Jifunze kwa Ufupi Mashindano ya Pikipiki: MotoGP World Championship

Jifunze kwa Ufupi Mashindano ya Pikipiki: MotoGP World Championship

Utoto hawezi kuacha, siku mfatilie mwanzo mpaka mwisho kuna muda anaonyesha show off hata pasipotakiwa. Alipokuwa na Honda Repsol alikuwa na balaa sana.

Hata yule mwamba Quatararo siku hizi anakuwa nyuma itakuwa umri. Kwenye motogp kuna makabulu wa ki South wanacheza tangu miaka ya nyuma
Hahaha jamani Fabio umri umeenda? Kazaliwa 98 sijui 99 yule!? Nadhani ni pikipiki maana 2021 alikua vizuri sana alivitoka mreplace Rossi nadhani alichukua World Champion.

Sahivi dah kuingia top 10 tu haiwezekani.
 
na hadi leo top speech iliowahi kuonekana kwenye race ni 366 km/h.
Uwiiiih 366km/h hata ukigawia mbili bado sijawahi ifikia na ki'baiskeli' changu toka HONDA😄😄😄🤣

kwenye kona wanalala hivi, inayowasaidia kukata kali saaana wakiwa katika speed kali, sometimes utaona magoti yanagusa chini.
Waga ni utamu sana kuwacheki, hasa wakiwapiga slo-mo aaaah hadi nywele zinasimama
MotoGP ni more exciting kuangalia sana sometimes naonaga kuliko F1 sema marketing yake haifikii F1.
Exactly.
 
Wale wanaocheza Pro wanafanya kila mbwembwe mkuu, ukipata muda kamtizame akiwa anacheza Masoud, Juma, Babu Eddy. Beginners na Intermediate wapo wengi hao ndio wanacheza bila mbwembwe
Hawa wahuni kuna siku walipita pale university corner kuelekea Mwenge, yaani kuanzia pale Mataa hadi kufika usawa wa ile pacha ya Chuo kikuu walikuwa wanatembea na tairi moja huku la mbele wakiwa wameinua, halafu walikuwa speed balaa, Baja zilikuwa na sauti mzito kuteka attention ya kila mtu kuwatazama. Sijui waliishia wapi maana hadi wanapotea machoni bado walikuwa wanatembelea tairi moja.

NB: kipindi hiko, flyover ilikuwa haijajengwa.
 
Kati ya mbio za vyombo vya moto napenda kuangalia ni hii
Ila bado nashangaaga sana mtu ana dondoka na pkpk anainuka nduki hata kuvunjika hamna tech iliyo tumika hapo ni 🔥🔥🔥🔥
Jamaa wanavaaga vizuri, wana mavazi maalumu na safety standard nzito nzito.

Kiatu utakuta ni milioni kadhaa, helment ndo usiseme. Asikwambie mtu ukivaa vizuri ajali za pikipiki haziumizi kihiiivyo. Mie shahidi
 
Uwiiiih 366km/h hata ukigawia mbili bado sijawahi ifikia na ki'baiskeli' changu toka HONDA😄😄😄🤣

Waga ni utamu sana kuwacheki, hasa wakiwapiga slo-mo aaaah hadi nywele zinasimama

Exactly.
Hahaha hawa kwenye kona wako slow kuliko F1 ila kwenye straights bike zipo fast.

Brake discs zake zinafikaga hadi 150 degrees joto. Oya zile boda shikamoo
 
Hahah wale jamaa wana majeraha mwili mzima kama bodaboda wetu tu.

Sema ile suti wanayovaa aisee iko advanced sana kwenye protection. Gharama yake zaidi ya $5,000 za zingine zina hadi airbags.

Lasttime mtu amekufa kwenye ajali MotoGP sijui ni 2011 ile.
Halfu za kwao zinajazwa upepo tofauti na safety gear za kawaida,,, pia najiuliza wanapokata kona wanagusisha goti chini huwa ni style ya aina yake,, sijui wanavalisha nini kwenye goti
 
Hawa wahuni kuna siku walipita pale university corner kuelekea Mwenge, yaani kuanzia pale Mataa hadi kufika usawa wa ile pacha ya Chuo kikuu walikuwa wanatembea na tairi moja huku la mbele wakiwa wameinua, halafu walikuwa speed balaa, Baja zilikuwa na sauti mzito kuteka attention ya kila mtu kuwatazama. Sijui waliishia wapi maana hadi wanapotea machoni bado walikuwa wanatembelea tairi moja.

NB: kipindi hiko, flyover ilikuwa haijajengwa.
Hao wa kunyanyua tairi (wheelie boy) wao wanaita dede, wanakuwa convoy ya bike mbalimbali kuna wanaotumia bike sports na wengine bike za kawaida wamezifanyia mods.

Kila Jumapili walikuwa na ratiba ya kupita Tabata,Magomeni,kinondoni,msasani soko la samaki, wanaenda Kawe Tanganyika packers mpaka Mbezi kwa Zena
 
Shida mtu private kushiriki imagine gharama za maandalizi.
Wapo wanaoshiriki private, ila ni gharama sana. Hizo bike kwa vijana wa Bongo ni ghari kumiliki. Wengi wanacheza na bike za kuazima au kushare.

Bike za bajeti ya chini uanzie 7m,ukiiburuza haswa lazima ukimaliza rally upige Services kubwa ya tairi,rings,oil
 
Back
Top Bottom