Mahitaji
Mchele kikombe 1
Hiliki kiasi
Sukari 1/2-3/4
Yai 1
Tui la nazi vikombe 2
Hamira kijiko cha chai kimoja
Namna ya kutaarisha
1)Osha mchele na roweka hadi uwe laini kiasi.
2)weka mchele,hiliki,yai,hamira na tui la nazi kwenye blenda....saga hadi viwe laini
3)mimina kwenye bakuli...subiria uumuke
Namna ya kupika
1)weka chuma cha kuchomea(usitie mafuta) katika jiko moto kiasi... kikipata moto chota upawa mmoja wa mchanganyiko wako na mimina kwenye chuma chako...zungusha ili utandazike
2)funika na ufunikio juu..ukiona mkate wafanya vitundu tundu toa na weka pembeni.
3)fanya hivo hadi umalizie zilobaki
Mkate wa chila tayari kwa kuliwa