Jifunze kutokuamini watu ili uepuke kuumizwa

Jifunze kutokuamini watu ili uepuke kuumizwa

Ndugu wana jamvi hbr ya leo.

Naandika kwa msisitizo kuwa jitahidi sana sana upunguze kuamini watu katika jambo lolote punguza imani ya kuamini watu ili kuepeuka kuumizwa na kupoteza pesa.

Watu wengi wameumizwa kipesa na kimapenzi na watu waliowaamini, haijalishi ni mtu wako kiasi gani punguza kuamini watu kwa kuwa kuna watu wameumizwa na watu ambao walidumu nao katika biashara miaka kadhaa lakini mwisho wa cku waliwaibia.

Vifuatavyo ni visa vya watu kuumizwa na watu waliowaamini na hawa ni watu nawajuwa so ni visa vya kweli.

1. Miaka 5 nyuma rafiki yangu wa karibu nilimpa buku 10 hakunirejeshe mpaka leo.

2. Mdogo wangu Mwenge sokoni hapa Dsm alikuwa na rafiki yake wanafanya biashara ya viatu akamtuma mzigo kama mara 5 analeta bila shida, cku moja akamwambia amepata chimbo Kenya kuna bei nafuu dogoo akampa 3M mpaka leo miaka 5 jamaa hajarudi tena.

3. Mdogo wangu mwingine ana duka la Pharmacy Angola pharmacy mfanyakazi aliaminiwa akaingiza hasara ya milioni 17 aliiba kutokana na uzembe wa usimamizi.

4. Mfanyakazi staff moja alimpa dogo 250K za kitanda cha chuma 5×6 dogo akatengeneza cha kwanza kikawa hakifiti na godoro kikarudishwa atengeze kingine mpaka leo fundi katoroka kijiwe coz alikuwa na madeni mengine mwaka wa 2 sasa hayupo.

5. Mzee mmoja Moshi alikuwa na rafiki yake sana akampa mashamba yake kama dhamana achukulie mkopo Bank jamaa hakumaliza mashamba yule mzee mwaka juzi alikuwa anahaha mashamba yasiuzwe, na jamaa haonekani.

6. Muuzaji wa magari mtaani ukisikia kisa chake mpaka kushuka na kuingia kwenye madeni ya 1B ambayo kwa sasa amelipa bado kama milioni 100 baadhi ya hasara ni kuamini watu.

7. Unamtumia Manzi kwa kumuamini unatuma Nauli half haji.

8. Mwaka juzi niliingia hasara ya zaidi ya milioni 9 kwa kumuamini mtu, nilivyomshika nikapeleka polisi bahati mbaya AKAFA pesa nikapoteza utamdai marehemu???

9.Mwezi 7 nyuma rafiki yangu alimuazima mtu waliyezoea muda mfupi Laptop jamaa kamzurum na kahama mkoa.

10. Mjomba wangu kiukoo cku moja alipakia karanga gunia 100, wakafika njiani wakalala dreva kaamka ucku katoroka na mzigo, Ilikuwa Lori kalipiga mkono likasimama akapakia mzigo so hakuchukua tahadhari hata no za Gari.

11. Wanaume wengi tumelea mimba si zetu na watoto si wetu kisa kuamini wapenzi na wake zetu.

NDUGU WANA JF hii ni mifano michache kati ya mingi niliyonayo ambayo nimeona kwa macho yangu, unamuamini mtu mwisho wa cku anakuumiza.

WATU WENGI WAAMINIFU NDIYO HUWA WANAUMIZWA KWA KUWA HUHISI WATU WOTE NI WAAMINIFU KAMA WALIVYO WAO, KUNDI HILI HUUMIZWA ZAIDI ZAIDI.

Binafsi suala la kuamini watu nimeachana na kupunguza kwa asilimia 85%

Suala la kukopesha pesa mtu nimeacha mwisho nitakupa 30k hata ukinizurumu basi siyo issue.

Nasisitiza tena acha kuamini watu kupita kiasi, mtu unaweza kufanya naye biashara miaka 4 ila mwisho wa cku ukampa 30M asionekane tena.
Mada nzuri sana na imenigusa moja kwa moja. Sitawahi tena muamini mtu yoyote.
 
2019 nilimpa rafiki mkopo wa millioni 400 , mwamba alikuwa na hardware kubwa hapa dar , by then tumejuana since chuo , ilipofika miezi mitano baadaye muda wa malipo , aliingia mitini naskia siku hizi anabangaiza njombe na iringa, iliniuma sana kwa kuwa almost inipeleke bankruptcy then ,namshukuru mungu niliponea mufilis
 
Biblia inasema Amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu Yer:17:5,tatizo letu wanadamu hasa watz tunajiona wajanja hatutaki kufuata miongozo ya dini,Sheria za nchi.Naiomba srikali ishikilie hapo hapo kwenye tozo hadi tunyooke
 
2019 nilimpa rafiki mkopo wa millioni 400 , mwamba alikuwa na hardware kubwa hapa dar , by then tumejuana since chuo , ilipofika miezi mitano baadaye muda wa malipo , aliingia mitini naskia siku hizi anabangaiza njombe na iringa, iliniuma sana kwa kuwa almost inipeleke bankruptcy then ,namshukuru mungu niliponea mufilis
Pole Sana chief. You know many Stupid Black people ukikaa nao kweny story zao Ni eti Hakun tajiri alie fanikiwa bila dhuruma, wizi, utapeli, rushwa and the like

So wako wanafanyia hayo watu eti nao watengenez njia wafanikiwe. You can't imagine hio mindset ipo na ina pass kikazi na kizazi.
 
