Jifunze njia nzuri ya kufanya manunuzi kwenye mtandao (Ebay, Amazon, Bestbuy)

Natoa hiyo huduma. Na mzigo wako utaupata popote ulipo. Hivi karibuni nitaweka Thread maalumu kwa kazi hii. Nitumie PM au email mw1rct(at)gmail.com
Mkuu lini utafungua huo uzi?
 
Asante ndugu kwa elimu yako nilikitamani kitabu fulani nikashindwa jinsi ya kukinunua lakini kwa muongozo huu naweza jaribu.Nikishindwa nitarudi kwako kwa muongozo zaidi.
 
Habari wana JF,

Kwa mwenye uzoefu na huu mtandao wa amazon.com; nahitaji kununua SONY A/V receiver. Kabla ya kununua ningependa kujua mambo yafuatayo:

1. Kodi ambazo nitalipa hapa Tanzania baada ya bidhaa kufika - ni kodi gani na kiasi gani? Hii bidhaa inauzwa USD 500.
2. Inachukua mda gani mpaka bidhaa inafika Tanzania mara tu baada ya kukamilisha malipo.
2. Je, naweza kuwatumia DHL?/Ni jinsi gani bidhaa itanifikia?

Naombeni ushauri/mwongozo kwa mwenye uzoefu na huu mtandao.
 
nami nasubiri muogozo huo,kuna vitu nataka kununua amazon na ebay ila nasita sita kufanya kwa mambo kama hayo
 
kaka vip hawa jamaa wanaoitwa alibaba
 
Tafadhali naomba mnifahamishe hili wakuu,nimeagiza mzigo belgium wa saa za mkononi kwaajili ya kuuza na nataka mzigo ufike dar kwa njia ya posta nimeambiwa anaenitumia ajiregista mzigo ndo utafika salama lakini ni kilo mbili mbili tu hubeba kwa njia ya regista kwaamana hyo Mzigo wangununagika kilo 4 nifunge box 2 kwa kilo 2 mbili sasa naomba mnifahamishe zaid juu ya hili na je ushuru utakuaje hapo utapofika bongo?

Wazee wa tra, Japo nimeambia kua nikishalipia kule hizo kilo 4 ni laki30 basi hapa silipi tena zaid ya kwenda kusign box na kuchukua lakini naombeni maoni yenu zaidi wakuu je hili ni la kweli?
 
Kuna thread kibao zilishawekwa humu jins ya kufanya manunuzi Ebay, ila kwa faida ya wengine nitarudia kwa kifupi ambavyo mimi natumia / naelewa, naamin wengine wataongezea kutokana na uzoefu wao.

kwanza kabisa kun online retails site kibao tofaut tofauti mfano Alibaba, Ebay, Amazon, Wadi na hata siku hiz bongo tuna Kyamu, JUMIA na kadhalika, anyway ziko nying ila utofauti unakuja na utendaj wao.

ndo maana unakuta Alibaba wanamrejesho mbaya kutoka kwa wateja hasa wa nje ya china maana mfumo wao kuthibiti matapel uko weak na wala hawako makin kushughulikia matatizo ya wateja kutapeliwa.. Alibaba inafanya vizur china sababu mtu akinunua anapata bidhaa yake halisi aliyonunua sababu wateja wengie wanatumia stail ya cash on delivery so hapo tapel hawez kumpiga maana kama utanunua online then muuzaj akutumie bongo usishangae kutumiwa nokia toch wakat umenunua iphone, kuna kesi nying zimefunguiliwa na watu kutoka nchi mbali mbali wakilalamikia kupokea bidhaa tofaut na walizonunua ama wanazipokea zikiwa tofaut na maelezo yalipo online, hasa kuhusiana na countefits, unakuta saa inauzwa unaambiwa ni Genuine Seiko ama swiss watch kumbe ni countefits ama isitumwe kabisa hapa nitazungumia kuhusu Ebay na Amazon ambao nina experience nao wa miaka zaid ya miaka minne

Kwa kifupi online retails sites nyingi zina act as a middle man kati ya muuzaj na mnunuaji, kuna online shops chache ambazo pia zinauza product wanazotengeneza wao wenyewe mathalan Amazon. ambao pamoja na kuwa kama mtu wa kati lakini pia wanauza baadhi ya product wanazotengeneza wenyewe kama vile Amazon TV, Amazon Tablet, Amazon E reader maarufu kwa jina la kindle, Amazon Phone inaitwa fire na vitu vingine vingi, lakin pia wanaruhusu watu kuuza bidhaa zao mpya ama used kupitia mtandao wao,

