Jifunze njia nzuri ya kufanya manunuzi kwenye mtandao (Ebay, Amazon, Bestbuy)

Mkuu, ni upi usalama wa kulipa Aliexpress na Amazon kwa kutoa details zako za bank account?
Mifumo yote ni salama.

Alipay na Amazon Pay - Ni mifumo salama itumiwayo na aliexpress (alipay) na Amazon (amazon pay) kufanya manunuzi.

Ambapo mnunuzi unaweka taarifa zako za card na malipo yanafanyika kiusalama kabisa.

Kwa mifumo yote miwili, Seller hapewi fedha hadi pale wewe mnunuzi utakapo thibitisha kuwa umepokea mzigo
  • Iwapo mzigo hujapokea REFUND hufanyika na fedha inarudishwa kwenye kadi husika.
 
Appreciated Mkuu.
 
Naomba namba ya simu kuna kitu nataka kuagiza u.s.a
 
wakuu nataka niagize bidhaa kutoka alliepress, sasa changamoto imekuja kwenye malipo ya bidhaa ,bytheway mimi nina crdb card tu
kwa wajuzi wa haya mambo nisaidieni niopoe mzigo nje kwa mara ya kwanza kabisa mmi nina crdb card
 
Hivi Mkuu Mwl RCT sasahivi gharama ya ku-import vitu toka nje haijapanda sana maana naona magu amaebana vitu vingi sana hapo bandarini + sera yake ya v wonder nahisi ndio itakuwa balaa zaidi. Hali ikoje sasahivi???
 
Mmmh ngoja wajuvi wa hayo mambo waje
 
Hivi Mkuu Mwl RCT sasahivi gharama ya ku-import vitu toka nje haijapanda sana maana naona magu amaebana vitu vingi sana hapo bandarini + sera yake ya v wonder nahisi ndio itakuwa balaa zaidi. Hali ikoje sasahivi???
Inategemea mzigo na mzigo.
 
Naombeni kujua ni platform zipi naweza agiza bidhaa online na kulipia kwa kutumia mpesa, tigo pesa apa Tanzania tofauti na kikuu.com
 
Je kama hauna postal,ni njia gani nyingine ya kutumia kwa gharama nafuu sawa na posta ili mzigo ukufikie?

Wanasema mizigo mingi ikifika pale posta uibiwa, je ni kwel?

Je utaratibu wa kujua ushuru wa kitu ulichonunua au unachotaka kununua, uko vipi?

Je mzigo ukiibiwa pale posta, hela yko utarudishiwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…