Jifunze kumuacha aende

Jifunze kumuacha aende

It's a good advice ngoja niufate maana wakati nnaopitia Mungu ndo anayejua[emoji30] [emoji30] Ila tatizo kamoyo nako hakataki kukubali kumuacha aende dah,ntajitahidii
Daah. we are on the same boat aisee. Sijui hata nifanyeje ila acha tu nianze moja ingawa naona nazidi kupoteza muda tu na kuwachelewesha watoto shule
 
Hahahaaa. Ngumu hiyo jirani unaeza pasha kiporo ukashindwa kumpiga na chini.

We waeza jirani?
Sasa ukishindwa kumpiga chini maana yake unampenda. Unashikilia hapo hapo.

Jiran kwann unamoyo mgumu saana
 
JIFUNZE KUMUACHA AENDE

• Kamwe usihisi kama ulimwengu ndio unakaribia mwisho pale akupendae anapokuacha.

MUACHE AENDE !

• Kujaribu kumlazimisha mtu akupende ni sawa na kujaribu kumlazimisha Nguruwe kutambua usafi na uzuri. Usimlazimishe akupende, mwache mwenyewe akupende, kama hakupendi...

MWACHE AENDE !

• Wewe ni wa thamani mno kulilia penzi. Mtu ambae anakupenda kweli atakuheshimu na hataku 'treat' kama uchafu. Kama atakuchukulia wewe kama uchafu...

MUACHE AENDE !

• Usipoteze muda wako wa thamani kujaribu kumshawishi au kuomba mapenzi. Mtu mwingine pembeni anakupenda wewe kwa dhati, ila wewe uko busy mno kumuogesha nguruwe! Kwanini?

MUACHE AENDE !

• Usikasirike pale mtu wako anapompenda mwingine tofauti na wewe. Siku zote hua ni vigumu kumshawishi NYANI kwamba Asali ni tamu kuliko ndizi...

MUACHE AENDE !

• Mwanamke/mwanaume yeyote anaekuchukulia kirahisi siku zote atachukulia faida kwako, atakugeuza atakavyo kama chapati akijua hufurukuti, yeye sio Mungu wa kukufanya atakavyo...

MUACHE AENDE !

• Kuna watu hawatakupenda hata kama utajitoa kiasi gani kwao. Ni sawa tu. Kukukataa kwao haimaanishi kwamba una kitu kibaya, bali ni maana kwamba hawako kwa ajili yako. Usilazimishe duara kuwa pembe tatu...

MUACHE AENDE !

CHA KUJIFUNZA

• Hauwezi badilisha maoni mabaya ya watu juu yako, ila unaweza ukazuia maoni yao mabaya yasikubadilishe wewe kama wewe!

• Acha kichwa chako kiongoze moyo wako kukuondoa katika mahusiano sumu. Lengo la mahusiano sio kuleta mafadhaiko ila ni kuongeza furaha juu ya ile uliyokuwa nayo mwanzoni ulipokuwa haupo ktk mahusiano.

NI NGUMU SANA ILA KWA MUSTAKABALI WA FURAHA YAKO YA SASA NA YA BAADAE ME NAKWAMBIA MUACHE AENDE MPE NA NAULI KABISA!

Kama ipo ipo tu...!

Tupo pamoja??

Share
UTADHANI UMENIANDIKIA MIMI,NIMEPATA FARAJA GHAFLA !!!
Bravo!!!!
 
Alisamehe mdomoni ila kashindwa kulitoa rohoni, heri muishie hapo maana huyo haupo tena moyoni mwake.
Kweli mis powers shida ipo kwangu tu kumtoa rohoni na mawazoni ye binafsi ananitumia sms anawake na anampend sana, mwanzo alinambia ivo ivo ila mwisho akanambia haikua kweli ndo akanisamehe,saiv karudia tena so nakosa decision, nimepanga mwakani niandae posa ikiwa rejected basi
 
Daah. we are on the same boat aisee. Sijui hata nifanyeje ila acha tu nianze moja ingawa naona nazidi kupoteza muda tu na kuwachelewesha watoto shule
[emoji30] [emoji30] ,polee ila bora kuanza upya kuliko kumpenda mtu asokupenda, inaumiza ila ndyo hivo, Mimi kuna kamtu nakapenda ila kenyewe hakapendi hata ukucha wangu[emoji3] [emoji3] ,yaani unajua mtu hakupendi mpk unafahamu kabisa aisee
 
Ni kweli katika mapenzi muda mwingine unajikuta mtu wa stress na mawazo na kumuacha inakua ngumu nisaidien nifanye nin....hiyo msichana kila Mara yupo bize na kuchat na mtu mwingine na sometimes ananitoroka sijui nifanyaje...nimeishi nae miaka mitatu ya upenz
 
Back
Top Bottom