Mchawi mmoja akakaa kiringeni kwenye kiti na kutamka,
Nakutuma Pepo mchafu, nenda kwa mtu yule( akamtaja jina),
Nenda jigeuze ewe Pepo uwe chuma, nenda kakae kwenye mguu wake, asiweze kutembea.
Mtu yule aliyetamkiwa maneno Yale, alikuwa amelala usingizi,
Alipoamka asubuhi, akajaribu kushusha mguu aende kujisaidia, hakuweza, mguu ulikakamaa, ukawa ngumu, haujikunji, maumivu alipata makali mno,
Hakujua kilichotokea alipolala, kumbe wabaya wakaweka chuma ndani ya mguu.
Semesha ugonjwa wowote wenye jina, utakusikia na kukutii kwa Jina la YESU.
Aamen