Ebay wao hawana bidhaa wanazotengeneza ila wanaruhusu muuzaj kuweza kutangaza na kuuza vitu kwenye webiste yao kwa malipo ya ada kidogo,

Ebay wanatumia Paypal katika swala la malipo ( ebay na paypal walikuwa kampuni moja ila ss hv wamesplit kwa sababu za kibiashara lakin bado ni sisters companies)

Amazon wao wanamfumo wao pia wa malipo

Muuzaj na Mununuaj wote wanatakiwa kuwa na Account kwenye hizi online shoopings website wakiweka details zao zote kuanzia physical Address had jinsi watakavyofanya malipo, kwenye malipo ni lazima ulipe kwa kutumia Credit card, zipo Tassi tofaut zinazotoa credit card ila zinazojulikana sana ulimwengu ni Mastercard na Visa, kwa hiyo unaweza ukatumia hizo ama ama nyinginezo wanazozikubali, unaweza ukafungua account ya hiz credit card kupitia Local bank yako, mfano Exim wanatumia Mastercard, CRDB , NBC wanatumia VISA card. ziko za madaraja tofaut kuanzia Silver had Gold

Kinachofanyika ni kuwa kama ww ni muuzaj ama Mnunuz unafungua Account na hiz retails mfano Ebay , Amazon na nyinginezo, kama ni Muuzaj bas unatakiwa kutangaza uhalisia wa Bidhaa zako iwe used ama Mpya , unakuwa unalipa kias kidogo cha fee kwa wao kukuruhusu kutangaza na kuuza bidhaa yako pale, ikitokea umeuza then pia kuna percent inaweza ikabak kwao. unapojisajili na kujaza namba yako ya credit card Ebay kupitia Paypal , na Amazon pia watajaribu kucharge kiasi kidogo za fedha ( mara nyingi ni Dola moja) kwenye hiyo account ilikujua kama ni legit na pia ww ndio mhusika, charges zikikubaliwa then ndo wata kuaccept kama legit seller ama buyer, na hiyo dola moja wanairudisha kwenye account yako.

MUUZAJI ANATAKIWA AWEKE TAARIFA KAMILI NA ZA KWEL KWA BIDHAA ANAYOUZA IKIAMBATANA NA PICHA IKIWEZEKANA, Ebay ama Amazon Watatumia hizo taarifa na mawasiliano kati ya Muuzaj na Mnunuz kuweka kutafuta suluhisho kama kutakuwa na Dispute kat yao

Mnunuaji ukinunua bidhaa online kinachotokea ni kuwa Ebay ama Amazon wanact kama vile Broker ama Mediator wa mnunuzi na muuzaji maana yake ni kuwa kama mnunuaji unalipa kupitia Amazon ama paypal kwa Ebay, then Amazon ama Ebay huwa hawamlipi muuzaj had pale utakapokuwa umepokea mzigo wako, ama anaweza kulipwa kabla lakini ikitokea mnunuaj akacomplain na wakajiridhisha kuwa muuzaj ana makosa unarudishiwa pesa yako na wao wana deal na muuzaj na ndio maana hawaruhusu makabidhano ya mkono kwa mkono hata kama mnakaa mtaa mmoja wanarecomend itumike njia ya kutumiana kupitia currier agencies kwani kule kutakuwa na proof of delivery,

Amazon na Ebay they are very secure and reliable , kwan tofaut na Alibaba wao huwa wanaweka mashart magumu kwa muuzaj kuliko mnunuzi, hii ni sababu hawatak kuchafuliwa jina maana ukitapeliwa itaonekana ni Ebay, wamejifunza kutokana na makosa ya zaman ndo maana ss hiv wako makini

NB: KUMBUKA KUSOMA DETAILS ZOTE ZA BIDHAA UNAYOTAKA KUNUNUA KAMA UNA WAS WAS MUANDIKIE EMAIL MUUZAJ KUPATA UFAFANUZI, EBAY NA AMAZON WATATUMIA MAWASILIANO YAKO NA DETAILZ ZA BIDHAA ILI KUPATA SULUHU YA DISPUTE YOYOTE NDO MAANA MAWASILIANO YA EMAIL YANAKUWA RECOMEND NA WALA SIO KUWASILIANA KWA NJIA YA SIMU.

