavyo...

MUACHE AENDE !

• Kuna watu hawatakupenda hata kama utajitoa kiasi gani kwao. Ni sawa tu. Kukukataa kwao haimaanishi kwamba una kitu kibaya, bali ni maana kwamba hawako kwa ajili yako. Usilazimishe duara kuwa pembe tatu...

MUACHE AENDE !

CHA KUJIFUNZA

• Hauwezi badilisha maoni mabaya ya watu juu yako, ila unaweza ukazuia maoni yao mabaya yasikubadilishe wewe kama wewe!

• Acha kichwa chako kiongoze moyo wako kukuondoa katika mahusiano sumu. Lengo la mahusiano sio kuleta mafadhaiko ila ni kuongeza furaha juu ya ile uliyokuwa nayo mwanzoni ulipokuwa haupo ktk mahusiano.

NI NGUMU SANA ILA KWA MUSTAKABALI WA FURAHA YAKO YA SASA NA YA BAADAE ME NAKWAMBIA MUACHE AENDE MPE NA NAULI KABISA!

Kama ipo ipo tu...!

Tupo pamoja??

Share
 
Back
Top Bottom