Itakuwa ulimloga,haiwezekani anabangaiza with 400mil,hebu elezea vizuri,najua utajitetea ni karma

Nimeamini mtu juzijuzi tu hapa kanichapa 300k. Jamaa rafiki yangu sana tumesoma wote ameishi kwangu kipindi ameyumba kidogo, lakin 300k imemshinda imani
Pole sana, na kibaya zaidi ukimdai inaonekana wewe ndiyo mbaya zaidi huna utu huna huruma yeye alilokufanyia haoni kama ni kosa.

Pole sana, ukata huu 300k si haba
 
Pole Sana chief. You know many Stupid Black people ukikaa nao kweny story zao Ni eti Hakun tajiri alie fanikiwa bila dhuruma, wizi, utapeli, rushwa and the like

So wako wanafanyia hayo watu eti nao watengenez njia wafanikiwe. You can't imagine hio mindset ipo na ina pass kikazi na kizazi.
yule alikuwa rafiki wa chanda na pete mpaka leo huwa najiuliza hyo hela tu ndiyo ilifanya ageuke, so sad
 
Mada nzuri sana na imenigusa moja kwa moja. Sitawahi tena muamini mtu yoyote.
Huo ndiyo uhalisia kaka, mtu asiyemuani ni ngumu kukuibia au kukuumiza maana hutampa nafasi kwa kitu au jambo lolote la dhamani, lakini mtu unayemuamini ni rahisi zaidi kukuumiza na kukufelisha kwa kuwa unamuamini.
 
2019 nilimpa rafiki mkopo wa millioni 400 , mwamba alikuwa na hardware kubwa hapa dar , by then tumejuana since chuo , ilipofika miezi mitano baadaye muda wa malipo , aliingia mitini naskia siku hizi anabangaiza njombe na iringa, iliniuma sana kwa kuwa almost inipeleke bankruptcy then ,namshukuru mungu niliponea mufilis
Mtu wako wa karibu sana ndiyo mwenye nafasi kubwa ya kukufilisi, kukuibia na kukuingiza katika matatizo kwa kuwa unamuamini na kumpa nafasi.

Visa vingi vya kuumizwa vinaanzia kwa watu tuliowaamini zaidi.

Tunapaswa kuaminiana ila punguza kuamini watu kwa vitu vikubwa kupita kiasi ambapo ikitokea kinyume na makubaliano bado utaweza kuhimili stress na changamoto hiyo
 
Itakuwa ulimloga,haiwezekani anabangaiza with 400mil,hebu elezea vizuri,najua utajitetea ni karma
wala sikumroga , wagamga nawajua matata ila yule mpaka watoto wake walikuwa God children wangu , harusi yake ya m,andugu zake zote nilikuwepo mpaka kwao walikuwa wananijua , mpaka watoto wetu walicheza pamoja sana tu .
sema sikutaka kumfatilia , nyumba zake ,magari mpaka biashara ilipigwa mnada na creditors , alifilisika kulingana na nijuavyo , sema then angenijia anipe ukweli tungecheki namna , mbona wakuu pale CRDB najuana nao wengine mpaka kesi nimewawakilisha , ila yy alitorokea kunakoni , binaadam bana acha tu
 
Pole Sana chief. You know many Stupid Black people ukikaa nao kweny story zao Ni eti Hakun tajiri alie fanikiwa bila dhuruma, wizi, utapeli, rushwa and the like

So wako wanafanyia hayo watu eti nao watengenez njia wafanikiwe. You can't imagine hio mindset ipo na ina pass kikazi na kizazi.
Hiyo mindset ya kijinga kabisa, huwezi kuendelea kwa kudhuruma hata siku moja
 
Mtu wako wa karibu sana ndiyo mwenye nafasi kubwa ya kukufilisi, kukuibia na kukuingiza katika matatizo kwa kuwa unamuamini na kumpa nafasi.

Visa vingi vya kuumizwa vinaanzia kwa watu tuliowaamini zaidi.

Tunapaswa kuaminiana ila punguza kuamini watu kwa vitu vikubwa kupita kiasi ambapo ikitokea kinyume na makubaliano bado utaweza kuhimili stress na changamoto hiyo
usemalo ni kweli , siku hizi imani ilikufa kabisa , hata watoto wangu huwa nawaangalia kwa mbali kwa ishu za pesa
 
2019 nilimpa rafiki mkopo wa millioni 400 , mwamba alikuwa na hardware kubwa hapa dar , by then tumejuana since chuo , ilipofika miezi mitano baadaye muda wa malipo , aliingia mitini naskia siku hizi anabangaiza njombe na iringa, iliniuma sana kwa kuwa almost inipeleke bankruptcy then ,namshukuru mungu niliponea mufilis
Umesema mia 4 ....aisee unapatikana wapi mkuu
 
watu mnakopeshana mamilion kizembe tuu...mimi 120k tu ilizama nikajifunza jambo ukiweza kumpa mtu hela mpe kiasi unachoweza kusamehe
 
Umesema mia 4 ....aisee unapatikana wapi mkuu
😂😂 tanzania ye2 tu hii , ila yule ni vile tulikuwa kama mandugu , tumebebana since chuo ,alifanikiwa mbele yangu kimaisha kwa muda nilikaa kwake , tukajuana muda , sema alivoniosha mpaka leo siamini
 
Hizi mambo za kukopesha ukipiga hesabu unajikuta umelaza pesa nyingi nje

Mwezi wa kwanza kuna kademu nilikakopesha 200k dalili ya kulipwa siioni saivi nafikiria nikatombe tu
 
Back
Top Bottom