Jifunzeni Siasa za Freeman Mbowe; Anachofanya Maria Sarungi ni ukosefu wa heshima kwa Mamlaka halali

Maria Sarungi, Mwanaharakati na Mwanachama hai wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo amekuwa akiendesha kampeni za kutukana na kudhalilisha Viongozi/Mamlaka halali kwenye mitandao ya kijamii kwa mgongo wa kudai katiba mpya.

Sio tatizo kudai anachokiamini, tatizo ni namna anavyoendesha hizo harakati zake, zimekuwa ni harakati za kutukana watu, kudhalilisha mamlaka halali na muda mwingine kubeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hakuna ubishi kuwa Mheshimiwa Freeman Aikeli Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema ni Mmoja wa Wanasiasa wa upinzani wenye mafanikio makubwa na historia itamuandika kwa wino wa dhahabu. Mbowe amekuwa wakati wote akikosoa, kushauri au kufanya harakati bila kudhalilisha au kutweza utu na heshima za watu wengine. Hawa wanaojiita wanaharakati wa mitandaoni ni bora wakajifunza na kuiga heshima na hekima ya Mwenyekiti wao.

Tunaweza kutoa dukuduku zetu bila kutukana, kukebehi au kudharau watu wengine na Serikali yetu ikasikiliza na kufanyiia kazi. Maria Sarungi, mamlaka unayoidhalilisha imewekwa na Wananchi. Serikali inafanya mambo mengi ya maendeleo haiwezekani kila siku wewe ni kukosoa tu as if hakuna Shule mpya zinazojengwa, barabara, miradi ya maji, hospital, vituo vya afya, miradi ya Umme, SGR, NHPJ, Elimu bure etc.

Tanzania ni nchi yetu, itajengwa na Watanzania.

Mungu ibariki Tanzania.

Mungu mbariki Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
The devil is in the details. Unaweza ambatanisha baadhi ya screenshots za hayo matusi ambazo alizipost huyo Maria?
 
Kigogo alikua anamtukana sana Magufuli mlikua mkishangilia.

Well inavyoelekea kama Taifa tumekubaliana kwamba matusi ndio njia sahihi ya kueleza matamanio yetu kwa viongozi.
Vikao gani hivyo tulivyokubaliana kama Taifa kuwatukana na kuwafedhehesha viongozi wetu wa Taifa?

Unajua nini huwa kinafuata baada ya matusi? Ukisikia watu wanatukanana, tarajia kinachofuata ni ngumu, matokeo, mitama na vingine vya Aina hiyo. Ndicho kweli tumekubaliana kama Taifa? Tutwangane ndipo tuheshimiane?
 
Mwanaharakati na Mwanachama hai wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo amekuwa akiendesha kampeni za kutukana na kudhalilisha Viongozi/Mamlaka halali kwenye mitandao ya kijamii kwa mgongo wa kudai katiba mpya.
  • Je tangu lini ni mwanachama wa hiko chama?
  • Je unao uthibitisho?
  • Rejea kauli yake ya Jun 5, 2022
==
1663322493180.png

==
Code:
Chanzo
https://twitter.com/mariastsehai/status/1533345700012081152?lang=en
 
Matusi hajawahi kujenga Nchi Stroke
Mamlaka halali huletwa na chaguzi za haki. Kilichofanyika uchaguzi wa SM 2019 na GE 2020 ni mjinga tu anaweza kusema hii ni mamlaka halali. Tunaposisitiza chaguzi za haki, lengo ni kuhakikisha kunapatikana heshima ya mamlaka hiyo. Unapopata mamlaka kwa njia za kihayawani, usitegemee kupata heshima usiyostahili.
 
Maria Sarungi, Mwanaharakati na Mwanachama hai wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo amekuwa akiendesha kampeni za kutukana na kudhalilisha Viongozi/Mamlaka halali kwenye mitandao ya kijamii kwa mgongo wa kudai katiba mpya.

Sio tatizo kudai anachokiamini, tatizo ni namna anavyoendesha hizo harakati zake, zimekuwa ni harakati za kutukana watu, kudhalilisha mamlaka halali na muda mwingine kubeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hakuna ubishi kuwa Mheshimiwa Freeman Aikeli Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema ni Mmoja wa Wanasiasa wa upinzani wenye mafanikio makubwa na historia itamuandika kwa wino wa dhahabu. Mbowe amekuwa wakati wote akikosoa, kushauri au kufanya harakati bila kudhalilisha au kutweza utu na heshima za watu wengine. Hawa wanaojiita wanaharakati wa mitandaoni ni bora wakajifunza na kuiga heshima na hekima ya Mwenyekiti wao.

Tunaweza kutoa dukuduku zetu bila kutukana, kukebehi au kudharau watu wengine na Serikali yetu ikasikiliza na kufanyiia kazi. Maria Sarungi, mamlaka unayoidhalilisha imewekwa na Wananchi. Serikali inafanya mambo mengi ya maendeleo haiwezekani kila siku wewe ni kukosoa tu as if hakuna Shule mpya zinazojengwa, barabara, miradi ya maji, hospital, vituo vya afya, miradi ya Umme, SGR, NHPJ, Elimu bure etc.

Tanzania ni nchi yetu, itajengwa na Watanzania.

Mungu ibariki Tanzania.

Mungu mbariki Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Mama amekuona subiri mkeka ujao unaweza kupewa u dc
 
Back
Top Bottom