Kwenye Website zote kuna jinsi ya kuwasilina na wauzaj kwa njia ya Emali ambapo Amazon ama Ebay wanapata copy ya kila Email exchange kat yenu kwa hiyo hata kama muuzaj aliongopa kwenye maelezo bas anakuwa kajifunga, na usifanye biashara na mtu anayetaka malipo yafanyike nje ya Amazon ama Paypal kwa upande wa Ebay, mathalan kutumia Western Union kwan western union haina jinsi ya ku claim kama umeletewa bidhaa feki

Kwenye manunuzi, ni kuwa tafuta bidhaa unayotaka kuinunua, angalia muuzaj anarecomend malipo kwa njia gani kama ni paypal then huyo atakuwa sio croocks, maana matapel wengi hawatak kutumia paypal kwan paypal inatoa upendeleo kwa munuaj kuliko muuzaj, hasa kukiwa na dispute , then unatakiwa usome kwa makin maelezo ya bidhaa husika mahali ilipo mda itakao chukua kukufikia na aina ya usafirishaj, ujiridhishe then utafanya malipo na kusubiria mzigo wako.

Cha muhimu ni kuhakikisha unaelewa bidhaa unayotaka kuinunua na unakubaliana na masharti ya muuzaj na staus ya kifaa kama ni used basi ni used kwa kiwango gani, maana kama kuna chembe chembe za u ignorance then utajikuta huna hak kama uta complain kuwa bidhaa sio yenyewe ama ina shida, wakat kumbe hukusoma maelezo ya muuzaj,

Kama huna uhakika acha tafuta nyingine, wauzaji wa bidhaa tofaut wako wengi. the trick to get a good deal kwenye onine shooping ni patience and reading reviews za watu waiowah tumia hizo bidhaa, uzuri ni kuwa wenzetu wakinunua bidhaa huwa wanazipa review na piwa wanacomment kuhusianan na muuzaj, kwani muuzaj credibility yake inapanda pale watu wanapocomment mazur kuhusiana nae . ndo maana utakuta mtu akikuuzia kitu anaomba umepe stars walau tatu ama tano kabisa kwani anajua wateja wanangalia mtu ana postive review kias gani.

Binafsi natumia Mastercard ya Exim, najua CRDB na NBC wao wanatumia VISA, siwez kuwazungumzia sana kuhusu huduma zao sababu sina experience nao ila kikubwa ni kuwa ni vizuri ukafungua Account ya credit card katika bank ambayo una account nayo tayar ya kawaida kwani itarahisha taarifa zako za kibank kuhamishwa kutoka acount moja kwenda nyingine,

Taratibu za ufugaji zinatofautiana, ila ni kuwa utachagua unataka credit card ya daraja lipi , kuna kuanzia Silver, Bronze na Gold, madaraja yanatofautiana viwango, Gold unaweza ukafanya transaction had milioni kumi, Bronze unaweza ukafanya transaction had ya milion 5, silver unaweza fanya transaction ya had milion moja, kumbuka transaction utakayoruhusiwa kufanya ni 80% ya thaman ya kad yako, kwa hiyo kama umechagua silver ya milion moja bas utaweza tumia laki nane tu,

Kwa mastercard ya Exim napata riba ya shilingi 10,000 kila mwez sijui kuhusu Visa za CRDB ama NBC ama Mastercard ya Barclays, na ukichelewa kulipa ( ku top up) account yako kuna penalt ya shlingi 5000, sijui kuhusiana na bank zingine.

Ukishafungua account ya credit card , na ukapatiwa card yako utalazimika kuisajili ionline kwenye mtandano wa tasis husika kama ni mastercard basi utalazimika kuisjaili humo, ili iweze kuwa activated, then baada ya hapo unaweza kuanza kuitumia.

Mfano kama unataka kujiunga na Paypal, jisajili na ingiza namba za credit card yako watacharge kiasi had cha dole mbili ili kujridhisah kama kweli account ni legit, then watairudisha hiyo pesa.

Huu utaratibu wa kucharge ni wakawaida kwa tassis zote zinazokubali kufanya online shopping, iwe paypal amazon ama Myus.

NB: Kuna tatizo la sisi ambao tumo Sfrica kushindwa kununua bidhaa nying kwa watumaj wachache ndo wanakubal kutuma africa wengine hawakubal.. ila kuna wajasiriamal ambao wako marekan wamefungua kampun inaitwa MYUS ukijiunga nao kwa ada ya dola 7 kwa mwez wanakupa address ya marekan ( kama sanduku la posta) ambayo utatumia kupokelea bidhaa zako..

