Jifunzeni Siasa za Freeman Mbowe; Anachofanya Maria Sarungi ni ukosefu wa heshima kwa Mamlaka halali

Sasa maria ana matusi gani mbona akina shamu nginja huwalalamikii hafu ndo wenye matusi
 
Ukimuona adui yako anashangilia ujue kuna sehemu umekosea, lakini ukiona adui yako anapiga kelele ujue umemtwanga ahahaha( R.I.P JPM)
 
Sasa mbona unafanyo ndo Harakati zake
 
Huyu kamanda kwa hekima, busara na ustahimilivu ni mfano bora kabisa wa kuigwa hata kwa 'watesi' wake.
Umeandika vyema na umejenga hoja vizuri, naungana na wewe lakini umekosea kusema serikali hii imewekwa na wananchi, labda kama haukuwepo wakati Magufuli anaibaka na kuinajisi demokrasia.

Hakukuwa na uchaguzi 2020.
 
NONSENSE !!!!!!!!!! STOP IT.
 
M
koloni alijenga shule bora ya Tabora, MV Liemba na MV Victoria ambazo bado zinachapa kazi tukiacha Ikulu ya Dar es Salaam na bado aliondoka kwa heshima bila kuacha wafungwa wa siasa taka za kutunga, pia aliruhusu kila mtu amdai Uhuru bila woga na kesi za kubuma.
 

Maria sarungi sio mwana CHADEMA.
 
Kadi sio shida, Mtu anaweza asiwe na kadi ya CCM lakini bado akawa ni mfuasi wa CCM, Maria ni mfuasi kindaki ndaki wa Chadema.
Unampa ufuasi wa Chadema kwa sababu yeye anatetea haki kutamalaki kama ambavyo Chadema ni watetezi wa haki.
 
Kigogo alikua anamtukana sana Magufuli mlikua mkishangilia.

Well inavyoelekea kama Taifa tumekubaliana kwamba matusi ndio njia sahihi ya kueleza matamanio yetu kwa viongozi.
kwa maoni yako kosa moja lina halalisha kosa lingine au nimelewa vibaya?
 
Mungu akubariki kwa wale ambao hawajui historia hufikiri kuwa uhuru wa Tanzania kauleta Magu.
 
Wewe ndiye ulimpa Maria kadi ya Chadema?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…