Tuseme unataka kununua simu lakin muuzaj haitumi bongo basi ww unampa mtumaj addrss yako ya US then wale wa MYUS wakipokea wanakutaarifu na pia wanakuchagulia less expensive charges za kutuma bongo then wanakutumia .. unaweza ukawaambia waaubir
mizgo mingine ili watume kwa pamoja ama unaweza ukawamvia warudishe mzigo wau wakupigienpiha wakutumie .. wanatuma mizgo kokote dunian

NB: PAYPAL wameingia mkataba na bengi nyingi dunian ili kuwawezesha watu wanaofanya wanaouza bidhaa zao online waweze kulipwa kupitia Paypal na wao paypal wanadeposit moja kwa moja kwenye account ya muuzaj mara pale mzigo utakapopokelewa na mnunuaji, bahat mbaya tanzania bado so ukiuza kitu online mathalani pesa yako italipiwa kwenye paypal, basi hautaweza ichukua kupitia bank njia pekee utakayoweza tumia ni ww kuitumia tena hiyo pesa kwenye manunuz ya vitu, mwaka jana nilisoma mahali kuwa paypal wameingia mkataba na KCB ya kenya upande wa kenya ili waweze kupokewa fedha zao.

Nawasilisha.
 
Asante mkuu maelezo yako ni thamani sana,vp nikinunua mfano simu used marekani,ikifika bongo inabidi nilipie kodi?
 
Maelezo mazuri tena leo nilikuwa naulizia mambo haya haya ya Ebay. Sasa Nilitaka maelezo kidogo kama Nina Kadi ya Benki(ATM CARD) mi ninayo ya CRDB .. nataka iwe inatumika Kufanya Manunuzi Online.. inakuwaje?
 
Huku duniani sio lazima Credit card,card yoyote ya Bank unaweza jiandikisha Paypal
 
Huku duniani sio lazima Credit card,card yoyote ya Bank unaweza jiandikisha Paypal
Hapana si kadi yeyote.

Ni baadhi ya kadi. Kutegemea benki husika.

Mfano NMB wana kadi za zamani - ambazo huwezi kuzitumia paypal/ kufanya malipo katika mtandao.

ila kwa sasa wana card mpya za Visa/Mastercard utazoweza kuunga na Paypal/ Kufanya online transaction
 
Tumepishana lugha,ninaposema huku duniani,ina maana ni nje ya Tanzania, Kadi ya benki yoyote unatumia kunununua online
 
Asante mkuu maelezo yako ni thamani sana,vp nikinunua mfano simu used marekani,ikifika bongo inabidi nilipie kodi?

kwa sasa kuna uwezekano mkubwa wa kuilipia, mi niliagiza tablet na redio ya gar, ilibidi niilpie kod, ingawa kabla ya hapo ilikua nikilipia shipping bas mzigo naletewa had mlangoni na silipi chochote, ingawa nimesikia wanaanzia dola 50 kukata kodi, chini ya hapo hawakat, kikubwa unayenunua kwake aambatanishe na docs inayoonyesha bei aliyokuuzia, maana unaweza ukajikuta umenunua IPhone used kwa dola 200, lakin ndugu zetu wa pale customer yye akakupigia kodi ya iphone mpya dola 800, so kukiwa na docs inayoonyesha malipo halisi inasaidia
 
jamani tofautisheni kat ya debit card na credit card, kuwa na card yenye nembo ya mastercard ama visa card haimaniish ni kuwa unaweza kufanya online transaction. kuna card ambazo zimekuwa linked na mastercard ama visa card lakini huwez kufanya transaction online kwani zile ni debit card na sio credit card.

Debit unaweza kutumi kwenye ATM yeyote inayokubaliana na mtandao husika (mastercard ama VISA) bila kujali bank yako ama kulipia vitu kwenye merchant devices kama zile POS za kwenye supermarket . ila online transaction huwez fanya , credit card ndio unaweza fanya transaction online
 
Maelezo mazuri tena leo nilikuwa naulizia mambo haya haya ya Ebay. Sasa Nilitaka maelezo kidogo kama Nina Kadi ya Benki(ATM CARD) mi ninayo ya CRDB .. nataka iwe inatumika Kufanya Manunuzi Online.. inakuwaje?

kwanza hakikisha kuwa card yako ni credit card na sio debit card.. kama ulipofungua account wakakakupa form zao kujaza na wala hawakukwambia uka iactivate hiyo card online then card yako itakuwa ni debit card unatakiwa ufungue account ya credit card
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…